Jumatano, 21 Muharram 1447 | 2025/07/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hotuba ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan katika Mkutano na Waandishi wa Habari kwa Anwani: Makubaliano ya Entebbe, Bwawa la Al-Nahdha, na Kupuuza kwa Watawala Maslahi Muhimu ya Ummah

Makubaliano ya Entebbe ambayo yanaonyesha wazi njama dhidi ya haki za maji za Misri na Sudan, kiwango cha uzembe wa watawala wa Misri na Sudan, na msimamo wao dhaifu kuelekea njama zinazofanyika.

Soma zaidi...

Udanganyifu wa Chaguo: Kwa nini Upigaji Kura katika Mfumo wa Kisekula Unawabwaga Waislamu

Jamii ya Kiislamu ina majukumu muhimu, ndani na kimataifa. Ndani ya nchi, Waislamu wanapaswa kuunda majukwaa yao ya kisiasa, si kwa madhumuni ya kupiga kura, bali kuimarisha kitambulisho cha Kiislamu, kujenga mafungamano ya jamii, na kushiriki katika dawah. Kwa kushughulikia masuala ya kijamii kama vile ukosefu wa makao, mwanya wa kiuchumi, na maadili ya kifamilia, Waislamu wanaweza kuonyesha masuluhisho ya Uislamu kwa matatizo ya kijamii, wakiyawasilisha kama jibu kwa changamoto za kisasa. Uwepo imara wa Waislamu, katika jamii na kwenye mitandao ya kijamii, unaweza kushajiisha kutafakari juu ya hekima ya mafundisho ya Kiislamu.

Soma zaidi...

Makala ya Hivi Punde ya New York Times ni Mfano Mwingine wa Mkakati wa Kugawanya wa Marekani Miongoni mwa Mujahidina wa Afghanistan

Mnamo Oktoba 24, The New York Times ilichapisha makala kutokana na mahojiano na Waziri wa Mambo ya Ndani wa sasa wa Afghanistan, ikiwa ni pamoja na moja yenye kichwa, “Je, Mwanamgambo Aliyetafutwa Zaidi Afghanistan Sasa Ni Tumaini Lake Bora la Mabadiliko?” Makala hizi zinalenga kuleta mgawanyiko na kuwaelekeza baadhi ya Mujahidina katika maslahi ya Marekani.

Soma zaidi...

Kuanguka kwa Kile Kilichosalia cha Jani la Mtini Lililochakaa ambalo Hadhara ya Magharibi Inafikiri Inaficha Aibu Yake!

Kazi ya kulizika zimwi hili ni wajibu kwa Umma wa Kiislamu, kwani ndio mmiliki wa hadhara badali iliyostaarabika ambayo inaweza kwa sifa zote kuuendeleza wanadamu kwa maadili ya kibinadamu ambayo Mwenyezi Mungu amewachagulia watu wote. Umma lazima uasisi chombo cha kisiasa ambacho kinawakilisha hadhara ya kimungu ya Kiislamu ambacho, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, itaiondoa batili na kuipa ushinda haki. Hivyo basi, watu wote wenye ikhlasi katika Ummah lazima wafanye kazi ya kusimamisha Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume kwa kuyataka majeshi ya Waislamu kukata mikono ya Magharibi katika nchi zetu.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan: Mkutano na Waandishi wa Habari “Makubaliano ya Entebbe, Bwawa la Al-Nahdha, na Kupuuza kwa Watawala Maslahi Muhimu ya Umma”

Hizb ut-Tahrir / Wilayah Sudan ilifanya mkutano na waandishi wa habari mnamo siku ya Jumamosi tarehe 23 Rabi’ al-Akhir 1446 H sawia na 10/26/2024 M katika afisi yake mjini Port Sudan, wenye kichwa: “Mkataba wa Entebbe, Bwawa la Al-Nahdha, na watawala kupuuza maslahi muhimu ya Umma”.

Soma zaidi...

Viumbe Vidhalilifu Zaidi Vyatishia na Kuahidi! Je, Mtajibu Vipi?

Ulimwengu mzima umeshuhudia athari kubwa ya Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa kwa jeshi la umbile la Kiyahudi, ambalo lilijivunia nguvu, uwezo, ufikiaji, na uwezo wake wa kijasusi, hadi wakawadanganya walimwengu kwamba wao ndio jeshi lisiloshindwa na kwamba wao ndio wenye nguvu kuu katika Mashariki ya Kati, mlinzi wa maslahi ya Magharibi katika kanda hiyo, na kiongozi wa Amerika na Uingereza.

Soma zaidi...

Jibu la Swali: Hukmu ya Miamala ya Kifedha na Kibiashara kupitia Mtandao wa Intaneti

Je, ni ipi hukmu ya biashara, kwa mfano, kununua dinari, mafuta, dhahabu nk kwa dolari wakati wa bei nafuu, kisha kuiuza kwa wakati wa bei ya juu ili kupata faida, huku ukijua kwamba yote haya yanapatikana kwenye mtandao, na anaweza kuhamisha pesa benki na kuzitoa wakati wowote anapotaka?

Soma zaidi...

Umbile la Kiyahudi Halitanusurika na Mashambulizi ya Makombora ya Khilafah Rashida

“Picha za satelaiti za shabaha mnamo siku ya Jumanne – kambi ya anga ya Nevatim kusini mwa ‘Israel’, nyumbani kwa ndege zake za kivita aina ya F-35-zinaonyesha kwamba zaidi ya makombora 32 ya Iran yaliweza kutua ndani ya eneo la kambi hiyo, kulingana na uchambuzi wa Profesa Jeffrey Lewis, katika Taasisi ya Middlebury ya Mafunzo ya Kimataifa huko Monterey, California.”

Soma zaidi...

Wale Waliotazama Moto wa Gaza Wamehukumiwa Udhalilifu!

Ikiwa Bw. Erdogan angekuwa mkweli, angejibu uwepo huu wa kigaidi kwa nguvu za kijeshi, mateso haya yasingetokea Gaza. Ikiwa kweli wewe ni mkweli, hutanyamaza tena kuhusu mauaji yanayofanywa na magenge ya Kiyahudi huko Gaza na Lebanon, bali utahamasisha jeshi. Kwa hivyo, kanda na jiografia iliyo chini ya moto itakomesha ukatili huu, na utafanya kile kinachohitajika hata ikiwa kimechelewa.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu