Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 488
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Karibu Ramadhan, mwezi wa ushindi, mwezi wa bishara njema, mwezi wa kujadidishwa imani na kutakasa nyoyo, mwezi wa utiifu na kushindana katika mambo mema. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliyetufikisha Ramadhan, mwezi huu mtukufu ambao tunahisi ndani yake maana ya rehema na umoja baina ya Waislamu. Karibu, Ramadhan.
Kwa kuzingatia mauaji ya halaiki ya kikatili ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa miezi mitano iliyopita yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa kwa Waislamu zaidi ya 110,000.
Baada ya kuutafuta mwandamo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, mkesha huu wa Jumatatu, muandamo wa mwezi mpya kwa mujibu wa matakwa ya Shariah unathibitishwa, na kwa hiyo kesho, Jumatatu ni siku ya kwanza ya mwezi uliobarikiwa wa Ramadhan kwa mwaka huu wa 1445 H.
Hizb ut Tahrir / Wilayah Syria: Amali ya Kuutafuta Mwezi Muandamo wa Ramadhan Al-Mubarak 1445 H
Hizb ut Tahrir / Uholanzi iliandaa kisimamo kikubwa cha kuinusuru Gaza tukufu, wakati wa ziara ya mhalifu Herzog raisi wa umbile nyakuzi la Kiyahudi jijini Amsterdam kuhudhuria ufunguzi wa jumba jipya la makavazi la mauaji ya halaiki (Holocaust).
Kalima iliyotolewa na Ustadh Abdo Al-Dilli (Abu Al-Mundhir) wakati wa kisimamo kilichoandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Syria siku ya Ijumaa: “Magereza Yenu Hayakatishi Azma Yetu, bali Yanazidisha Uthabiti Wetu!
Mnamo tarehe 4 Machi 2024, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alisema, “Pakistan ya kidemokrasia ni muhimu kwa maslahi katika ya Marekani na Pakistan, na ushirikiano wetu na Waziri Mkuu mpya Shehbaz Sharif na serikali yake utaendelea kuzingatia kuendeleza maslahi haya ya pamoja.” Kwa hivyo, Marekani inasalia katika udhibiti kamili wa Pakistan kupitia vibaraka wake katika uongozi wa kijeshi.
Enyi Maafisa na Askari wa Jeshi la Pakistan! Kumekuwa na vilio vya kutosha vya kuomba kutoka Gaza hadi kwenu! Kumekuwa na vilio vya kutosha kwa wale ambao wana masikio yanayosikia na nyoyo zinayohisi. Katika miezi hii mirefu, yenye uchungu na isiyotulia, tumesikia visingizio vyenu vyote vya kutokuchukua hatua. Hakuna udhuru wenu hata mmoja unaokubalika, kwa mujibu wa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw).
Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 100 M (103 H) ya kuvunjwa Dola ya Kiislamu (Khilafah) na chini ya giza la uvamizi na mauaji ya halaiki yanayoendelea dhidi ya watu wetu katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina), Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon ilifanya kongamano lenye kichwa: “Khilafah ndio Mkombozi wa Nchi na Mtetezi wa Waja”