Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
| H. 8 Jumada I 1447 | Na: H.T.L 1447 / 10 |
| M. Jumanne, 28 Oktoba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Lebanon
Wamemtembelea Mheshimiwa Mbunge Dkt Osama Saad
(Imetafsiriwa)
Kwa kuzingatia shambulizi la Marekani dhidi ya Lebanon na kanda hii kupitia uhalalishaji mahusiano na kujisalimisha, na juhudi za Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Lebanon kuzuia shambulizi hili, ujumbe kutoka hizb, ukiwakilishwa na wanachama wa Kamati Kuu ya Mawasiliano na Kamati ya Amali katika Eneo la Kusini, ulimtembelea Mheshimiwa Mbunge Dkt. Osama Saad afisini kwake Sidon mnamo Jumatatu, 27/10/2025.
Ujumbe huo ulizungumzia mchakato wa uhalalishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi ambao Amerika inajaribu kuulazimisha juu ya Lebanon na kanda hii, na umuhimu wa kukabiliana nalo. Hivi ndivyo Hizb ut Tahrir inavyofanya. Kufuatia uzinduzi wa kampeni yake, vikosi vya usalama viliwakamata kiholela wanachama wake wawili katika mji mkuu, Beirut. Kuzuiliwa kwao kuliendelea kwa siku tano bila mashtaka yoyote ya kisheria au hati za kukamatwa!
Mheshimiwa Mbunge huyo alisema kwamba alikuwa amezungumzia mapema mada ya “amani” katika hotuba yake ya bunge mbele ya Bunge la Lebanon, katika kile alichokiita “amani ya kujisalimisha” kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano kusini mwa Lebanon mnamo 27/11/2024. Kwa kweli, katika siku za hivi karibuni, imekuwa amani ya kujisalimisha na utiifu. Mheshimiwa Mbunge huyo alilaani kukamatwa kwa wanachama wa hizb na mbinu ya kiholela inayotumiwa na mamlaka dhidi ya wale ambao hawakubaliani nao.
Kulikuwa na makubaliano wazi kuhusu haja ya kuzuia shambulizi hili la uhalalishaji mahusiano la Marekani na Wazayuni dhidi ya Lebanon na kanda hii, na kuhusu haja ya kuongeza uelewa wa watu kupitia semina, mihadhara, na shughuli za umma.
Ujumbe ulimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa mapokezi hayo, ukielezea matumaini kwamba njia za mawasiliano kati ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon na Mheshimiwa Mbunge huyo zitaendelea.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Lebanon |
Address & Website Tel: 009616629524 http://www.tahrir.info/ |
Fax: 009616424695 E-Mail: ht@tahrir.info |



