Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kampeni ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:

“Janga la Korona Baina ya Uislamu na Urasilimali!”

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
                              Kampeni Pana ya Kiulimwengu kwa Anwani:                                 

“Janga la Korona Baina ya Uislamu na Urasilimali!”

Virusi vya korona (Covid-19) vimeenea ulimwenguni mashariki na magharibi, vimesimamisha mambo ya kimaisha ya kila siku, na watu wenyewe wametii kujifungia ndani majumbani mwao kwa hofu ya maambukizi, swala za Ijumaa na jamaa zimesimama, hata Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu (Msikiti wa Makkah) na msikiti wa Mtume wake (saw) iko mitupu bila ya wafanyaji Umra wala wanaoswali, hali ambayo hawezi akaifikiri mchambuzi mahiri na mtafiti bora duniani! Yote haya ili ithibiti kauli ya Mola wetu mwenye izza na utukufu: “Na mwanadamu ameumbwa kuwa ni dhaifu”

Hakika ya walimwengu wote wanakabiliana na janga hili na wana haja kubwa sana ya uangalizi wa uhakika kutoka kwa Dola yenye kushughulikia kikweli mambo ya watu, ambao wana haja ya Dola yenye kushughulikia ubinadamu na sio mada na faida tu. Binadamu leo anahitaji Khalifah atakaye yachukulia maradhi kuwa ni kadhia ya kibinadamu awali kabisa bila ya kuangalia dini zao, madhehebu yao na asili zao. Na sio kadhia ya kiuchumi yenye manufaa yenye kutegemea katika utatuzi wake upeo wa manufaa ya nchi binafsi, kama ilivyotokea katika nadharia ya “Kinga ya Watu” ambayo Uingereza ilitaka kuifanyia kazi katika janga hili la korona.

Dunia leo inahitaji uongozi mpya wa kiulimwengu ili kuwatoa watu kwenye kiza na kuwapeleka kwenye nuru na kutoka katika jeuri ya usekula na urasilimali wake na kuwapeleka kwenye uadilifu wa Uislamu na Dola yake (Khilafah ya Uongofu ya pili kwa njia ya Utume). Na hakika muda wake umefika kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu zisizoshindwa na Mwenye kuhimidiwa, na hasa baada ya kupita miaka 99 tangu kufutwa kwa nidhamu ya Khilafah ambayo ilikuwa ikitumiwa na Dola ya Uthmaniyya, na hilo sio zito kwa Mwenyezi Mungu. “Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kutimiza jambo lake, hakika Mwenyezi Mungu amejaalia kila kitu kwa kadari maalumu”.

Na katika ukurasa huu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tutafanya kampeni pana kwa ajili ya kila kinachochapishwa na Hizb ut Tahrir ulimwenguni kuhusiana na janga la virusi vya korona (Covid-19). Na Mwenyezi Mungu (swt) ndiye Mwenye kuwafikisha, Mlinzi mzuri na Mwenye nusra nzuri.

Ijumaa, 3 Shaaban 1441 H sawia na 27 Machi 2020 M

-Fuatilia Kampeni kwa Lugha Nyingine-

 Jibu la Swali
Athari za Virusi vya Korona

02 Sha’ban 1441 H sawia na 26/3/2020 M

[Al-Waqiyah TV]

-Kipindi cha Mambo ya Ummah-

“Korona Yaangusha Fikra ya Kirasilimali Kwa Pigo la Kuimaliza”

Wageni:

Mhandisi Salah Eddine Adada (Abu Mohammad)
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Na

Daktari Yusuf Al Haj Yusuf

Mwanachama wa Hizb ut Tahrir Uingereza

Muongozaji wa Kipindi

Ustadh Adnan Mazyan

Jumamosi, 19 Rajab 1441 H sawia na 14 Machi 2020 M

[Al-Waqiyah TV]

-Mjadala Mubashara-

“Korona… Vita vya Kibaiolojia au Mwenendo wa Kimaumbile?!”

Mjadala na Mhandisi Salah Eddine Adada (Abu Mohammad)
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

 

Alhamisi, 19 Jumada al-Akhira 1441 H sawia na 13 Februari 2020 M

   
  
 Alama Ishara za Kampeni   

      
   

 

#Korona    tw  instagram
 #Covid19   tw  instagram 
كورونا#    tw  instagram

-Taarifa kwa Vyombo vya Habari-

Katika Janga hili, Lazima tumtegemee Mwenyezi Mungu (swt), Tutafute rehma zake (swt), na Tukimbilie Kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (swt)

Jumatatu, 28 Rajab I 1441 H - 23 Machi 2020 M

Mkurupuko wa Virusi vya Korona: Janga Jingine Linalo Fichua Madhara ya Urasimali na Tawala zake 

Alhamisi, 24 Rajab 1441 H - 19 Machi 2020 M

Kuzuia Kuenea Kwa Virusi vya Korona ni Jukumu la Kisheria

Jumatano, 23 Rajab 1441 H - 18 Machi 2020 M

-Makala na Maoni ya Habari-

Athari za Virusi vya Korona

Alhamisi, 2 Sha'aban 1441 H - 26 Machi 2020 M

Vichwa vya Habari – 25/03/2020

, 1 Sha'aban 1441 H - 25 Machi 2020 M

                             Urasilimali Hudanganya na Kuhofisha kwa Maslahi ya Kidunia! 

28 Rajab 1441 H - 23 Machi 2020 M 

Mfumo wa Kisekula Hauwezi Kupambana na Virusi vya Korona

Jumapili, 19 Rajab 1441 H -

-Video zilizorekodiwa-

Virusi vya Korona vinathibitisha mambo mawili!
 Ustadh Munzir Abdullah
Mwanachama wa Hizb ut Tahrir Denmark

Jumanne, 29 Rajab 1441 H sawia na 24 Machi 2020 M

[Al-Waqiyah TV]

-Maoni ya Kisiasa-

“Athari ya Korona katika Nidhamu ya Kimataifa”

Mwanafikra wa kisiasa Ahmad al-Khatwan (Abu Hamza)

Bait al-Maqdis – Ardhi yenye Baraka (Palestina)

Jumatano, 23 Rajab al-Muharram 1441 H sawia na 18 Machi 2020 M

-Kuangaziwa na Vyombo vya Habari-

 

 

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 06 Aprili 2020 19:30

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu