Alhamisi, 22 Muharram 1447 | 2025/07/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Kukamatwa kwa Ndugu yetu Al-Munawar Hakutabadili Uhalisia wa Vita vya Kipuuzi nchini Sudan

Jana asubuhi, Jumanne, tarehe 19 Rabi` al-Akhir 1446 H sawia na 22/10/2024 M, chombo cha usalama kilimkamata Ndugu Al-Munawar Dafallah Mustafa, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, kutoka nyumbani kwake katika mtaa wa Al-Sharif Al-Aqab katika mji wa Al-Qadharif, kwa misingi ya majadiliano katika kundi la WhatsApp, ambapo Ndugu Munawar alieleza uhalisia wa vita vinavyoendelea nchini Sudan, kwamba ni mzozo kati ya nguzo mbili za ukoloni; Amerika na Uingereza.

Soma zaidi...

Kuikomboa Palestina na Kuwanusuru Watu Wake Ni Jukumu la Lazima kwa Jeshi la Kinanah – Misri

Tunaukumbusha Ummah kwamba kadhia ya Palestina ndio shina lake na linapaswa kubaki katikati ya mazingatio yake. Wajibu wa halali kuhusu matendo ya umbile la Kiyahudi haupaswi kufungika kwa kulaani au kupinga pekee; badala yake, inatoa wito wa hatua za dhati na za kivitendo ili kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa.

Soma zaidi...

Sakata ya Genge la Watoto Wachanga nchini Uturuki

Maelezo ya kutisha ya sakata ya “genge la watoto wachanga” nchini Uturuki yametikisa taifa. Watu, wakiwemo madaktari, wauguzi na wafanyikazi wa hospitali, walifanya njama ya uhamishaji watoto wachanga wagonjwa hadi hospitali za kibinafsi kwa pato la kifedha. Angalau watoto 12 walipoteza maisha kutokana na vitendo vya genge hilo, kwani utunzaji muhimu ulipuuzwa kwa ajili ya faida. Kutokana na uhalifu huu wa kutisha uliopangwa, washukiwa 22 kati ya 47 walikamatwa, hospitali 10 za kibinafsi jijini Istanbul zilifungwa, na katika siku zilizofuata, ilifichuliwa kuwa uhalifu huu ulifanyika katika majimbo mengine manne.

Soma zaidi...

Firauni Rahmon Awawinda Vijana wa Kiislamu nchini Tajikistan

Majaribio ya dhalimu Rahmon ya kusitisha mwamko wa Uislamu miongoni mwa watu yanafanana na wazimu wa Firauni wa Misri. Baada ya kujua juu ya utabiri kwamba maangamivu yake yangetoka kwa mwanamume aliyezaliwa kati ya wana wa Israeli, Firauni, akiwa ameshikwa na hofu, aliamuru wavulana wote wanaozaliwa wauawe. Askari wake waliwaua kikatili watoto wachanga wa kiume, bila kumsaza yeyote.

Soma zaidi...

Shirika la Ushirikiano la Shanghai ni Sehemu ya Mfumo wa Dunia wa Amerika

Hizb ut Tahrir imeeleza kwa kina katika “Utangulizi wake wa Katiba,” kwa nini Waislamu hawaruhusiwi kusalimu amri kwa mfumo wa dunia wa Marekani. Inasema, “Umoja wa Mataifa umeanzishwa kwa misingi ya mfumo wa Kibepari, ambao ni mfumo wa Kikafiri, na zaidi ya hayo ni chombo kilicho mikononi mwa dola kubwa, hasa Marekani, ambayo inakitumia kwa ajili ya kulazimisha ushawishi wake juu ya mataifa madogo, ambayo dola za sasa katika Ulimwengu wa Kiislamu ni sehemu yake.”

Soma zaidi...

Gaza: Mwaka Mmoja ndani ya Mauaji ya Halaiki, Na Hakuna Msaada kutoka kwa Vikaragosi vya Magharibi

Ni dhahiri kwamba mwaka mmoja baada ya kuanza kwa mauaji ya halaiki, viongozi wa Waislamu hawajaweza kukata kamba wanazoshikilia mabwana zao. Kwa kufanya hivyo wanauthibitishia Ummah kwamba wao hawasimami pamoja na Waislamu. Wanasimama na pamoja uvamizi, na dola za Magharibi. Kwa hiyo ni wakati wa Ummah kuamka kama kizazi kipya. Ni wakati wa Umma kuungana chini ya Dini moja, bendera moja, kiongozi mmoja. Ni wakati wa sisi kuacha kuomba amani na usitishaji vita na kuanza kuitisha suluhisho halisi.

Soma zaidi...

Mkutano wa SCO jijini Islamabad: Siasa za Jiografia ndani ya Kivuli cha Uhasimu wa Marekani na China

Chini ya ulinzi mkali jijini Islamabad, Mkutano wa 23 wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai (SCO) ulianza kwa kishindo cha kawaida. Mkutano huo uliohudhuriwa na dola zenye nguvu kama China, Urusi, India, Pakistan, Iran na baadhi ya jamhuri za Asia ya Kati, ulimalizika kwa kutiwa saini hati nane, zinazohusu bajeti ya shirika hilo, shughuli za sekretarieti ya SCO, na juhudi za kukabiliana na ugaidi katika kanda. Jambo kuu lililoangaziwa lilikuwa ni kuidhinishwa kwa China kama Mwenyekiti kwa kipindi cha 2024-2025.

Soma zaidi...

Dhalimu Hasina ameanguka, lakini Washirika wake Waaminifu wa Kihindi bado wapo na wanaendelea kueneza Uzushi dhidi ya Hizb ut Tahrir

Tungependa pia kusisitiza kwa Inspekta Jenerali wa Polisi wa Bangladesh Bw. M Mainul Islam kwamba unashikilia wadhifa wa uwajibikaji unaotaka kuzingatia ukweli halisi. Baada ya kumpindua dikteta Hasina, watu wa nchi yetu hakika hawatarajii uongo wa wazi kutoka kwa wadhifa wako kama vile maafisa wa kutekeleza sheria walivyofanya wakati wa utawala wa dhalimu Hasina.

Soma zaidi...

Mswada wa Marekebisho ya 26 ya Katiba: Chini ya Khilafah, Madaraka na Mamlaka Vinaamuliwa na Qur'an Tukufu na Sunnah, Wakati Kuna Mivutano ya Kuendelea ya Madaraka Chini ya Demokrasia

Chini ya mfumo tawala wa Demokrasia, mzizi halisi wa ufisadi ni uwezo wa walio wengi waliochaguliwa kubadili kila sheria, kila kifungu cha katiba, kila kanuni na kila agizo. Nguvu ya kutunga sheria inavipa vikundi tawala uwezo wa kubadilisha sheria kulingana na maslahi yao, sio tu kupitia mlango wa nyuma, lakini kupitia mlango wa mbele. Nguvu ya sheria ndiyo inayoliruhusu Bunge kuhalalisha wizi unaofanywa na waporaji na wafujaji kupitia Sheria ya Maridhiano ya Kitaifa, kukubali kunyang'anywa madaraka na madikteta kwa nguvu, kupitisha mipango kadhaa ya msamaha kwa mirengo inayotawala na kutoa kinga ya kikatiba ya kutoshtakiwa kwa wale wanaohusika na mambo muhimu zaidi ya nchi.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu