Jumanne, 13 Muharram 1447 | 2025/07/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  9 Muharram 1447 Na: H 1447 / 02
M.  Ijumaa, 04 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh Iliandaa Maandamano na Matembezi ya kupinga Uhamishaji wa India wa Waislamu hadi Bangladesh kwa Mtutu wa Bunduki

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh, iliandaa maandamano na matembezi leo (Ijumaa, 4 Julai 2025) baada ya swala ya Ijumaa katika misikiti mbalimbali ya Dhaka na Chittagong kupinga uhamishaji unaoendelea wa India wa Waislamu hadi Bangladesh kwa mtutu wa bunduki. Wanachama mbalimbali wa Hizb ut Tahrir walitoa hotuba katika maandamano hayo ambayo yalimalizika sambamba na matembezi.

Hivi karibuni serikali ya Modi imekuwa ikiwachukulia Waislamu wa India kama wanyama, ikiwaita wahamiaji haramu, kubomoa nyumba zao na kuwafukuza kwa nguvu hadi Bangladesh. Wazungumzaji katika mikusanyiko ya maandamano walilinganisha tabia hii ya Hindutva India na umbile la Kiyahudi. Wazungumzaji hao walikosoa tabaka tawala za na wasomi wa sasa wa kisekula, wakisema kwamba wanajaribu kuficha ukweli halisi kwa kuita tabia hii ya uchokozi ya India kuwa ni matokeo ya mahusiano wa kiuadui ya India na Bangladesh baada ya kuanguka kwa dhalimu Hasina. Walakini, mauaji ya mpakani, unyanyasaji wa maji, mateso ya Waislamu ndani ya India, kuanzia kubomolewa kwa Msikiti wa Babri wa kihistoria ili kujenga hekalu ili kufuta mila ya utawala wa Kiislamu wa miaka elfu moja, ikionyesha kiburi kama kudai kufukuliwa kwa kaburi la Aurangzeb, uundaji wa Sheria mpya ya Uraia (CAA), na Sajili ya Raia nk, yamekuwa yakiendelea kwa muda mrefu. Kwa hakika, tabia hii ya Hindutva India ni sehemu ya mchakato unaoendelea wa hali ya kutokuwa na taifa na kufuta kitambulisho cha Waislamu nchini India, kama vile umbile la Kiyahudi linavyoendelea kufanya huko Palestina. Mwenyezi Mungu ﷻ asema,

[لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ ٱلنَّاسِ عَدَاوَةًۭ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱلْيَهُودَ وَٱلَّذِينَ أَشْرَكُواْ]

“Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina.” [Surah Al-Ma’idah: 82].

Wazungumzaji waliangazia sababu mbili za tabia hii ya kiburi dhidi ya Waislamu na Uislamu ya dola ya Hindutva ya India. Kwanza, ijapokuwa Waislamu wa eneo hili wamefungwa na Imani na damu moja, mkoloni wa kafiri Uingereza aliwagawanya Waislamu kwa msingi wa utaifa (Wahindi, Wabangladeshi, Wapakistani nk.) ili kuwadhoofisha, na kuwapandikiza watawala wa kisekula kuwa wakala wao kwa watu wa eneo hili. Wanasiasa na wasomi wa kisekula ni wanafiki sana hivi kwamba wananguruma kama simba marara dhidi ya ukandamizaji wa Mabaniani walio wachache nchini Bangladesh, na wanaonekana kama paka dhidi ya ukandamizaji wa Waislamu 'walio wachache' nchini India. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«لَيْسَ مِنَّا مَنْ دَعَا إِلَى عَصَبِيَّةٍ، وَلَيْسَ مِنَّا مَنْ قَاتَلَ عَلَى عَصَبِيَّةٍ، وَلَيْسَ مِنَّا مَنْ مَاتَ عَلَى عَصَبِيَّةٍ»

“Si katika sisi atakayelingania Asab Asabiyyah (utaifa); si katika sisi atakayepigana kwa ajili ya Asabiyyah; na si katika sisi atakaye kufa kwa ajili ya Asabiyyah” (Abu Dawud).

Pili, India ni wandani wa kikanda wa mkoloni kafiri Amerika, haswa mwanachama wa Quad, moja ya miungano ya kijeshi katika eneo la Indo-Pasifiki. Kama vile Amerika mkoloni Kafiri inavyolitumia umbile haramu la Kiyahudi katika Mashariki ya Kati kukandamiza Umma wa Kiislamu, wao vile vile wanatumia Dola ya Hindutva ya India Asia Kusini.

Wazungumzaji walitukumbusha jukumu letu sisi kama Waislamu: Ni faradhi kwa Waislamu wote kuwasaidia Waislamu katika sehemu yoyote ya dunia wanaposhambuliwa. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[وَإِنِ ٱسْتَنصَرُوكُمْ فِى ٱلدِّينِ فَعَلَيْكُمُ ٱلنَّصْرُ] “Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia [Surah Al-Anfal: 72]. Matabaka ya sasa tawala ya kisekula ya Waislamu sio walinzi wa Umma wa Kiislamu; hawapeleki vikosi vyetu vya kijeshi kuwasaidia Waislamu wa Palestina-Kashmir-Arkan, wakati kwa wito wa Amerika, wanatuma vikosi vya kijeshi chini ya uongozi wa Umoja wa Mataifa na kumwaga damu.

Hatimaye, wazungumzaji waliwataka Waislamu kusema: Waislamu wanateswa duniani kote kutokana na kukosekana mlinzi wa kweli wa Umma wa Kiislamu – Khilafah.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam (Khalifa) ni ngao Waislamu hupigana nyuma yake na hujihami kwaye” [Sahih Muslim].  Kwa hiyo, ni lazima tushikamane katika kusimamisha Khilafah bila ya kuwatazama watawala hawa vibaraka. Ni lazima tuwaite wana wanyoofu wa Umma wa Kiislamu wanaohudumu katika jeshi kutoa Nusrah (msaada wa kimada) kwa chama chenye ikhlasi cha Umma wa Kiislamu, Hizb ut Tahrir, katika kusimamisha Khilafah kwa njia ya utume.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu