Jumatatu, 25 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

DVD “Amali za Kimataifa za Hizb ut Tahrir katika Kuinusuru Gaza!”

Kwa kuzingatia matendo ya kishujaa ya mujahidina katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina mnamo 7 Oktoba 2023, chini ya kauli mbiu ya “Kimbunga cha Al-Aqsa,” dhidi ya umbile nyakuzi la Kizayuni, ambalo limeendelea katika uvamizi wake dhidi ya Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa na kuzingirwa kwake na mashambulizi ya mabomu yanayoendelea ya Ukanda wa Gaza kwa zaidi ya miaka 19, umbile hilo limefichuliwa jinsi lilivyo: umbile la kuchukiza, msingi wake ni dhaifu kuliko utandu wa buibui.

Na kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yameendelea kwa zaidi ya miaka miwili, yanayofanywa na umbile la Kizayuni (kwa usaidizi wa moja kwa moja wa Marekani) dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, na kusababisha kuuawa shahidi, kujeruhiwa, na kutoweka kwa zaidi ya Waislamu 220,000 hadi sasa, Wazayuni wamefichuliwa mbele ya rai jumla ya umma ya kimataifa, wakifichua asili yao ya uhalifu.

Kwa mnasaba wa kupita miaka miwili ya vita vinavyoendelea vya umbile nyakuzi la Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inawasilisha kwa watetezi wake, wafuasi, na wageni kwenye tovuti zake na inasimulia kazi hii kubwa, yenye kichwa:

“Amali za Kimataifa za Hizb ut Tahrir katika Kuinusuru Gaza.”

Ina mkusanyiko mkubwa wa amali, matembezi, makongamano, semina, na machapisho yaliyoandaliwa na kutolewa na Hizb ut Tahrir katika maeneo yake ya utendaji kote ulimwenguni katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kwa kuinusuru Gaza haswa, na ardhi iliyobarikiwa (Palestina) kwa jumla. Katika amali hizi, Hizb ut Tahrir ilitoa wito kwa majeshi ya Ummah wa Kiislamu kutangaza jihad na uhamasishaji wa jumla ili kuwanusuru Waislamu wanaokandamizwa katika ardhi iliyobarikiwa (Palestina) na kuukomboa Msikiti wa Al-Aqsa uliobarikiwa na Palestina yote inayokaliwa kimabavu, kutoka mto wake hadi bahari yake, kutokana na uchafu wa Mayahudi wauaji na wahalifu. Ilitoa wito wa kung'olewa kwa umbile lao kubwa na kuangamizwa kabisa kutoka kwa uso wa dunia. Ilihimiza majeshi ya Ummah kufanya kazi kwa bidii na kwa dhati pamoja na Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu, na kuipa nusra kwa ajili ya kusimamisha dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume ambayo itafufua maisha kamili ya Kiislamu, kulinda matukufu ya Waislamu, kuhifadhi maisha yao, na kuwatunza kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyoamuru. Na huenda siku hii ikawa hivi karibuni.

Ijumaa, 21 Jumada al-Akhir 1447 H, sawia na 12 Disemba 2025 M

Imeandaliwa na Idara ya Machapisho na Kumbukumbu

katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Kupakua DVD Hii

(40 GB)

Bonyeza Hapa

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

#ArmiesToAqsa

#AqsaCallsArmies

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu