Jumamosi, 01 Safar 1447 | 2025/07/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:

Matembezi ya Halaiki ya Kuinusuru Gaza “Kuwahutubia wale Wanaohusika!”

Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa miezi 21, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi, kujeruhiwa na kupotezwa kwa zaidi ya wanaume na wanawake 200,000 Waislamu hadi sasa. Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki inaandaa matembezi makubwa ya halaiki kote nchini Uturuki.

“Tunaandamana hadi makao ya rais kwa ajili ya Gaza:

Je, muko tayari kuzungumza nasi kwa mtu anayehusika?”

Ambapo mashababu na wafuasi wa Hizb ut Tahrir/Wilayat Uturuki wataanza matembezi hayo kutoka makao makuu ya Chama cha Uadilifu na Maendeleo jijini Ankara kuelekea kwenye makao ya rais ili “kuzungumza na mwenye kuhutubiwa” kwa niaba ya Waislamu mjini Gaza, ambao wameachwa peke yao chini ya mzigo wa mauaji, kuzingirwa, na njaa kwa karibu miaka miwili.

Miezi 21 haswa imepita tangu uchinjwaji, mauaji ya halaiki, na ukandamizaji ulioanzishwa na umbile la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu katika Ukanda wa Gaza, kwa msaada wa Marekani na nchi za Magharibi. Tangu Oktoba 7, 2023, zaidi ya Waislamu 58,000 wameuawa shahidi na 137,000 wamejeruhiwa.

Kinyume chake, si utawala wa Uturuki, unaoongozwa na Erdogan, au tawala zozote za Kiarabu katika eneo hilo ambazo zimechukua hatua madhubuti kukomesha uvamizi na mauaji ya halaiki huko Gaza. Wala hawajafanya kazi hata kuhakikisha usambazaji wa misaada ya kibinadamu huko Gaza, na vifo vya watu wengi kutokana na njaa na kiu vimeanza.

Tangu Vita vya Kimbunga cha Al-Aqsa mnamo Oktoba 7, 2023, umbile nyakuzi la Kiyahudi limeendeleza jinai zake za mauaji ya halaiki, kukiuka sheria za vita na kanuni zengine zote, licha ya wito ambao tumeendelea kutoa; “Majeshi kwa Al-Aqsa” na “Muhammadshik hadi Gaza,” ambayo yanawataka viongozi kuchukua hatua madhubuti, na kutokana na kimya wa uziwi wa watawala ambao chini ya amri yao majeshi yanangojea, umbile la Kiyahudi linaendelea kufanya jinai za mauaji ya halaiki. Wakati Umma unatoa wito kwa watawala wake “kukusanya majeshi kuinusuru Gaza,” wanaendelea kujisalimisha na kukiuka Gaza kwa ajili ya Mayahudi wauaji na wale wanaosimama nyuma yao na kuwaunga mkono kwa fedha na silaha: Marekani, Magharibi, na mfumo wa kimataifa.

Kwa hiyo, sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki, tutaandamana kutoka makao makuu ya Chama cha Uadilifu na Maendeleo hadi kwenye makao ya Rais, kama sehemu ya jukumu letu, kuukumbusha Ummah wote kwa mara nyengine tena juu ya jukumu letu la kuchukua hatua za haraka za kuwanusuru Waislamu wanaodhulumiwa ambao wameachwa peke yao kwa zaidi ya siku 655, kina mama wanaowaaga watoto wao kwa njaa, na maiti za baba zao zilizochanika, na kuaga miili ya baba zao ambao waliuawa wakiwa katika mstari wa kusubiri kipande cha mkate.

Jumapili, 02 Safar Al-Khair 1447 H sawia na tarehe 27 Julai 2025 M

- Mahali na Wakati -

Mahali pa Kuanzia:

Matembezi yataanza kutoka makao makuu ya Chama cha Uadilifu na Maendeleo jijini Ankara na kuwasili katika Makao ya Rais (Chuo cha Urais)

Siku na tarehe:

Jumapili, 02 Safar Al-Khair 1447 H

sawia na 27 Julai 2025

Saa:

Saa 7 Adhuhuri saa za Madina (saa za Ankara)

- Video ya Ualishi wa Amali -

- Alama Ishara za Amali -

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

#ArmiesToAqsa

#AqsaCallsArmies

Kwa Maelezo zaidi, Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:

Tovuti Rasmi: Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Facebook: Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Twitter: Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Instagram: Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

YouTube: Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Jarida la Koklu Degisim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu