Ijumaa, 03 Dhu al-Hijjah 1446 | 2025/05/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  23 Dhu al-Qi'dah 1446 Na: 1446 / 13
M.  Jumatano, 21 Mei 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Nia na Malengo ya Ziara ya Afisa wa Uingereza nchini Uzbekistan
(Imetafsiriwa)

Mnamo Mei 13, 2025, Lord Cocker, Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, alifanya ziara rasmi nchini Uzbekistan. Ziara hii ni muhimu kwani ni ziara ya kwanza rasmi nchini Uzbekistan kwa mwakilishi wa serikali mpya ya Uingereza. Wakati wa ziara yake, alikutana na uongozi wa jeshi la Uzbekistan, akiwemo Naibu Waziri wa Ulinzi Kanali Jenerali Hamdam Qarshiyev na Kamanda wa Walinzi wa Kitaifa Luteni Jenerali Rustam Juraev. Mikutano hii ilithibitisha kujitolea kwa Uingereza katika kuimarisha ushirikiano wa ulinzi wa nchi mbili na Uzbekistan. Lord Cocker pia alitoa hotuba katika Chuo cha Jeshi la Uzbekistan, mara ya kwanza kwa Waziri wa Ulinzi wa Uingereza kuzungumza katika chuo hicho.

Ingawa ziara hii inaelezewa kama "ushirikiano," ni wazi kwa mtu yeyote mwenye ufahamu wa kisiasa kwamba inaendeshwa na maslahi na malengo ya kikoloni. Inajulikana vyema kuwa mojawapo ya mbinu kuu za sera ya ukoloni wa Uingereza ilikuwa mafunzo ya wafanyikazi waaminifu wa kudumu.

Ziara ya Waziri wa Ulinzi wa Uingereza katika Chuo cha Kijeshi cha Uzbekistan ni zaidi ya ziara tu. Kun.uz iliripoti mnamo Machi 17, 2018, kwamba "ilisisitizwa kwamba utekelezaji wa hatua zilizojumuishwa katika mpango wa ushirikiano wa kijeshi wa nchi mbili kati ya wizara za ulinzi za nchi hizo mbili, uliotiwa saini na wawakilishi wa Uingereza mnamo Januari 2018, utakuwa msingi wa ushirikiano wa kimataifa kati ya nchi hizo mbili. Mpango huo unajumuisha ushiriki wa wataalamu wa kijeshi wa Kiingereza katika operesheni za mafunzo katika taasisi za elimu ya kijeshi nchini Uzbekistan, ubadilishanaji utaalamu katika sekta mbalimbali za matibabu ya kijeshi, na mafunzo ya pamoja na mipango ya mafunzo.”

Kulingana na ripoti hizo, si vigumu kuelewa lengo halisi la ziara ya Waziri wa Ulinzi wa Uingereza. Uzbekistan sasa imekuwa shabaha kuu kwa mamlaka za kikoloni na uwanja wa siasa za kieneo ambapo mapambano yasiyoweza kusuluhishwa ya ushawishi na madaraka yanafanyika kati yao. Chini ya dhurufu kama hizi, Uingereza kimaumbile itatafuta mgao wake kwa mujibu wa sera yake ya jadi.

Kwa hiyo, ziara ya Lord Cocker inaweza kueleweka kama inayomaanisha: "Sisi pia tumo ndani ya mchezo mkubwa."

Uingereza ni mojawapo ya dola kubwa za kikoloni zinazojaribu kueneza ushawishi wake duniani kote. Ni miongoni mwa maadui wakubwa wa Uislamu na Waislamu. Ndiyo iliyoipindua Khilafah ya Uthmaniyyah, ikaugawanya Ummah wa Kiislamu, ikadunga kisu moyoni mwake, na ikaasisi umbile nyakuzi la Kiyahudi huko Palestina. Kati ya mwaka 1917 na 1924, ndiyo iliyochochea mzozo kati ya Waarabu na Waturuki katika nchi za Kiislamu na ikaongoza juhudi za kuiondoa Khilafah Uthmani. Uingereza haikuridhika na kuzigawanya ardhi za Waislamu; ilianzisha tawala vibaraka na mipaka ya bandia, ikiugawanya Ummah. Sera hii inaendelea kuitumikia, huku Ummah ukisalia bila dola wala mlinzi!

Uingereza haikutoa tu ardhi iliyobarikiwa ya Palestina kwa Mayahudi wanyakuzi, lakini pia inaunga mkono mauaji yao ya kikatili ambayo wamekuwa wakiyafanya huko Gaza na Palestina kwa miezi 19.

Watawala wanaokaa juu ya vifua vyetu wanajali tu kuhifadhi viti vyao vya utawala kwa kutumikia maslahi ya wakoloni makafiri. Chochote watakachokifanya, kamwe hawatawachukulia kuwa wao wenyewe. Mwenyezi Mungu Mtukufu anawakumbusha Waislamu juu ya hili katika Quran Tukufu, akisema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَتَّخِذُواْ بِطَانَةً مِّن دُونِكُمْ لاَ يَأْلُونَكُمْ خَبَالاً وَدُّواْ مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاء مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الآيَاتِ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini.” [Ali 'Imran 3:118], na Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[وَلَنْ تَرْضَى عَنْكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ]

“Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao.” [Al-Baqarah 2:120]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Enyi Madhalimu! Fungueni Macho yenu!

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu