Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 10 Rabi' I 1447 | Na: HTS 1447 / 22 |
M. Jumanne, 02 Septemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Watu wa Sudan, Mnaweza Kutibua Mpango wa Kuitenga Darfur, Basi Inukeni Kumtii Mwenyezi Mungu!
(Imetafsiriwa)
Katika hatua inayotarajiwa, kamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraka, Mohamed Hamdan Dagalo, alikula kiapo cha kikatiba kama mkuu wa Baraza la Rais la kile kinachoitwa serikali sambamba huko Nyala, mji mkuu wa Darfur Kusini, mnamo Jumamosi, 30/8/2025. Makamu wa Rais, wajumbe wa Baraza la Rais, na Waziri Mkuu pia walikula kiapo.
Hatua hii ilitarajiwa kama sehemu ya mpango wa uhalifu wa Marekani kutenganisha Darfur kupitia vibaraka wake, wakiwemo viongozi wa kijeshi, makamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na mamluki wa kisiasa.
Hatua hii ilikuja haraka baada ya Al-Burhan kukutana na Mshauri wa Rais wa Marekani Massad Boulos jijini Zurich, Uswizi, ambapo iliharakisha hatua hiyo kabla ya kuanguka kwa El Fasher.
Mbele ya uhalifu huu mkubwa, miitikio ya watu wa Sudan, katika sekta zao zote, ilitofautiana, kama ifuatavyo:
- Walioharakisha kutekeleza mpango huo na kuutekeleza kwa ulafi wa kuipendelea Marekani. Watu hawa lazima wakomeshwe na kuzuiwa kutekeleza uhalifu huu mkubwa.
- Watu waliofadhaishwa wanaoomba watu wakubali hali halisi ilivyo, kana kwamba kujitenga kwa Darfur ni hatima isiyoepukika ambayo lazima ukubaliwe! Hawa ni pamoja na wanasiasa, wanahabari na wengineo. Hatari yao inafichuliwa wanapoeneza mfadhaiko kwa bidii miongoni mwa wengine. Lazima wakomeshwe na kufahamishwa vipengee vya utawala vinavyowawezesha kukwamisha mpango huo.
- Kundi ambalo halijali kinachotokea, kana kwamba kinatokea kwenye sayari nyengine! Kwa sababu hawajui kinachoendelea karibu nao, lazima waelimishwe na nishati zao zihamasishwe ili kukwamisha mpango huo.
- Kundi lililotambua njama hiyo, linatarajia matukio na kuona nje ya ukuta. Kundi hili lazima lifanye kazi usiku na mchana, likikusanya nguvu za makundi yote, sio tu kukwamisha njama ya kuigawa Sudan na kutenganisha Darfur, lakini pia kurekebisha maisha, kubadilisha meza, na kuhamisha Ummah wetu kutoka kuwa shabaha ya njama na miradi ya uhalifu ya Kafiri Magharibi hadi kuwa kinara wa mwongozo na mwanga kwa kafiri huu wa Magharibi, kote ulimwenguni.
Sisi, katika Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan, tumekuwa, na tunaendelea kuwa waonyaji, tukifichua njama na kuhamasisha nia ya kuzuia njama za uhalifu.
Enyi Watu wa Sudan: mna uwezo wa kuzuia njama hii ya toleo la pili la kuichana nchi yenu, ambayo inalenga kutenganisha Darfur. Endapo Mtamtegemea Mwenyezi Mungu, kuomba msaada wake, na kufanya yafuatayo:
* Achaneni na kila kibaraka msaliti ambaye amejitwika jukumu la kutekeleza mpango huu, ima kwa kuunda serikali sambamba au kwa uzembe kuisalimisha El Fasher ili Vikosi vya Msaada wa Haraka viweze kukamilisha udhibiti wao katika eneo lote la Darfur.
* Kukusanya nguvu za watu wanyoofu katika watu wenye mamlaka na ulinzi, ili kutibua mpango na kuwakamata vibaraka na wasaliti.
* Kuhamasisha nguvu zote za vyombo vya habari, mimbari za misikiti, na nyinginezo ili kufichua njama na zana zake za utekelezaji ndani ya nchi, na kuwahamasisha watu kusimama dhidi yake.
* Kuhamasisha nguvu za watu wanyoofu, wasio na hatia ya uhusiano wowote na wasaliti, ikiwa ni pamoja na viongozi wa makabila, viongozi wa koo, wanafikra, wanamaoni, viongozi, wanasiasa, wanasheria, na watu wote mashuhuri, ili kuunda kizuizi kisichoweza kuvunjwa kulinda umoja wa mabaki ya nchi yetu.
Je, haya, yakichukuliwa pamoja, hayaundi nguvu ya kutisha inayoweza kutibua njama ya Amerika? Ambayo ni njama ya shetani scheme [إِنَّ كَيْدَ الشَّيْطَانِ كَانَ ضَعِيفاً] “Hakika hila za Shet'ani ni dhaifu” [An-Nisa: 76] [وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللّهُ وَاللّهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ] “Wakapanga mipango yao, na Mwenyezi Mungu akapanga yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa mipango.” [Al-Anfal: 30]. Mtume (saw) amesema:
«فَإِنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ بَعْدِي فَسَيَرَى اخْتِلَافاً كَثِيراً، فَعَلَيْكُمْ بِسُنَّتِي وَسُنَّةِ الْخُلَفَاءِ الْمَهْدِيِّينَ الرَّاشِدِينَ، تَمَسَّكُوا بِهَا وَعَضُّوا عَلَيْهَا بِالنَّوَاجِذِ»
“Hakika mwenye kuishi muda mrefu ataona fitna kubwa miongoni mwenu, basi shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Khulafa ar-Rashidyn (makhalifa walioongoka) wale wanaoongoa kwenye njia iliyo sawa. Shikamaneni nayo kwa ukaidi (ikamateni kwa majego).” Imesimuliwa na Al-Arbadh bin Sariyah, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, na imepokewa na Abu Dawud, Al-Tirmidhi, Ahmad na Ibn Hibban.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb Ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |