Kukamatwa kwa Ndugu yetu Al-Munawar Hakutabadili Uhalisia wa Vita vya Kipuuzi nchini Sudan
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Jana asubuhi, Jumanne, tarehe 19 Rabi` al-Akhir 1446 H sawia na 22/10/2024 M, chombo cha usalama kilimkamata Ndugu Al-Munawar Dafallah Mustafa, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, kutoka nyumbani kwake katika mtaa wa Al-Sharif Al-Aqab katika mji wa Al-Qadharif, kwa misingi ya majadiliano katika kundi la WhatsApp, ambapo Ndugu Munawar alieleza uhalisia wa vita vinavyoendelea nchini Sudan, kwamba ni mzozo kati ya nguzo mbili za ukoloni; Amerika na Uingereza.