Alhamisi, 09 Jumada al-awwal 1447 | 2025/10/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uundaji na Uvunjaji wa Vyama vya Kisiasa katika Uislamu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Wizara ya mambo ya ndani mnamo Ijumaa iliarifu kuhusu marufuku ya Tehreek-i-Labbaik Pakistan (TLP), ikisema kwamba serikali ya kifederali ina “hoja msingi” za kuamini kwamba chama hicho cha siasa za kidini kinahusishwa na ugaidi. (Dawn)

Maoni:

Uasi wa 1857 ulifanywa kuwa mfano kwa watu wa Bara Ndogo ili kuwaonya dhidi ya kuinuka dhidi ya wale walio madarakani. Waingereza waliweka mfano huo, lakini hata leo, watawala wanaendelea kuufuata. Tangu hata kabla ya kuundwa kwake, Pakistan imekuwa ikikabiliwa na mapambano ya mara kwa mara kati ya fikra za kitaifa na kidini. Kabla ya kugawanyika kwa Bara Ndogo la India, Bunge la Kitaifa la Congress la India liliibuka kama upande unaoitwa “mwakilishi” kwa watu wote wa India. Hata hivyo, ikawa wazi hivi karibuni kwamba viongozi wa Bunge walikuwa wakifanya kazi hasa kuunda serikali inayotawaliwa na Mabaniani, huku wakiiwasilisha kama harakati ya kitaifa. Viongozi wa Kiislamu kama Muhammad Ali Jinnah, Muhammad Ali Johar, Maulana Abul Kalam Azad, na Hussain Shaheed Suhrawardy walifanya kazi na Bunge la Kitaifa la India kwa sababu wazo la kujitenga halikuonekana kama suluhisho na waliamini katika bara ndogo lililoungana kama walivyoliona kila wakati.

Lakini baada ya muda, waligundua kuwa Bunge lilikuwa linahudumia maslahi ya Mabaniani, likiwaacha Waislamu nyuma. Kwa kujibu, chama kipya kiliundwa ili kulinda haki za Waislamu, Ligi ya Waislamu Wote wa India. Chama hiki kilikuwa zao la akili ya mwanadamu, ambayo ilitoa ufafanuzi wake wa kuishi na kuamka kwa Waislamu. Uislamu unataka kwamba fikra zote lazima zijitokeze kutoka kwa mfumo wa Kiislamu. Kulegeza msimamo kisha kukasababisha suluhisho lililopikwa nusu ambalo halikuwa la Uislamu, wala la ulimwengu wa kisasa. Takriban miaka 40 baada ya kuanzishwa kwake, Ligi ilifikia lengo lake kuu, kuundwa kwa nchi tofauti kwa ajili ya Waislamu wa India. Mwishowe, fikra za kitaifa zilishinda, lakini zilikuwa zimefungwa katika hisia za kidini ili kupata uungwaji mkono wa Waislamu.

Sisi Waislamu wa Pakistan hadi leo tunapambana na utiifu kamili kwa fikra ya utaifa. Hisia ya Kiislamu ya kujisalimisha imejikita sana ndani yetu kutolaani kwa ajili ya Palestina na hivyo hii inatoa fursa kubwa zaidi kwa hisia hii kutumiwa vibaya. Kwa kuwa siasa ni kuchunga na kujali masuala ya umma, chama cha kisiasa katika Uislamu ni mkusanyiko wa kikundi chenye imani kwa msingi wa Uislamu, ambao ni kheri yote, na ulinganizi wake kama itikadi ya kisiasa na mfumo unaotawala maisha. Kuhusu vyama vya kisiasa, rasimu ya katiba iliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir inasema, “Waislamu wana haki ya kuanzisha vyama vya kisiasa ili kuwahisabu watawala, au kufikia madarakani kupitia Ummah, kwa sharti kwamba vinaegemea aqida ya Kiislamu, na kwamba maamuzi vinayopitisha ni maamuzi ya Kiislamu. Kuanzishwa kwa chama hakuhitaji leseni yoyote, na kambi yoyote inayoegemea kitu chengine chochote isipokuwa Uislamu ni marufuku.” Pia hairuhusiwi kwa kundi miongoni mwa Waislamu kuegemea kitu chengine chochote isipokuwa msingi wa Uislamu kama imani na mfumo. Ingawa, kulingana na Kifungu cha 17 cha katiba ya Pakistan, Kila raia atakuwa na haki ya kuunda vyama au vyama vya wafanyakazi, chini ya vikwazo vyovyote vinavyofaa vilivyowekwa na sheria kwa maslahi ya ubwana au uadilifu wa Pakistan, utulivu wa umma au maadili.

Ukandamizaji wa hivi karibuni dhidi ya Tehreek-e-Labbaik Pakistan chini ya Sheria ya Kupambana na Ugaidi, na marufuku dhidi ya chama cha kisiasa, inaonyesha kwamba Serikali ya Pakistan ina vipimo tofauti kwa chama cha kisiasa kuliko vipimo katika Uislamu. Tehreek-e-Labbaik Pakistan ni chama cha kisiasa ambacho, kama makundi mengine ya kisiasa ya kidini, kimeshiriki katika uchaguzi na kinashikilia kiti katika bunge, ambacho kinaonyesha utiifu wake kwa mfumo na mgongano wake na fikra ya chama cha kisiasa katika Uislamu.     

Kwa hivyo muamala uliyopewa Tehreek-e-Labbaik unatoka katika mfumo ambao walioutambua na kuukubali kwa mara ya kwanza na baadaye wakaukosowa na hivyo kwa kujibu kikao dhidi ya sera ya Serikali kuhusu Palestina, wafuasi walioingia barabarani waliamiliwa kama waandamanaji wa uasi wa 1857. Ambayo inaonyesha hisia ya kutawala ya Uingereza iliyobebwa na uongozi wa leo. Hii inaonyesha kwamba tatizo liko katika kipengee cha kidini. Mara tu kitakapokuwa kimefagiwa kabisa kwa sera ya maslahi ya kitaifa, itakubalika kwa Serikali. Ikiwa leo Tehreek-e-Labbaik Pakistan itaacha mtazamo wa kidini, ingawa itahifadhi jina lake kama lilivyo, haitakuwa na madhara kwa watawala wa Pakistan.

Hairuhusiwi kwa vyama vya kisiasa kushiriki katika utawala wa kisekula unaoutenga Uislamu madarakani, si kwa kuunda serikali wala kwa kushiriki ndani yake, Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wapotofu.” [Al-Ma’ida: 47].

Hali ya leo nchini Pakistan inahitaji suluhisho lililohitajika karne moja iliyopita, si kuzaliwa kwa chama cha ‘All India Muslim League’, wala kuangamia kwa Tehreek-e-Labbaik ya leo, bali kuungana tena kwenye mzizi wa Uislamu, kuikabidhi Serikali kwa khalifa wa Mwenyezi Mungu (swt), ambaye atahukumu tu kulingana na maagizo ya Mwenyezi Mungu (swt). Mtawala ambaye atavipa kazi vikosi vyake kuikomboa ardhi ya Al-Qudsi kutoka kwa makucha ya Wazayuni. Wakati huu unaweza kutumika kama nukta ya mabadiliko kwa Waislamu kuungana tena na kitambulisho chao cha pamoja kilichojikita katika Uislamu, kitambulisho kinachovuka mipaka, makabila, na lugha.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ]

“Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.” [Al-Anbiya: 92].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu