Jumamosi, 17 Muharram 1447 | 2025/07/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  15 Muharram 1447 Na: 01 / 1447
M.  Alhamisi, 10 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Usaliti wa Watawala wa Pakistan na Kukumbatia Kwao Uhalalishaji wa Mahusiano:

Utangulizi wa Kujiunga na Mkataba wa Khiyana wa Abraham na Kutumikia Maslahi ya Amerika ya Trump na Umbile la Kiyahudi

(Imetafsiriwa)

Marekani ya Trump sasa inajitahidi kuunda "Mashariki ya Kati Mpya," ambayo inatumikia maslahi ya Marekani katika kanda hiyo, shauku kuu ikiwa ni kuhakikisha amani, usalama, na upanuzi wa kambi ya kijeshi ya Amerika katika Ulimwengu wa Kiislamu, inayojumuishwa ndani umbile la Kiyahudi. Inatafuta kuliweka umbile la Kiyahudi kama mamlaka kuu katika eneo hilo kisiasa, kiuchumi, na kimfumo. Licha ya haya yote, vibaraka wa Amerika ya Trump wamekimbilia kutekeleza mradi huu, na kutumikia maslahi ya bwana wao.

Hili lilianza na watawala ovyo wa dola za Ghuba na Sudan, na anayewafuata katika njama hii sasa ni Mkuu wa Majeshi wa Pakistan, Asim Munir, ambaye alifuja ushindi uliopatikana na Mwewe wa Jeshi la Anga la Pakistan dhidi ya adui mkubwa wa Pakistan, India. Munir kisha akamteua muuaji wa Gaza, Lebanon na Iran, Rais wa Marekani Donald Trump, kwa Tuzo la Amani la Nobel. Kiongozi wa umbile la Kiyahudi alivutiwa sana na wazo kwamba yeye pia, alimteua Trump, lakini kwa "Tuzo la Nobel la Vita," sio la amani.

Sasa zamu imefika kwa vibaraka wa kisiasa nchini Pakistan kuandaa njia ya utekelezaji wa mradi huu muovu. Msaidizi Maalum wa Waziri Mkuu wa Masuala ya Kisiasa, Rana Sanaullah, alisisitiza kwamba Pakistan inapaswa kufuata msimamo wa Ulimwengu wa Kiislamu kuhusu Mkataba wa Abraham, akisema "Ikiwa Saudi Arabia, Uturuki na Iran zitafanya uamuzi, na nchi za Kiarabu zilizoathiriwa moja kwa moja na suala hili zitafanya uamuzi, basi Pakistan inapaswa kukubaliana nao." Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje Ishaq Dar na Waziri wa Ulinzi Khawaja Asif walisisitiza kwamba Pakistan haitajiunga na makubaliano hayo, wakisisitiza kwamba utambuzi wowote wa "Israel" utagongana na uungaji mkono wake wa muda mrefu kwa suluhisho la dola mbili, na unaweza kuzingatiwa tu ikiwa utatumikia maslahi ya kitaifa ya Pakistan.

Licha ya uhalisia uliofichuliwa wa "Mkataba wa Abraham" ulioanzishwa na Marekani mnamo 2020 ambao ulifungua njia ya udhalilifu na khiyana ya uhalalishaji mahusiano wa Imarati (UAE), Bahrain, Oman, na Sudan, ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kwa balozi, kusainiwa kwa mikataba ya biashara, na ushirikiano katika teknolojia, watawala hawa waliojitenga na Ummah huu wanaendelea kukanyaga aqida ya watu wa Pakistan, na kujitenga kwa wazi kwa Nabii Ibrahim (as) kutoka kwa Mayahudi na Manaswara. Kama anavyosema Mwenyezi Mungu,

[مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَكِنْ كَانَ حَنِيفًا مُّسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ]

Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina.” [Surah Aali Imran: 67].

Bado watawala hawa wangali wanajitayarisha kujiunga na “Mkataba wa Abraham” mapema zaidi kuliko baadaye, wakidai kwamba watafuata pindi tawala nyengine katika Ulimwengu wa Kiislamu zitakapochukua uongozi, kama vile vibaraka wa Marekani waliopewa mafunzo na Uingereza katika Nyumba ya Saud, watawala wa Iran, na wanafiki wa Uturuki, wakiongozwa na mnafiki mkuu Erdogan. Kwa kufanya hivyo, wanachagulia kuwa wafuasi vipofu tu, kinyume na kauli ya Mtume wetu Mtukufu (saw) aliyesema, «لَا تَكُونُوا إِمَّعَةً تَقُولُونَ إِنْ أَحْسَنَ النَّاسُ أَحْسَنَّا، وَإِنْ ظَلَمُوا ظَلَمْنَا، وَلَكِنْ وَطِّنُوا أَنْفُسَكُمْ، إِنْ أَحْسَنَ النَّاسُ أَنْ تُحْسِنُوا، وَإِنْ أَسَاءُوا فَلَا تَظْلِمُوا»ۡ ‘Msiwe wafuasi vipofu (Imma’ah), wenye kusema: ‘Watu wakifanya mema, na sisi tutafanya mewa, na wakidhulumu, na sisi tutadhulumu.’ Bali zitieni adabu nafsi zenu, pindi watu wakifanya mema, fanyeni mema, na wakifanya maovu msifanye maovu.” (Tirmidhi)

Kupotosha uhalisia na kuonyesha kushindwa kama ushindi, kama vile walivyotapanya ushindi wa simba wa jeshi juu ya India, wakiipena Kashmir, na kufumbia macho usitishaji wa India wa Mkataba wa Maji wa Indus, kisha kutangaza hilo kuwa ni "ushindi," ambalo kwalo Mkuu wa Majeshi alipandishwa cheo hadi ngazi ya "Field Marshal" na mtawala wa Pakistan. kinachojulikana kama "suluhisho la dola mbili." Wanawasilisha msimamo huu kama wa heshima, wakati kwa hakika, mradi huu unaimarisha uwepo wa umbile la Kiyahudi kwenye zaidi ya 80% ya Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, na unauzwa kwa watu kama ushindi. Wanafanya kama vile msaliti mkubwa, Yasser Arafat alivyofanya, katika Makubaliano ya kisaliti ya Oslo, ambapo alikubali uvamizi wa Kiyahudi wa Ardhi Iliyobarikiwa, kwa badali ya Mayahudi kuitambua dola ya Palestina chini ya 20% ya Ardhi Iliyobarikiwa!

Enyi Waislamu wa Pakistan, haswa nyinyi, mashujaa miongoni mwa majeshi! Watawala wenu wa kisiasa na makamanda wa kijeshi wametangaza waziwazi utiifu wao kwa Mayahudi na Manaswara. Wamekuwa askari katika majeshi ya Trump na Netanyahu, wasio na haya katika kutia saini makubaliano yoyote yanayowatumikia mabwana zao, hata ikiwa ina maana ya kuritadi kutoka kwa Uislamu, na kufuata dini yao mpya ya "Ibrahim", au kusalimisha Kibla cha Kwanza na wa tatu ya Masikiti Mitatu Mitakatifu, Al-Masjid Al-Aqsa.

Khiyana hii ya kimakusudi si chochote ila ni matokeo ya uaminifu wao kwa maadui wa Ummah. Hata kama wanazungumza lugha yenu na wanasoma Qur’an Tukufu, hao ni miongoni mwa wanafiki ambao Mwenyezi Mungu (swt) alituonya kuwahusu. Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Surat Al-Munafiqun,

[وَإِذَا رَأَيْتَهُمْ تُعْجِبُكَ أَجْسَامُهُمْ وَإِنْ يَقُولُوا تَسْمَعْ لِقَوْلِهِمْ كَأَنَّهُمْ خُشُبٌ مُّسَنَّدَةٌ ۖ يَحْسَبُونَ كُلَّ صَيْحَةٍ عَلَيْهِمْ ۚ هُمُ الْعَدُوُّ فَاحْذَرْهُمْ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّهُ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ]

Na unapo waona, miili yao inakupendeza, na wakisema, unasikiliza usemi wao. Lakini wao ni kama magogo yaliyo egemezwa. Wao hudhania kila ukelele unao pigwa ni kwa ajili yao. Hao ni maadui; tahadhari nao. Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?[Surah Al-Munafiqun 4].

Lazima muwashike mikono yao, muwapindue, na mumpe Bay’ah yenu ya utiifu Khalifa Rashid (Khalifa Muongofu) ambaye anatawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt), na kuukomboa Msikiti wa Al-Aqsa na eneo la Israa na Miraj ya Mtume (saw), na kuliregesha bara dogo zima la India kwenye zizi la Ummah, chini ya bendera ya Tawhid inayounganisha Ummah wa Kiislamu bilioni mbili wenye nguvu chini yake.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu