Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 415
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Huku Kenya ikigubikwa na mrundiko wa deni la jumla ya Sh.10 trilioni, Rais William Ruto awataka wakenya wawe wakilipa ushuru vilivyo. Kulingana na rais serikali inanuia kukusanya Sh.2 trillioni kwa mwaka ujao. Rais amewataka raia wawe na tabia ya kulipa ushuru ipasavyo ili kusaidia serikali kulipa deni lake na kuikomboa kutokana na zigo hili.
Marekani inajiandaa kutuma ndege sita zenye uwezo wa nyuklia aina ya B-52 bombers kwenye kambi moja ya anga kaskazini mwa Australia, kulingana na Shirika la Utangazaji la Australia (ABC). Ikinukuu nyaraka za Marekani, ABC iliripoti kwamba Washington ilikuwa imeandaa mipango ya kina ya kuunda huduma maalum kwa ajili ya ndege hiyo katika Kambi ya Anga ya Tindal, takriban maili 185 kusini mwa jiji la Darwin katika Wilaya ya Kaskazini ya Australia.
Mara baada ya Sheikh Hasina kuwataka wananchi wajiandae kwa matumizi ya taa za kandili-karabai, ndipo mshauri wake wa masuala ya kawi Taufiq-e-Elahi akawashauri watu wachukue ahadi ya kutotumia umeme mchana.
Hizb ut Tahrir Wilayah ya Kenya imechapisha toleo jipya la Jarida la UQAB kwa ajili ya mwezi wa Novemba 2022 M.
Sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan tunafurahi kutoa mwaliko kwa ndugu katika vyombo vya habari, wanasiasa, na wasomi kuhudhuria na kushiriki katika Mkao wa Kadhia za Ummah wa kila mwezi, ambao unashughulikia masuala ya kisasa
Serikali ya rais haikutosheka na kutia saini hati ya mpito kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ili kukaza mshiko wake kwa nchi hii na wananchi, wala haikutosheka na kutoa rushwa kwa Chama Kikuu cha Wafanyakazi cha Tunisia kwa ushiriki wake katika uhalifu wa kujisalimiisha kwa masharti ya IMF na dozi yake hatari, wala haikutosheka na kuzua mashtaka ya kidulma na ya kirongo dhidi ya wanachama wa Hizb ut Tahrir kuidhoofisha hizb na kuishughulisha ili isifichue njama zake na duara za kikoloni na zan zao za kifedha. Haikutosheka na yote hayo.
Migogoro ambayo Misri inakumbwa nayo si mipya wala si matokeo ya sadfa. Badala yake, ni mkusanyiko wa migogoro, baadhi yake ikiburuza mengine, iliyosababishwa na urasilimali ulioitawala Misri kwa miongo kadhaa, na zana zake, wasaliti vibaraka.
Sehemu ya khutba ya Ijumaa ya Sheikh Yusuf Makharza (Abu Hammam).
Mnamo tarehe 10 Oktoba 2022, Waziri Mkuu wa Malaysia alitangaza kulivunja Bunge la 14 ili kutoa nafasi kwa Uchaguzi Mkuu wa 15. Tangazo hili linahitimisha uvumi na makisio ambayo yalikuwa yamekua makali zaidi tangu Septemba.