Jibu la Swali: Mazungumzo kati ya Marekani na Iran
- Imepeperushwa katika Maswali ya Kisiasa
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Ufalme wa Oman, ambao unaendesha upatanishi katika mazungumzo ya Marekani na Iran, ulitangaza mnamo Alhamisi (kuakhirishwa kwa raundi ya nne ya mazungumzo ambayo yalipangwa kufanyika mnamo Jumamosi katika mji mkuu wa Italia, Roma, "kwa sababu za kiufundi," bila kutaja tarehe mpya. Al-Sharq, 1/5/2025). Mazungumzo ya awali yasiyo ya moja kwa moja kati ya Marekani na Iran yalianza mnamo tarehe 12 Aprili 2025 katika mji mkuu wa Oman, Muscat, kwa upatanishi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Badr Al-Busaidi.