Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 495
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Palestina haitakombolewa kwa kujifunza kuhusu historia yake. Kususia, kutengwa na vikwazo havitaikomboa Palestina. Palestina haitakombolewa kwa msaada wa chakula. Palestina itakombolewa wakati wana shupavu wa Umma katika majeshi ya Waislamu watakapowaasi watawala wasaliti, wakavunja minyororo yao na kuandamana kuelekea Al Quds.
Rais Sadyr Japarov alifanyia marekebisho sheria kuhusu “maliasili zilizo chini ya ardhi” na “maeneo yanayoishi viumbe hai (biosphere)” ambapo utafiti wa kijiolojia na utafiti katika maeneo ya yanayoishi viumbe hai (biosphere), uchunguzi wa kijiolojia wa rasilimali za dunia, uchimbaji wa akiba muhimu na kazi ya uchunguzi wa kijiolojia kwa rasilimali za chini ya ardhi zitafanywa kwa msingi wa uamuzi wa serikali.
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ulikutana afisini kwao mjini Port Sudan mnamo siku ya Alhamisi, tarehe 1 Dhul-Qi'dah 1445 H sawia na 9 Mei 2024 M, ukiongozwa na Ustadh Nasser Ridha, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan, na wanachama wa Hizb: Abdullah Hussein, Mratibu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano
Enyi Waislamu: Inatosha sasa. Ukatili unaofanywa na Mayahudi kwa watu, miti na mawe hauhesabiki! Sasa wanavamia kivuko cha Rafah, ambacho utawala wa Misri ulikichulia kuwa mstari mwekundu ambao haungekaa kimya kuhusu uvamizi dhidi yake.
Kutokana na mvua za msimu na mafuriko katika mikoa ya Kati na Kaskazini mwa Afghanistan, zaidi ya watu mia tatu wamepoteza maisha huku makumi ya wengine wakitoweka. Idadi kubwa ya nyumba na mashamba ya kilimo pia imeharibiwa.
Kutekwa nyara kwa Naveed Butt tangu tarehe 11 Mei 2012, ni dhambi kubwa na ukiukaji wa wazi wa haki za binadamu. Hakuna kesi ya ugaidi, uasi au uhaini iliyosajiliwa dhidi ya Naveed Butt. Zaidi ya hayo, hakuna kesi hata ya kumdhuru nzi, au kung'oa jani kutoka kwa mti, ya Naveed Butt mwenye huruma na mkarimu.
Hizb ut Tahrir / Uholanzi iliandaa maandamano katika mji mkuu wa Uholanzi, Amsterdam, kuinusuru Gaza, yenye kauli mbiu “Komesheni Mauaji ya Halaiki Mjini Gaza.” Maandamano hayo yalizunguka mitaa ya Amsterdam, yakisindikizwa na nyimbo za vijana wakitaka kunusuriwa kwa Gaza na kuhamasishwa kwa majeshi ya Waislamu.
Inasikitisha kwamba licha ya nchi za Magharibi kutekeleza jinai za kivita dhidi ya Mujahidina na Waislamu wa Afghanistan katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, utawala wa sasa unatafuta maingiliano ya karibu na wahalifu hao, huku ukifanya mikutano ya kisiasa na kiusalama na wanadiplomasia na maafisa wa usalama wa Marekani na Uingereza.
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia inaendeleza kuinusuru kwake Gaza ambapo mpaka sasa imeandaa matembezi 33 tangu kuzinduliwa cheche ya Kimbunga cha Al-Aqsa, na ina nia ya kuuamsha Umma na majeshi yake hadi wasimamishe dola la Uislamu aliyowafaradhishia juu yao Mwenyezi Mungu.