Afisi ya Habari	
				
				Wilayah Lebanon
			
| H. 11 Jumada I 1447 | Na: H.T.L 1447 / 11 | 
| M. Jumapili, 02 Novemba 2025 | 
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Katikati ya Mashambulizi ya Marekani kwa ajili ya Kuhalalisha Mahusiano na Kusalim Amri! Ziara Nyingine ya Mara kwa Mara ya Mjumbe wa Marekani Ortagus nchini Lebanon!
 (Imetafsiriwa)
Kwa kuzingatia mashambulizi ya Marekani dhidi ya Lebanon na eneo hili pamoja na mradi wa kuhalalisha mahusiano na kusalim amri, na juhudi za utawala wa Trump na timu yake kuwaleta watawala zaidi wa Waislamu katika Makubaliano ya Abraham, inakuja ziara ya mjumbe wa Marekani Morgan Ortagus nchini Lebanon na umbile nyakuzi la Kizayuni, iliyojaa shinikizo, vitisho, na hali za kisiasa, usalama, na kiuchumi zilizolazimishwa nchini Lebanon. Ziara hii iliambatana na ziara ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiarabu na Mkurugenzi wa Ujasusi wa Misri, ikionekana kutimiza lengo moja! Hapo awali, mjumbe wa Marekani Tom Barrack alielezea vitisho na mitazamo ya utawala wake kuhusu Lebanon na eneo hili kwenye jukwaa lake la X: “Ikiwa Beirut itaendelea kusita, Israel inaweza kuchukua hatua kwa upande mmoja – na matokeo yatakuwa mabaya sana,” Ili kukamilisha picha hii, kama Barrack alivyoielezea katika taarifa hiyo hiyo: “Lakini vipande viwili muhimu vya usanifu huu wa amani vinabaki kutokamilika,” alisema, akimaanisha Damacus na Beirut.
Kujibu ziara hizo, kauli, na vitendo vyengine, tunasema yafuatayo:
Kwanza: Uingiliaji kati wa Amerika na washirika wake katika ardhi za Waislamu unatumikia maslahi ya Amerika na umbile la Kizayuni, si maslahi yetu, hasa kwa vile Amerika ndiyo msaidizi mkuu wa umbile la Kizayuni katika siasa, uchumi, fedha, silaha, na vyombo vya habari, dhahiri na kwa uwazi.
Pili: Ziara ya mjumbe huyo siyo isiyo egemea upande wowote, kama wengine wanavyoweza kufikiria! Badala yake, inakuja ndani ya muktadha wa sera iliyo wazi ya Marekani katika eneo hili inayounga mkono umbile la Kizayuni na kuchangia katika uwezeshaji wake wa kijeshi na kisiasa. Kile ambacho mjumbe wa Marekani anawasilisha si chengine ila ni kulazimisha udhibiti, kuendeleza utiifu, na kupungua kwa ubwana. Ni aina ya kusalim amri na kujisalimisha kwa Wazayuni, na hili ni jambo ambalo Mwenyezi Mungu (swt) anaharamisha kwa Waislamu.
Tatu: Kukubali maagizo haya na kusaini makubaliano yoyote yanayoendeleza mamlaka ya kigeni ni usaliti kwa Mwenyezi Mungu (swt), Mtume Wake (saw), Ummah wa Kiislamu, na wale wote waliopigana au kujitolea ili kufukuza umbile hili nyakuzi kutoka Lebanon na Palestina.
Nne: Kuamiliana na umbile la Kizayuni kunachukuliwa kuwa uhalifu na idadi kubwa ya watu wa Lebanon, Waislamu na wasio Waislamu, si tu kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, bali pia chini ya sheria ya kisekula iliyotungwa na mwanadamu ambayo mamlaka za Lebanon zinaifuata, na hata chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu kwa jumla. Hili ni kweli hasa baada ya umbile hilo la jinai kufanya mauaji ya halaiki mjini Gaza, uhalifu ambao halijasita, na halitasita, kuurudia nchini Lebanon na ardhi zengine za Waislamu.
Tano: Kampeni ya Marekani na uvamizi dhidi ya eneo hili hautafanikiwa. Amerika haitafanikiwa katika juhudi zake za kuunda upya eneo hili kama inavyotaka. Ingawa inaweza kuwa na mradi wake kwa eneo hili, unaotegemea ukoloni, kuwapora watu, kuwapotosha Waislamu, na hata kuwapotosha kutoka kwenye Dini yao kwa kuwaita kwenye “imani ya Abrahim,” Waislamu, kwa upande wao, wana mradi wao wenyewe, ulioahidiwa kutawala na Mwenyezi Mungu (swt): mradi wa Khilafah ya pili kwa njia ya Utume. Mradi huu uko karibu sana, Mwenyezi Mungu akipenda, na ni mradi huu ambao utachora upya ramani ya eneo, na kwa hakika ulimwengu mzima kwa mara nyengine tena, ukitimiza bishara njema ya Mtume:
«إنَّ اللَّهَ زَوَى لي الأرْضَ، فَرَأَيْتُ مَشارِقَها ومَغارِبَها، وإنَّ أُمَّتي سَيَبْلُغُ مُلْكُها ما زُوِيَ لي مِنْها»
“Hakika Mwenyezi Mungu amenikusanyia ardhi na nikaziona pande zake za mashariki na magharibi, na watu wangu wataitawala sehemu zake zote zilizokusanywa kwangu yangu” [Imepokewa na Muslim].
Umbile la Kiyahudi litaangamizwa, kama Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alivyobashiri bishara njema katika Hadith yake:
«لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يُقَاتِلَ الْمُسْلِمُونَ الْيَهُودَ، فَيَقْتُلُهُمُ الْمُسْلِمُونَ...»
“Hakitafika Kiyama kabla ya Waislamu kupigana na Mayahudi na Waislamu kuwaua...” [Bukhari na Muslim].
Kwa kumalizia, Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Lebanon inaendelea kutabanni sera ya kuzima kampeni ya Marekani na mashambulizi yake dhidi ya Lebanon na eneo hili kwa njia ya kuhalalisha mahusiano na kusalim amri, na hakuna kitakachoizuia kutokana na hili. Tunaonya mamlaka za Lebanon dhidi ya kuendelea kwenye njia ya kuhalalisha mahusiano na kusalim amri! Tunawalingania watafute ulinzi kutoka kwa watu wao ili kukabiliana na hili, na wasibadilishe jambo hilo kwa kisingizio cha mipaka, ujenzi mpya, au ushawishi wa mfumo wa kimataifa.
[وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَىٰ أَمْرِهِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]
“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf: 21]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
 katika Wilayah Lebanon
|  Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Lebanon  | 
					
					 Address & Website  Tel: 009616629524 http://www.tahrir.info/  | 
					
										 Fax: 009616424695 E-Mail: ht@tahrir.info  | 
					



