Ijumaa, 20 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Sheria ya Kupambana na Upotoshaji wa Habari

Sheria ya Kupambana na Upotoshaji wa Habari, pia inaitwa Sheria ya Mitandao ya Kijamii, imepitishwa na Bunge Kuu la Uturuki na kuanza kutekelezwa. Kwa mujibu wa sheria hii, mtu yeyote anayesambaza hadharani taarifa zisizo za kweli kuhusu usalama wa ndani na nje, utangamano wa umma na afya kwa jumla ya nchi kwa njia inayozua wasiwasi, hofu au kuogopa miongoni mwa umma kwenye mitandao ya kijamii kwa njia inayoleta usumbufu kwa amani ya umma ataadhibiwa kwa kifungo kuanzia cha mwaka 1 hadi miaka 3.

Soma zaidi...

Vichwa vya Habari 28/10/2022

Kwa maana hiyo, kupanda kwa Sunak ni mafanikio makubwa yasiyopingika, iwe unakubaliana na siasa zake au la. Bila kuwa na uwezo wa kudai aina yoyote ya historia ya kuwa mhamiaji mzuri zaidi, Sunak bado amekaidi uwezekano kama mtu wa Asia kufika nafasi ya juu zaidi nchini. Safari yake ni ukumbusho wa jinsi Waingereza weusi na kahawia wanapaswa kupigana dhidi ya mkondo ili kuchukuliwa kwa uzito.

Soma zaidi...

Miitiko ya Kisiasa kwa Wadhifa wa Kiislamu wa Hizb ut Tahrir Inathibitisha Kufilisika kwa Demokrasia

Mnamo Oktoba 7, 2022, Hizb ut Tahrir / Denmark ilichapisha kipeperushi chini ya kichwa "Waislamu Wapendwa - Demokrasia iliyokumbwa na mgogoro ni dhidi ya Uislamu wenu. Msishiriki katika tambiko lisilo na maana la uchaguzi!" Mbali na kuashiria mgongano wa wazi kati ya Uislamu na demokrasia, kipeperushi hicho, ambacho kimesambazwa katika miji kadhaa, kina ukosoaji kadhaa wa demokrasia ya kisekula

Soma zaidi...

Mauaji ya Nablus, na Ushujaa wa watu wake, Yafichua Wazembe, na Kutuma Ujumbe kwa Majeshi ya Kiislamu!

Mujahidina watano waliuawa shahidi, akiwemo mmoja wa viongozi mashuhuri wa kundi la Areen Al-Asoud (Shimo la Simba), Wadih al-Hawah, na wengine zaidi ya 20 walijeruhiwa kwa risasi za jeshi la Mayahudi. Majeraha ya watano kati yao yalielezewa kuwa mabaya, wakati wa shambulizi kwenye Mji wa Kale wa Nablus.

Soma zaidi...

Kwa Ujumbe wa Hamas Uliomzuru Muuaji Bashar “Jitahidini na Iman, pindi Zitakapotokea Fitna katika Ash-Sham”

Kwa masikitiko makubwa, tulishuhudia ujio wa ujumbe wa Hamas na makundi ya Wapalestina unaoongozwa na Khalil Al-Hayya katika ziara rasmi ambayo ni ya kwanza baada ya Hamas kutangaza mnamo Septemba 15 kwamba itarejesha uhusiano wake na utawala haramu wa Baathi na kurejea kifuani mwa mhalifu Bashar, baada ya mpasuko ambao uliendelea tangu 2012, wakati mkuu wa afisi ya kisiasa ya vuguvugu hilo...

Soma zaidi...

"Uvumilivu" wa Watawala wa Ghuba Unajumuisha Vipengee na Sheria zote Isipokuwa Uislamu na Waislamu!

Chini ya kichwa cha urongo cha "Uvumilivu", watawala wa Imarati walizindua hekalu jipya la moja ya dini za kikafiri katika eneo la Jebel Ali. Hapo awali walitotora hisia za Waislamu walipofungua makanisa kadhaa kwa ajili ya Wakristo, na pia sinagogi la Mayahudi. Yalikuwa yameundwa na wizara iitwayo Wizara ya Uvumilivu mnamo 2016 ili kupigia upatu ufunguzi wa mahekalu ya ziada ya makafiri chini ya kichwa cha “Uvumilivu.”

Soma zaidi...

Watoto wa Palestina Wanalilia Majeshi ya Waislamu

Tangu mwanzoni mwa 2022, zaidi ya watoto 45 wa Kipalestina wameuawa shahidi, na uvamizi wa Kiyahudi umeongezeka katika Ukingo wa Magharibi na Jerusalem, katika wiki chache zilizopita, ambao umesababisha vifo vya watoto zaidi, wa mwisho wao akiwa ni mtoto Mahmoud Al-Samoudi, mwenye umri wa miaka 12, ambaye alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu