Jumatatu, 28 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  26 Rabi' II 1447 Na: H.T.L 1447 / 09
M.  Jumamosi, 18 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ukamatwaji wa Wanachama wa Hizb ut Tahrir jijini Beirut!
(Imetafsiriwa)

Katika marudio ya mbinu na hatua za ukamataji holela wa vyombo vya usalama bila msingi wowote wa kisheria, wa watu—baadaye waliotambuliwa kuwa wanachama wa chombo cha usalama chenye mfungamano na serikali—wakiwa kwenye pikipiki waliwakamata wanachama wawili wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Lebanon walipokuwa wakigawanya taarifa moja ya kulaani kuendelea kwa uvamizi wa Kiyahudi dhidi ya Lebanon na watu wake. Kukamatwa huku kulitokea jana, 17/10/2025, baada ya Swala ya Ijumaa mbele ya Msikiti wa Imam Ali katika eneo la Tariq al-Jadida jijini Beirut.

Je, Lebanon, chini ya kipindi chake kipya chini ya uongozi wa kamanda wa zamani wa jeshi na jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki—aliyeahidi hali ya sheria—itadumisha mbinu za tawala zilizokufa? Ni kipi kilichowatia hofu kutoka kwa Hizb ut Tahrir? Je, ilikuwa ni kulaani kwake uvamizi wa Kiyahudi? Au mazungumzo yake juu ya njia ya serikali kuelekea uhalalishaji mahusiano na kusalim amri kunakosimamiwa na Amerika? Au wito wake wa kukabiliana na kampeni za Kiyahudi na Marekani nchini Lebanon na kanda? Au ilikuwa ni jaribio la kunyamazisha sauti licha ya madai ya mabadiliko ya mbinu za mamlaka hiyo na viongozi wake wa usalama wanaodai kufanya kazi ya kuweka sheria?

Kila mtu anajua kwamba Hizb ut Tahrir haitanyamazishwa na njia hizi, na uzoefu wao nazo nchini Lebanon na kwengineko unashuhudia hili. Hizb itaendelea kukabiliana na uvamizi wa Kiyahudi dhidi ya Lebanon na watu wake, na itakabiliana na dhihirisho lolote la kuhalalisha mahusiano au kusalim amri kwa mradi wa Amerika.

Tunadai mamlaka ikomeshe unyanyasaji huu dhidi ya kusema neno la haki na kutoa maoni ya kisiasa. Tunawataka wawaachilie huru mara moja na kwa haraka ndugu zetu Hassan Abdul Hadi na Salah Daoud bila kuchelewa au kukawia. Hizb ut Tahrir inajulikana kuwa ni nani, na njia yake ya utekelezaji wa kisiasa na mapambano kupitia maneno na hoja inajulikana vyema. Mamlaka hazina hoja ya kukamatwa kwao zaidi ya kuendelea na mbinu ile ile ya vyombo vya usalama, licha ya baadhi ya mabadiliko katika sura zao, lakini hakuna mabadiliko katika matendo na tabia yake!

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Lebanon, ambayo inawakilisha sehemu ya Waislamu, haitakubali kuwa shabaha rahisi kwa uvamizi wa vyombo vya usalama, ambavyo vinawapuuza wale wanaotishia amani ya Lebanon na watu wake kwa mantiki ya nguvu za kimwili, kisha kuja kuwaonea wale wanaopaza sauti zao kwa maneno, hoja, na hatua ya kisiasa.

[إِنَّ الَّذِينَ فَتَنُوا الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ الْحَرِيقِ]

“Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.” [Al-Buruj: 10]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 009616629524
http://www.tahrir.info/
Fax: 009616424695
E-Mail: ht@tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu