Jumamosi, 21 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Utegemezi wa Dola za Kikoloni za Kikafiri Humpora Mtu Utashi wa Kisiasa, Hupotosha Dira ya Mtu na Kupoteza Nguvu za Mtu

(Imetafsiriwa)

Gazeti la Al-Rayah – Toleo 564 - 10/09/2025 M

Na Ustadh Muhammad Saeed Al-Aboud

Kwa kuzingatia ukandamizaji unaoendelea Syria kwa matakwa ya Amerika na mfumo wa kimataifa, watu wanahisi wameporwa utashi wao, kukosa uwezo wa kufanya maamuzi yao wenyewe, na kuhofia mustakabali wao. Ili kuelewa ni nani anayeamua mambo nchini Syria na kwa nini tumepoteza uwezo wetu wa kufanya maamuzi, lazima tuhakiki mkondo wa mapinduzi ya Syria tangu mwanzo wake.

Serikali wa zamani ilipotumia jeshi na vikosi vya usalama dhidi ya wananchi, wanamapinduzi waliamua kuunda vikundi ili kuwalinda waandamanaji kwa silaha nyepesi. Hili liliimarika kuwa uundaji makundi ya kimapinduzi yaliyoteka silaha za utawala huo na kuweza kukomboa asilimia 70 ya nchi. Waliinua Rayah (bendera za jihad) na wakataka utawala wa Uislamu. Baadhi yao hata walitabanni rasimu ya katiba iliyopendekezwa na Hizb ut Tahrir, ambayo ilizitia hofu dola za kimataifa, zikiongozwa na Amerika. Waliingilia kati ili kuunga mkono serikali nyuma ya pazia, ambayo ilisababisha watu kuzindua maandamano ya Ijumaa yenye kichwa “Amerika, je, chuki yako haijashibishwa na damu yetu?” Hii inaashiria utambuzi wa watu juu ya utiifu wa serikali ya zamani kwa Amerika na uungaji mkono wake kwake. Hili liliilazimu Marekani kuzama zaidi katika ulaghai wake, hivyo ikaagiza vyombo vyake kutoka tawala jirani kama vile Uturuki, Saudi Arabia, Jordan, Qatar, na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuingilia kati kudhibiti mapinduzi hayo kwa kunyang'anya uamuzi wake kupitia usaidizi kwa pesa chafu za kisiasa. Kwa kusudi hili, ilianzisha vituo vya kijeshi vya MOC na MOM. Lengo la usaidizi huu lilikuwa ni kupenya safu za mapinduzi, kukamata uamuzi wake, kuudhibiti, na kuuelekeza kwenye vita vya pembeni ili kuumaliza, haswa kwa vile msaada huo ulikuwa wa silaha zisizofaa ambazo hazikuweza kuzima mashambulizi ya angani, makombora na mizinga. Mishahara ilikuwa midogo, hata ikawa ni njia ya ufisadi kwa viongozi walioiona kuwa chanzo cha utajiri kupitia aina mbalimbali za ufisadi. Hili liliyafunga pingu mapinduzi ya ash-Sham, ambayo yalikumbwa na ufisadi na kutegemea msaada baridi, badala ya ngawira za dhati za vita na utawala wa zamani, ambao ulikuwa ndio sababu ya masaibu yake, kuyadhoofisha, na kuyakomboa maeneo kutoka kwake.

Kwa njia hii, mapinduzi yalipoteza uhuru wake na uwezo wake wa kufanya maamuzi. Maandamano yalizuka, yakidai marekebisho ya mwelekeo na kuregeshwa kwa mamlaka sahihi ya ufanyaji maamuzi. Walakini, yalikabiliwa na uhalalishaji na walafi, kama ilivyo hali sasa, kwa kisingizio cha “Watu watakula wapi?!” Kana kwamba tuko kwenye mapinduzi ya watu wenye njaa! Makundi hayo yalijishughulisha na msaada, waungaji mkono, na uunganishwaji wa makundi kupitia ushirikiano, lakini bila mafanikio, kwani yalifungwa pingu kwa amri za waungaji mkono wao.

Uhalalishaji wa viongozi wa makundi daima umekuwa kwamba, “watachukua pesa, lakini hawatatekeleza maagizo ya waungaji mkono wao.” Hii ndiyo hoja inayotumiwa na wale wanaohalalisha sera ya utumwa na utiifu kwa maagizo ya Marekani na zana zake, ambayo serikali mpya ya Damascus inafuata. Walakini, hili liko mbali na uhalisia. Usaidizi huo umemomonyoa azma ya viongozi wa makundi, ambao wametekeleza maagizo, wamesalimisha maeneo, wametekeleza makubaliano ya Sochi na Astana, wamejitolea kupunguza kasi, na hata kupigana vita vya chuki dhidi ya mujahidina mukhlisina waliopinga kufungwa kwa mipaka.

Sawia na haya ndiyo yanayojiri mikononi mwa serikali mpya hivi leo, huku ikiingilia kati kuwazuia mujahidina kupata ushindi wa uhakika katika vita kadhaa, kama ilivyotokea katika vita vya pwani na Suwayda. Hii ni kwa kufuata tu amri za waungaji mkono wao, ambazo zimewaweka watu wa ash-Sham katika hatari kubwa ambazo zingeweza kushindwa kwa urahisi na kuondolewa lau uamuzi ungefanywa kwa njia huru.

Ndio, mkengeuko ulianza tangu mwanzo, kuweka rejani ufanyaji maamuzi kwa nchi zinazokula njama, zikiongozwa na Amerika, na kujisalimisha kwa maagizo ya Thomas Barrack, mjumbe wa Amerika nchini Syria, ambaye alijulikana kama “Kamishna Mkuu,” kutatupeleka tu shimoni. Mtu asiyekuwa na uwezo wa kufanya maamuzi katika mapinduzi hatakuwa mtu mwenye maamuzi madarakani. Hii ni kwa sababu wanaomuunga mkono watadhibiti maamuzi yake na anachopaswa kufanya ni kutekeleza uamuzi wao. Ameingia kwenye shimo la mjusi ambalo hataweza kutoka isipokuwa kwa kukata mikono ya wasaidizi wake.

Utawala wa sasa wa Syria umeshughulishwa na nyanja ya kiuchumi kwa gharama ya misingi ya mapinduzi, una furaha kushirikiana pamoja na mfumo wa kimataifa mfumo wake wa kiuchumi wa kibepari, ambao unawaahidi majumba marefu, vichuguu vya metro, na miradi ya utalii ambayo itawafunga pingu zaidi. Kisha wanadai watatoka humo hadi kwenye kivuli cha Uislamu! Kushikamana na madhalimu na makafiri ni hasara iliyo wazi katika dunia hii kabla ya akhera, na sio njia ya haki na ya kusimamisha Dini.

Kwa hivyo, ilikuwa ni lazima kutahadharisha dhidi ya kupuuza misingi ya mapinduzi na kujitolea mhanga kwa mujahidina, hasa kwa shinikizo la Marekani kwa utawala wa sasa kuuondoa Uislamu madarakani na kuleta mabaki ya utawala wa zamani karibu, na kuwarudisha wengi wao kwenye misimamo yao ya kazi licha ya hatari kubwa inayoletwa na jambo hili. Aidha, kuna majaribio ya kuwatenga watu wenye ikhlasi katika nafasi za ushawishi na kuwaoanisha na nguvu zisizoutaka Uislamu, na hivyo kuongeza vizuizi na vikwazo vya kurekebisha mkondo.

Leo ni lazima tujihadhari na maamuzi hatari zaidi yanayoukabili Umma wa Kiislamu, yaani uhalalishaji wa kuitupilia mbali Shariah na usimamishaji wa hukmu ya sheria kwa mujibu wa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt) kwa kisingizio cha kutokuwa na uwezo, maslahi ya kibinafsi, na fikra ya hatua kwa hatua (tadarruj). Hili limepelekea kupinduliwa kwa misingi na kauli mbiu zote zilizotolewa na watu wa ash-Sham katika mapinduzi yao. Tumeona kuachiliwa kwa kadhia ya Palestina na madai kwamba ash-Sham haitakuwa uwanja wa uzinduzi wa vita dhidi ya Mayahudi, na kuharakishwa kwa uhalalishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi, kupitia mikutano ya siri na ya dhahiri, ahadi za amani na Mayahudi, na kuingia katika Makubaliano ya Abraham “pindi dhurufu zitakaporuhusu.” Yote haya ni kuuzuia Ummah kutimiza yale ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameuwajibisha kuyafanya, ambayo ni kusimamisha Shariah yake na kukomboa ardhi za Waislamu, kwa kutekeleza amri za waungaji mkono na kuhadaiwa kupitia ustawi wa kiuchumi, ambao chini yake rasilimali za nchi zinauzwa kwa wawekezaji na makampuni ya kilafi ya kibepari.

Mwishowe, yeyote anayeshika uongozi lazima awe na maadili na mtetezi wa mradi wa Kiislamu kwa njia iliyo wazi na ya kina, kwa kuzingatia Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt), Sunnah ya Mtume Wake (saw), Makubaliano ya pamoja (Ijmaa’) ya Maswahaba (ra) na qiyas (mlingano wa Shari’) halali ya Kiislamu zinazowasilisha. Yeyote anayechukua uongozi lazima awe huru kutokana na ushawishi wa dola na maagizo yao. Maagizo yao husababisha Ghadhabu za Mwenyezi Mungu (swt) na yanagongana na amri Zake za Shariah. Huu ni mteremko hatari kuelekea kwenye shimo la utegemezi, utumwa, na udhalilifu. Asema Mwenyezi Mungu (swt): وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ“Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.” [Surah Hud:113].

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu