- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Baada ya Miezi Saba ya Hatua za Kimataifa, Syria Imenaswa baina ya Matarajio ya Nchi na Chaguo la Hatima
(Imetafsiriwa)
Gazeti la Al-Rayah – Toleo 557 - 23/07/2025 M
Na: Ustadh Abdo Al-Dali (Abu Al-Mundhir)*
Tangu Disemba 8, 2024, Syria imeshuhudia ziara mbalimbali za kidiplomasia katika ngazi mbalimbali. Ziara hizi haziwezi kuelezewa kuwa ziara za kawaida, haswa baada ya kuchunguza historia ya nchi zilizo zuru Damascus na kuelewa uhalisia wake.
Tunaweza kusema kwamba Syria kwa sasa inakabiliwa na mabadiliko makubwa katika uhusiano wake wa kimataifa tangu Bashar al-Assad kukimbia. Tukio hili la ghafla liliibua vuguvugu hili la kidiplomasia, haswa baada ya muda mrefu wa kudorora kisiasa na hatua zinazoyumba kuelekea uhalalishaji mahusiano. Tukio hili limelikanganya kanda hii; Matokeo yake yatakuwa ni kuunda upya ramani ya kidiplomasia ya kanda hii, au kufuata tu nyayo za wale waliotangulia.
Wajumbe wengi kutoka nchi za Kiarabu na Magharibi wamemiminika Damascus, katika hali ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu kuzuka kwa mapinduzi mwaka 2011. Je, wajumbe hawa ni kina nani? Kwa nini wamekuja? Malengo yao ni yapi?
Ziara ya Waingereza baada ya Miaka Kumi na Nne:
Mnamo tarehe 5 Julai 2025, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, David Lammy, alizuru mji mkuu wa Syria, ikiwa ni mara yake ya kwanza katika kipindi cha muongo mmoja. Katika ziara hiyo, alikutana na Rais wa mpito wa Syria Ahmad al-Sharaa na Waziri wa Mambo ya Nje Asaad al-Sheibani, na kutangaza kutenga takriban dolari milioni 129 za misaada ya kibinadamu na maendeleo, na kuthibitisha uungaji mkono wa nchi yake kwa utulivu na afueni ya Syria. Lammy alisisitiza kuwa Uingereza inafungua ukurasa mpya na Syria, akibainisha kuwa msaada huo utajumuisha uchimbaji wa madini, ukarabati wa miundombinu na uwezeshaji wa asasi za kiraia, huku akisisitiza haja ya kuwawajibisha wale wanaohusika na uhalifu wa kivita.
Marekani kulegeza vikwazo:
Mnamo Juni 30, 2025, Marekani ilitoa uamuzi wa kulegeza vikwazo vya kiuchumi vilivyowekewa Damascus. Hatua hii ilikuwa sehemu ya kifurushi cha mabadiliko katika sera ya kigeni ya Marekani kuelekea Mashariki ya Kati. Duru za Marekani zilisema kuwa uamuzi huo unalenga kuhimiza serikali ya Syria kusonga mbele na mabadiliko yake ya kidemokrasia na kuunga mkono utulivu wa kikanda.
Usaidizi wa Wazi wa Saudia:
Mnamo Februari 2025, Ahmed al-Sharaa alizuru Saudi Arabia, ambapo alipokelewa rasmi na Bin Salman. Mkutano huo ulishughulikia masuala ya ujenzi na ushirikiano katika sekta ya nishati, elimu na afya, pamoja na kujadili msaada wa uwekezaji wa Ghuba katika miundombinu ya Syria. Ziara hiyo ilibeba ishara maalum, kwani ilikuwa ni ziara ya kwanza ya kigeni ya rais mpya wa Syria, na ilionekana kama ishara ya kuongezeka kwa maelewano kati ya Damascus na miji mikuu ya Ghuba.
Jumuiya ya Kimataifa yachukua hatua:
Mnamo tarehe 12 Januari, Riyadh iliandaa kongamano la kimataifa liliohudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi kumi na saba, zikiwemo Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, pamoja na nchi kadhaa za Kiarabu. Kongamano hilo lilijadili kuondolewa hatua kwa hatua kwa vikwazo, kuunga mkono juhudi za ujenzi wa taasisi nchini Syria, na uwezeshaji wa serikali ya mpito.
Ziara za Ulaya: usaidizi wa masharti na ufuatiliaji wa makini:
Mnamo Januari 3, 2025, mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa na Ujerumani waliwasili jijini Damascus kwa ziara yenye mwelekeo wa kisiasa na kibinadamu. Walizuru Gereza la Sednaya na kukutana na viongozi wa upinzani na watu rasmi, kama sehemu ya juhudi za kuunga mkono haki ya mpito, na kujenga imani na jumuiya ya kimataifa.
Mnamo Machi, Ujerumani ilifungua tena ubalozi wake jijini Damascus, baada ya miaka kumi na tatu ya kufungwa, na kutangaza kifurushi cha msaada cha Euro milioni 300, kilichotolewa kusaidia miundombinu, huduma za afya, na programu za elimu kwa wakimbizi wanaoregea.
Kurudi kwa balozi za Kiarabu:
Nchi za Kiarabu hazikuwa mbali na harakati hii. Mnamo Mei 2025, Morocco ilituma mjumbe wa kiufundi kupanga kufunguliwa tena kwa ubalozi wake jijini Damascus, katika utekelezaji wa maagizo ya kifalme. Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria pia alizuru Damascus mnamo Februari 2025, na kutangaza uungaji mkono kamili wa nchi yake kwa awamu ya mpito. Kuhusu Iraq, ilituma ujumbe wa ngazi ya juu wa usalama mnamo Disemba 2024 ili kuratibu ushirikiano wa mpaka na kuzuia kupenya kwa makundi yenye itikadi kali.
Hayo hapo juu yanaonyesha kuwa matokeo yaliyopatikana, pamoja na juhudi kubwa za jukwaa maarufu na mujahidina, hayakuwa ya kuridhisha wala ya kutia moyo kwa nchi. Je, wangehakikishiwa vipi, ikizingatiwa kwamba walifanya kazi usiku na mchana kuzima na kukomesha mapinduzi?
Walikuwa wakiendelea kwa hatua wazi, zisizo na utata: kuhalalisha mahusiano na kuizalisha upya serikali. Shinikizo lililotolewa kwenye jukwaa maarufu ni msukumo wa ziada kwa kile kilichopangwa.
Kauli za Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki hazikuwa za bure, wala mikutano ya Saraqib na Abu al-Zandin haikosa maana, wala mazungumzo ya kufungua vivuko kutoka Maarat al-Nasan na Abu al-Zandin hayakuwa ni maneno ya kupitisha tu. Badala yake, zote zilikuwa hatua za halisi ndani ya mpango wazi.
Ikiwa kile kilichotarajiwa hakikufikiwa, basi kwa nini wajumbe hawa? Na kwa nini ziara hizi? Je, haingekuwa sahihi zaidi kususia na kuitenga Syria kabisa?
Jibu linaweza kupatikana katika taarifa zilizoambatana na vita, ambazo zilizungumza waziwazi juu ya haja ya kudhibiti harakati, na kuizuia kwenda kwenye njia zisizokubalika kwa nchi hizi.
Taarifa za Iraq, Jordan, na umbile la Kiyahudi, ambazo zilionyesha "uzito wa hali" na "umuhimu wa kuingilia kati ili kuidhibiti," zinafichua sababu ya kasi hii ya kidiplomasia, kutoka kwa ziara hadi kulegeza vikwazo, na zaidi.
Ikiwa tutachunguza misimamo ya nchi zilizotajwa katika makala ya mapinduzi, tunapata rekodi mbaya na nia mbaya, bila kusaza hata moja. Wote walishiriki katika majaribio ya kukomesha mapinduzi, kupanga, kula njama, na kujitahidi, kwa kila njia, kuyazuia yasifikie mwisho ulio salama.
Baada ya rekodi hii ya misimamo na sera, inadhihirika wazi kwamba wajumbe hao leo hawakuja kwa sababu ya hamu ya kheri. Badala yake, walipaswa kuzuia njia ambayo hawaitaki. Wanatafuta kuibakisha Syria kuwa dola ya kisekula, tiifu, isiyo na uwezo wake wa kufanya maamuzi yenyewe, iliyo mateka kwa sheria zao, fikra na masuluhisho hayo. Wanataka kutuzuia kutokana na ukombozi (tahrir), tusiwe na uwezo wa kuamua, na tusiwe na hadhi.
Ni wokovu gani unaoweza kutoka kwa wale waliotukoloni na kutukandamiza? Je, ni kutoroka kupi kunaweza kuwepo mikononi mwa wale waliotunyang'anya uhuru wetu na kuhujumu jukwaa letu maarufu na mapinduzi yetu?!
Leo, miezi saba baada ya harakati hii, bado hatuwezi kusema kwamba Syria imefanya chaguo lake. Fursa ingalipo, na kugeuza kosa bado kunawezekana. Ima tunachagua kuwa watoa maamuzi na kuwa na sauti katika ulimwengu huu, au tunabaki kwenye njia ya utegemezi, tuporwe maamuzi yetu na tufujwe!
Fursa haitarudiwa... Jitahidini kwa kile kilicho haki, kimbilieni hadhi, na jihadharini na kuchelewesha au kusitasita, asije Yule Aliyekupeni ukombozi (tahrir) kutoka kwa Bashar akakutelekezeni na kukuacheni kwa hila zenu wenyewe, akikuongozeni kwenye shimo huku mkiona!
Nchi hizi si taasisi za kutoa misaada, na misimamo yao kwetu haileti matunda mazuri. Kinachotokea leo si kwa manufaa yetu, isipokuwa ikiwa sisi ndio watoaji maamuzi. Chaguo liko mikononi mwetu, na mzunguko bado uko chini ya udhibiti wetu. Kwa hiyo kuweni makini, kuweni makini sana! Hebu na tugeuze kile kinachotokea leo kuwa lango ambalo kwalo tunaingia ulimwenguni kama mabwana, waheshimiwa, na wenye nguvu.
* Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria