Wasifu wa Amiri
- Imepeperushwa katika Wasifu wa Amiri
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Ni kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu (swt) ndio twaishi katika zama za mwisho. Hii ni zama ambayo imezungukwa na usiku ulio na kiza cha Ukafiri ambacho kila mwenye akili timamu atashtushwa kukishuhudia.
Jarida la Al-Waie lilipokea baadhi ya kumbukumbu za ndugu muheshimiwa, Salim al-Amr. Tunapeperusha baadhi yake kwa kuwa ndani yake muna mafunzo na manufaa, insha'Allah kwa wale ambao watazingatia.
Fikra ambayo juu yake imebuniwa Hizb ut Tahrir, inayo wasilishwa katika wanachama wake na ambayo inafanya kazi kuuyeyusha Umma kwayo, ili uichukue kama kadhia yake, ni fikra ya Kiislamu, yaani, ‘Aqeedah ya Kiislamu pamoja na sheria zinazotokamana nayo na fikra zilizo jengwa juu yake.
jia iliyo tabanniwa na Hizb ut Tahrir kulingania da’wah ni njia ya kisheria iliyovuliwa kutoka katika seerah ya Mtume (saw) katika utendakazi wake katika ulinganizi wa da’wah.
Baada ya kusoma, kutafakari na kuchunguza kuhusu hali ya sasa ya Umma huu na kiwango ulichofikia, na hali katika zama za Mtume (saw), na katika zama za Makhalifah wanne walioongoka na katika zama za waliofuata baada yao, na kupitia kuregelea seerah na njia ambayo yeye (saw) alibeba da’wah kutoka wakati alipoanza mpaka alipo simamisha dola Madina.
Licha ya Uislamu kuwa ni mfumo wa kiulimwengu, lakini njia yake haimruhusu yeyote kuifanyiakazi kiulimwengu tokea mwanzoni.
Amiri wa Hizb utTahrir ni Alim, Sheikh Ata Abu Rashta (majina kamili Sheikh Abu Yasin Ata ibn Khalil ibn Ahmad ibn Abdul Qadir al-Khatib Abu Rashta). Ni mwanasheria, mwanachuoni na mwandishi wa Kiislamu.
Kazi ya Hizb ut Tahrir ni kubeba da’wah ya Uislamu ili kubadilisha hali ya mujtama fisidifu ili kuugeuza kuwa mujtama wa Kiislamu.