Heshima ya Wanawake wa Kiislamu ni ya Khiyari katika Demokrasia za Kiliberali
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 3 Oktoba, CBS News iliripoti kwamba mwanamke mmoja Muislamu alizuiliwa na polisi wa Philadelphia ambao walimvua hijabu yake. Wakati wa saa 20 ya kukamatwa kwake, aliachwa wazi na hakupewa njia ya kubadilisha nguo zake. Kwa sasa ameajiri mshauri wa kisheria kutoka Baraza la Mahusiano ya Kiislamu la Marekani (CAIR) na anataka haki kwa unyanyasaji wake.