Ni Lazima ikumbukwe kwamba Marekani ni Nchi ya Kikoloni; Kujisalimisha kwa Sera zake za Ushuru Kutahatarisha Ubwana wa Taifa!
- Imepeperushwa katika Bangladesh
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Marekani, mchuuzi wa kimataifa wa ubepari, imeibua 'dhoruba ya ushuru' duniani kote, ikipuuza kanuni za uchumi wa soko huria – moja ya falsafa kuu za ubepari – na sheria na kanuni za kile kinachojulikana kama Shirika la Biashara Duniani (WTO) ililounda. Hii, kwa mara nyingine, inathibitisha kwamba mfumo wa kibepari hauna utu na wa kinyonyaji. Serikali ya mpito ya Bangladesh imetabanni sera ya utiifu katika kukabiliana na hatua za ushuru za Marekani. Tayari wamefanya uamuzi wa kujitoa mhanga kununua ndege 25 za gharama kubwa aina ya Boeing, pamoja na kuagiza pamba na LNG kutoka Marekani, ingawa nchi nyingi zinaghairi oda zao kutokana na utendakazi duni wa Boeing. Na wanafanya mikutano ya moja kwa moja na Marekani, wakiweka umma katika giza kupitia 'makubaliano fiche ya kihistoria' (NDA).