Jumamosi, 01 Safar 1447 | 2025/07/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  23 Muharram 1447 Na: 1447 / 02
M.  Ijumaa, 18 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Majanga na Maafa ni Matokeo ya Kimaumbile ya Kukosekana Dola yenye Kujali

(Imetafsiriwa)

Katika msururu wa ajali za mara kwa mara na moto wa kutisha-hasa ule moto wa ukumbi wa harusi wa mwaka 2023 huko Ninawi, ambao uligharimu maisha ya zaidi ya watu 120 na kujeruhi 200; moto wa mwaka 2021 katika Hospitali ya Al-Hussein huko Dhi Qar, ambao uliua zaidi ya watu 92; na moto wa mwaka 2021 wa kituo cha utengaji wagonjwa wa COVID-19 katika Hospitali ya Ibn Al-Khatib jijini Baghdad, ambao ulisababisha vifo vya watu 82-unakuja msiba mwengine tena wa kutisha. Moto mkubwa ulizuka katika soko kuu la Kut jioni ya Jumatano, 16 Julai 2025. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq ilithibitisha kuwa moto huo, ambao ulizuka ndani ya jengo la biashara la ghorofa tano katikati mwa mji wa Kut, uliwaua watu 61, ikiwa ni pamoja na miili 14 iliyoungua ambayo bado haijatambuliwa. Waathiriwa wengi walikufa kutokana na kuvuta moshi. Wizara hiyo iliongeza kuwa jengo hilo ambalo lilikuwa na mkahawa na kituo cha biashara, lilikuwa limefunguliwa kwa siku saba pekee.

Kujirudia kwa matukio hayo, kuundwa tu kwa kamati za uchunguzi, na matamko ya maombolezo bila kubainisha sababu za msingi au kuzuia kuenea kwake ni khiyana kubwa zaidi ya Ummah. Kila mtu anajua kuwa sababu za msingi ni kukithiri kwa ufisadi ndani ya dola, wingi wa mihimili ya maamuzi ya kisiasa, na wanasiasa kutelekeza wajibu wao wa kuchunga wananchi huku wakijikita katika kupora mali na kuhifadhi nyadhifa zao. Mamlaka zinazohusika hazina uwezo unaohitajika wa kukabiliana na moto na kuokoa familia zilizokwama kwa saa kadhaa. Aidha, vibali vya ujenzi na umiliki vilitolewa bila kuzingatia matakwa ya ulinzi na usalama. Kibaya zaidi majengo mengi yanajengwa bila vibali hata kidogo. Mifumo ya kuzima moto haipo katika majengo mengi ya serikali, na pale ilipo, mara nyingi imeharibika au haifanyi kazi. Kwa hivyo ni kawaida kushuhudia ongezeko hili la moto, ambalo linatokana na ufisadi wa kifedha, usimamizi mbovu, mapuuza, uzembe, na kukosekana kwa dola inayojali.

Enyi Waislamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ؛ فَالْأَمِيرُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ...»  “Kila mmoja wenu ni mchunga, na kila mmoja wenu ana wajibu juu ya raia wake. Na mtawala juu ya watu ni mchungaji na ataulizwa kuhusu raia wake...” [Imeafikiwa – al-Bukhari na Muslim]. Na kutoka kwa Mama wa Waumini, Aisha (ra), ambaye amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema nyumbani kwangu: «اللَّهُمَّ مَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئاً فَشَقَّ عَلَيْهِمْ فَاشْقُقْ عَلَيْهِ، وَمَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئاً فَرَفَقَ بِهِمْ فَارْفُقْ بِهِ» “Ewe Mwenyezi Mungu yeyote anayetawalishwa kusimamia mambo ya umma wangu na akawa mkali juu yao, kuwa mkali juu yake; na mwenye kutawalishwa kusimamia mambo ya umma wangu akawa mpole kwao, basi kuwa mpole kwake.” [Muslim] Hii ni Dua’a kutoka kwa Mtume (saw) dhidi ya yeyote ambaye anayechukua jukumu juu ya mambo ya faragha au ya hadharani ya Waislamu na kutenda bila ya mwongozo wa Muhammad (saw) na hivyo kuwadhuru.

Uongozi na kuwajali watu ni mzigo mzito na amana ambayo Mwenyezi Mungu atahisabu mtu. Haya ndiyo yalikuwa majibu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kama ilivyosimuliwa na Abu Dharr: Nikasema, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je, huniteui [wadhifa]? Akanipigapiga begani na kusema: «يَا أَبَا ذَرٍّ، إِنَّكَ ضَعِيفٌ، وَإِنَّهَا أَمَانَةٌ، وَإِنَّهَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ خِزْيٌ وَنَدَامَةٌ، إِلَّا مَنْ أَخَذَهَا بِحَقِّهَا وَأَدَّى الَّذِي عَلَيْهِ فِيهَا» Ewe Abu Dharr, wewe ni dhaifu, na hii ni amana, na Siku ya Kiyama itakuwa ni fedheha na majuto, na kuuchukua uongozi kwa haki yake na kutoa yale yanayostahiki kwake.” [Muslim]

Enyi Waislamu: Matukio haya na mengine mengi ni matokeo ya kimaumbile ya kukosekana uangalizi wa kweli wa mambo ya watu, na utawala wa mfumo mbovu uliosanifiwa na makafiri wavamizi, ambao sheria zao ziliwekwa na walinzi wao wafisadi wametiwa nguvu juu ya shingo za watu.

Suluhisho la maafa haya si katika kuonyesha huzuni, huruma, au matamko ya kuomboleza huku sababu kuu na chanzo cha mateso—mfumo potovu—kibaki bila kubadilika. Bali, suluhisho lipo katika kazi ya ikhlasi na bidii ya kuuondoa na kuweka mfumo unaotawala kwa Shariah ya Mwenyezi Mungu na kuangalia mambo ya watu kwa mujibu wa hukmu zake. Liko katika kumpa bayah Imamu mwadilifu ambaye anashambulia vikali dhidi ya aina zote za ufisadi, anakausha vyanzo vyake, na kukata mizizi yake—lengo lake kuu likiwa ni radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

[وَقُلِ اعْمَلُواْ فَسَيَرَى اللهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ وَسَتُرَدُّونَ إِلَى عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ]

“Na sema: Tendeni vitendo. Na Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini wataviona vitendo vyenu. Na mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhaahiri; naye atakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda.” [At-Tawbah:105]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 
E-Mail: hutiraq@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu