Alhamisi, 20 Safar 1447 | 2025/08/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Musiiangushe Gaza, Enyi Waislamu
(Imetafsiriwa)

Gazeti la Al-Rayah – Toleo 560 - 13/08/2025 M

Na Ustadh Abdullah Zaid

Ni masikitiko kwa usaliti! Maumivu yake yanaumiza moyo. Hakika, usaliti ni mchungu zaidi kwa nafsi kuliko maumivu ya njaa, kifungo, na mateso. Wananchi wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina wakiwemo watu wa Gaza wanautaka Umma wa Kiislamu kuwanusuru na kuwakomboa, kwa sababu udugu wa Kiislamu unawataka Waislamu kuwanusuru wanaodhulumiwa miongoni mwao. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ لَا يَظْلِمُهُ، وَلَا يَخْذُلُهُ، وَلَا يَحْقِرُهُ، التَّقْوَى هَا هُنَا وَيُشِيرُ إِلَى صَدْرِهِ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ»

“Muislamu ni ndugu ya Muislamu, hamdhulumu, wala hamtupi, wala hamdharau. Uchamungu uko hapa. Akaashiria kifuani mwake mara tatu.” (Imepokewa na Muslim). Hivyo, hofu ya Mwenyezi Mungu (swt) iliyo ndani ya nyoyo za waumini inawahitaji wafanye kila wawezalo kunusuru ndugu zao na dada zao, kukomboa Al-Masjid Al-Aqsa, mahali pa Safari ya Usiku ya Mtume, na kuondoa vikwazo vyote vinavyowazuia ndugu zao na dada zao.

Hata hivyo, Waislamu wanawezaje kuwanusuru ndugu na dada zao, wakati mipaka ya kitaifa ya Sykes-Picot inawagawanya?

Je, Waislamu wanawezaje kuwasaidia watu wa Gaza, wakati watawala wao wanakula njama na adui yao ili wafe njaa, waue na kuwalazimisha kusalimu amri?

Vipi Waislamu wanaweza kuwanusuru ndugu zao, wakati mashirika ya kijasusi yanahesabu pumzi zao, na kuwatesa kwa maneno wanayotumia kudhihirisha hasira zao? Na wanafuatilia mitandao ya kijamii na misikiti ili kulinda viti vya utawala vya wasaliti, vibaraka?!

Vipi Waislamu wanaweza kuinusuru Dini yao ilhali Maulamaa wa serikali wanazunguka kwenye mzunguko wa watawala vibaraka, wakiipamba batili yao kwao?!

Enyi Waislamu:

Hali yetu ya Gaza haiko mbali sana na ile ya ndugu na dada zetu wa Sudan, wala haitofautiani na yale yaliyowapata watu wetu huko ash-Sham, au ndugu na dada zetu wa Turkestan Mashariki, Burma, Somalia, Bosnia, na kadhalika. Maumivu ya usaliti yanasikika kote katika ardhi za Waislamu, nchi baada ya nchi, na maadui wa Uislamu wanavuruga umma wetu kila mahali. Uhalifu mkubwa zaidi uko kwa watawala vibaraka ambao wanashirikiana na maadui zao.

Leo Umma umefikia hali ya kufahamu kuwa ni Ummah mmoja, pamoja na Dini, fikra na hisia zake, na kwamba ni mwili mmoja unaovuja damu jeraha la Gaza, kwa sababu watu wa Hijaz, na watu wa Yemen wanaumia kwa mateso yake, na watu wa Misri wanaugua kwa maumivu kwa kuugua kwake. Hata hivyo, watu wa Hijaz, Misri, Sudan, Pakistan, Uturuki na nchi zote za Kiislamu wamefungwa kwa mipaka ya kitaifa, kuta na nchi za kitaifa kama maumbo tofauti na watu wa Gaza. Ukweli ni kwamba moyo, akili na nafsi hutamani na kuwaka kuwanusuru kaka na dada zao, hata hivyo, mkono unaoshambulia na mguu unaotembea umefungwa kwa kifungo cha watawala vibaraka na mipaka ya kitaifa.

Waislamu wanazidi kuamini kwamba watawala hao si chochote ila ni zana mikononi mwa Mayahudi na Wamarekani ili kuwakatisha tamaa Waislamu wasiwanusuru ndugu zao. Lau isingekuwa kwa vibaraka hawa, mamilioni ya watu wangeelekea Al-Quds, wakipaza Takbira, Allahu Akbar, ili waswali swala ya ushindi kwenye Al-Masjid Al-Aqsa.

Umma wa Kiislamu sio dhaifu wala haukukosa uwezo wa kuinusuru Gaza, au kuwanusuru wanaodhulumiwa miongoni mwa Waislamu. Wale wanaouonyesha Ummah hivyo ni wanafiki, watawala dhalimu wanaowafanya Waislamu wajisikie wanyonge na madhaifu, na ambao wanapigania damu, matukufu na heshima zao kwa Marekani na taasisi za kimataifa za kikoloni.

Wananchi wa Gaza wanautaka Umma wa Kiislamu na majeshi yake kuwaokoa na kuwakomboa kutoka kwa Mayahudi, huku watawala vibaraka wakiiomba Marekani na taasisi za kikoloni za kimataifa kuondoa mzingiro huo na kuruhusu misaada kuingia nchini humo! Hili linadhihirisha na kuthibitisha kwamba hawaichukulii kadhia ya watu wa Gaza kuwa yao wenyewe. Wanaoamua hatima ya Gaza ni Amerika na Mayahudi, huku dori yao waliyopewa ni kuwaweka Waislamu chini ya shinikizo la mashirika ya kijasusi na ukandamizaji, ili Amerika na Mayahudi waweze kutekeleza njama zao katika ardhi za Kiislamu.

Enyi Waislamu!

Kuingia mabarabarani na viwanjani kuunga mkono watu wa Gaza ni wajibu wa Sharia, lakini sio tu kuonyesha mshikamano au kutoa hasira na kisha kurudi nyumbani. Badala yake, kinachotakiwa kwenu ni kuyahamasisha majeshi ya Waislamu, na kuwalingania ili kupindua tawala zinazosimama baina yenu na nusra ya ndugu na dada zenu.

Jitokezeni kwenye viwanja vya umma ili kuyachochea majeshi kupigana Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt), na kuondoa mipaka ya kitaifa iliyochorwa na wakoloni.

Tunataka kwenda kwenye viwanja vya umma, na tusirudi, hadi viti vya utawala vitakapovunjwa na majeshi yajibu. Hatutakula mpaka watu wa Gaza wale, na hatutalala mpaka watu wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina wakombolewe. Tunataka kimbunga ambacho kitang'oa makundi ya uhaini, na kuondoa vikwazo na vizuizi vyote vilivyosimama baina ya Umma wa Kiislamu na kuungana kwake, kusimamisha Dini yake, na Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt) ili kulifanya Neno Lake kuwa Tukufu, na kulifanya neno la makafiri kuwa chini kabisa, na Neno la Mwenyezi Mungu kuwa juu kabisa.

Enyi Waislamu!

Muna uwezo wa kheri hii na munastahiki wema huu. Hakika nyinyi mumeipata kheri hii, basi mnusuruni Mwenyezi Mungu (swt) naye atakunusuruni na ataifanya imara miguu yenu. Ondoeni hofu ya watawala vibaraka katika nyoyo zenu, wala msitishwe na uwezo na kiburi cha Marekani, kwani uwezo wa Mwenyezi Mungu (swt) ni mkubwa zaidi, na Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu zaidi na mkali zaidi wa kuadhibu. Muumini anamtegemea Mwenyezi Mungu (swt) kwa tawwakul ya kweli, na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mlinzi wa mambo. Watu wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, kwa Usaidizi na Mwongozo wa Mwenyezi Mungu, watabakia kuwa washindi juu ya haki, na wale wanaowaangusha hawatawadhuru. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amesema,

«لَا تَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي ‌ظَاهِرِينَ ‌عَلَى ‌الْحَقِّ لَا يَضُرُّهُمْ مَنْ خَذَلَهُمْ، حَتَّى يَأْتِيَ أَمْرُ اللهِ وَهُمْ كَذَلِكَ»

“Kundi katika Ummah wangu litaendelea kushinda juu ya Haki, na wale wanaowaangusha hawatawadhuru mpaka ifike hukumu ya Mwenyezi Mungu, nao wangali hivyo.” (Imepokewa na Muslim). Tuna hakika na ushindi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na tunakulinganieni kuwa na ikhlasi mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) katika kuinusuru Dini yenu na ndugu na dada zenu, ili mupate utukufu wa kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Neema hii kubwa na heshima hii hupatikana tu kwa watu walio waaminifu kwa yale waliyo muahidi Mwenyezi Mungu (swt). Basi kuweni wakweli kwa Mwenyezi Mungu (swt), naye atakuwa mkweli kwenu. Inatosha kwenu katika jambo hili kwamba Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

[إِنَّ اللهَ اشْتَرَى مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنْفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ وَعْداً عَلَيْهِ حَقّاً فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنْجِيلِ وَالْقُرْآنِ وَمَنْ أَوْفَى بِعَهْدِهِ مِنَ اللهِ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُمْ بِهِ وَذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ]

“Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.” [Surah At-Tawbah 111]. Kwa ahadi hii huko ndiko kufuzu kukubwa.

Ewe Mwenyezi Mungu, zifungue nyoyo za Waislamu kwenye utiifu wako na nusra kwa ajili ya Dini Yako, na utujaalie kutoka Kwako mamlaka yenye kunusuru.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu