Afisi ya Habari
Uzbekistan
| H. 3 Jumada II 1447 | Na: 1447 / 05 |
| M. Jumatatu, 24 Novemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi kutoka Uzbekistan
Abdul-Majeed Butirov
[مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا]
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Surah Al-Ahzab: 23]
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir Uzbekistan yaomboleza kwa Umma wa Kiislamu mwanachama wa Hizb ut Tahrir:
Abdul-Majeed Butirov
Alitoka Andijan, na aliondoka kwenye makaazi ya mitihani akiwa na umri wa miaka 75 na kwenda mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Alikuwa mtu aliyesema neno la haki kwa mtawala dhalimu, akavunja kiburi cha ukafiri, na alikuwa mfano na kiigizo cha kuigwa kwa wengi kwa sababu ya ujasiri na uthabiti wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, licha ya uzee wake, na alikuwa mmoja wa wanaume na wana shujaa wa Ummah wa Kiislamu. Abdul-Majeed alikuwa mwandani mzuri, rafiki mkarimu, mnyenyekevu kwa waumini na mkali dhidi ya makafiri.
Ndugu yetu Abdul-Majeed alitumia karibu miaka 20 ya maisha yake katika magereza ya dhalimu Karimov, kama vile Jaslik na Zarafshan ambazo zina sifa mbaya kimataifa kwa mauaji, kwa ajili ya kuuokoa Ummah kutoka katika maisha duni unaoishi chini ya uzito wa utawala wa ukafiri na kwa ajili ya kusimamisha Dola ya Kiislamu ambayo Ummah unaishi kwa heshima na utu na ambayo kwayo ustawi na utulivu wa wote unadhaminiwa.
Chini ya mateso na ukandamizaji unaofanywa na vyombo vya mamlaka ya ukandamizaji vya utawala wa Uzbekistan, na mbwa wao wenye kichaa cha mbwa wanaoitwa Lokhmatch (yeye ni mfungwa ambaye, kwa badali ya kitu kidogo, hufichua hali za wafungwa kwa utawala kupitia matumizi ya nguvu, mateso na shinikizo [uchokozi]) hata magerezani sasa, ndugu yetu aliendelea kutangaza haki kwa uvumilivu na ukuu, licha ya udogo wa mwili wake, lakini hakurudi nyuma kamwe. Vile vile, Abdul-Majeed akawa uthibitisho kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya wanazuoni wa masultani wanaotumikia utawala dhalimu na kuzikamata mimbari za misikiti, ambazo ni sehemu za kulingania haki na wakatumikia utawala kwa vazi la Dini!
Alipata heshima hii kwa uimara wa imani yake kwa Mwenyezi Mungu pekee, utashi wake makubwa, na imani yake kamili katika ahadi ya Mola wa Walimwengu ya kuregesha Khilafah Rashida. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amkusanye ndugu huyu mpendwa mtukufu pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika Hawd Al-Kawthar, na tunamuomba yeye, Aliyetukuka, awape subira na faraja familia yake. Na kwa kumalizia, tunasema tu yale yanayomridhisha Mola wetu Mtukufu pekee: [إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ] “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Surah Al-Baqarah: 156].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uzbekistan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uzbekistan |
Address & Website Tel: |



