Alhamisi, 19 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  10 Rabi' I 1447 Na: 07 / 1447
M.  Jumanne, 02 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Iwe ni Suala la Mafuriko au Kashmir, Suala la Uchumi au Kukaliwa Kimabavu kwa Mito Yetu na Dola ya Kibaniani —Je, Tutaendelea Kungoja ‘Jumuiya ya Kimataifa’ Mpaka Lini Kutatua Matatizo Yetu?

(Imetafsiriwa)

Baada ya mafuriko makubwa katika majimbo ya kaskazini ya Khyber Pakhtunkhwa, hasa katika Buner na maeneo ya karibu, ambapo mamia ya watu walipoteza maisha na nyumba, mifugo, mali na magari kusombwa na maji, mafuriko mapya sasa yanapitia Punjab na baadaye yataelekea Sindh. Hapo awali, Karachi pia ilikumbwa na mvua kubwa. Tunamuombea Mwenyezi Mungu Mtukufu usalama na kheri, kwani pamoja na utabiri zaidi wa mvua, watawala wetu wameinua mikono juu tu na kuliacha suala zima kwa rehema ya jumuiya ya kimataifa. Wanaendelea kuwasilisha suala hili zima kwa namna ambayo ni kana kwamba haya ni mabadiliko ya tabianchi ambayo hayawezi kudhibitiwa kabisa na wao, na ikiwa ‘jumuiya ya kimataifa’ haitaingilia kati, wataachwa bila msaada kabisa – kana kwamba ulinzi wa maisha na mali ya watu wao sio jukumu lao bali ni la mfumo wa kimataifa!

Kwa watawala hawa, masaibu ya mamilioni ya watu si chochote ila ni fursa nyengine ya kukusanya michango na sadaka kutoka duniani kote kwa kisingizio cha misaada—fedha ambazo kwa kweli hutumika kujaza hazina zao. Katika muongo mmoja uliopita, Pakistan imekuwa ikipokea kwa wastani kati ya dolari bilioni 1.4 hadi bilioni 2 kila mwaka katika ufadhili wa tabianchi. Hasa baada ya mafuriko ya 2020, Pakistan ilipokea dolari bilioni 4 mwaka 2021. Pakistan tayari imeweka matakwa mbele ya jumuiya ya kimataifa ya ufadhili wa tabianchi mara nane zaidi ya kile inachopokea sasa, dolari bilioni moja ambayo iko chini ya Mpango wa Ustahimilivu na Uendelevu wa IMF unaolenga kukabiliana na tabianchi na udhibiti wa hatari ya maafa. Mnamo 9 Januari 2023, Kongamano la Kimataifa la Pakistan juu ya Ustahamilivu wa Tabianchi ulifanyika jijini Geneva, ambapo ahadi zinazozidi ombi la Pakistan la dolari bilioni 8 zilitolewa, ingawa hadi leo hii hata 20% ya hizo hazijatimizwa. Hivyo, badala ya kuchukua jukumu la kusuluhisha suala hilo, watawala wameibebesha mzigo huo jumuiya ya kimataifa na kuridhika na kukwapua sehemu za fedha walizopokea kwenye hazina zao wenyewe.

Suala hili haliishii kwenye mafuriko pekee bali linaakisi dira ya kudumu ya watawala hawa. Kipote cha watawala wanaamini kwamba suluhisho la matatizo yetu liko mikononi mwa mfumo wa kimataifa pekee, ambao bila msaada na mwongozo wake hatuna nguvu au uwezo wa kuyatatua. Watawala na watungaji sera wetu huutazama utungaji sera na utatuzi wa matatizo wa Magharibi kwa mshangao na wanazingatia kuning’inia kwake kama kipimo cha maendeleo, hadhara, na taaluma – hakika, wengi wao wamefunzwa nao moja kwa moja. Ni ‘dira’ hii haswa ambayo huzipa dola za kimataifa njia ya kuingilia kati katika masuala yetu na kulazimisha ajenda zao kulingana na sera zao. Iwe ni kuliacha suala la Kashmir kwa Umoja wa Mataifa, au kutafuta kutoka nje utekelezaji wa Mkataba wa Maji wa Indus kwa Benki ya Dunia, ni matokeo ya dira hii. Iwe ni nakisi ya sasa ya kiuchumi, upungufu wa mapato ya serikali, au mgogoro wa nishati, watawala wetu, chini ya dira hii, wameweka ajenda na maagizo ya IMF. Kutokana na dira hii hii, haki za makundi mbalimbali ya kijamii mara kwa mara hutungwa kwa mujibu wa ajenda za Ulaya na Marekani, na hivyo kuchochea maandamano ya kuendelea kutoka kwa watu wa Pakistan. Ndani ya taasisi zetu muhimu zaidi za serikali, uingiliaji kati unatekelezwa kwa jina la “mageuzi ya kitaasisi,” kama inavyoamriwa na Benki ya Dunia au Benki ya Maendeleo ya Asia. Kuhusu sera za kijeshi na ulinzi za Pakistan, mizozo ya mipaka, au mkakati wa Afghanistan—hizi zinasimamiwa moja kwa moja na Pentagon, CENTCOM, na Wizara ya Kigeni ya Marekani, huku watawala wetu wakiendelea kuwiana nazo. Matokeo ya dira hii, ubwana wetu umewekwa rehani kwa mfumo wa kimataifa. Kinaya ni kwamba watawala hawa, kwa sababu ya dira hii ya utumwa, wanajaribu kuficha kufeli kwao kutatua matatizo ya kitaifa kwa kuyatangaza kuwa ni “matakwa ya Mwenyezi Mungu.” Laiti wangekuwa na ujasiri wa kiakhlaki wa kukiri kufeli kwao!

Kwa mujibu wa Uislamu, Khalifa ana jukumu la kusimamia mambo yote ya watu, na hawezi kukabidhi jambo lolote la Waislamu kwa mamlaka ya kikafiri. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur’an: [وَلَن يَجْعَلَ اللَّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا] “wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [An-Nisa: 141].

Aya hii inataka kwa waziwazi kwamba Waislamu lazima wasiwape makafiri mamlaka juu ya jambo lolote kati ya mambo yao, na kufanya hivyo ni haramu kabisa. Khalifa ataikataa dira hii ya kitumwa na kuchukua jukumu la moja kwa moja kwa mambo yote ya Waislamu.

Kwa mujibu wa nyaraka zetu za sasa za bajeti, Pakistan inalipa rupia trilioni 8.2 katika malipo ya riba. Khalifa atasitisha matumizi ya nafasi hii ya fedha kwa malengo kama hayo yaliyokatazwa na haramu na badala yake atatumia kutekeleza miradi ya muda mrefu ya kulinda maisha na mali ya Waislamu dhidi ya mafuriko na majanga mengineyo. Bila ya kuwaondoa watawala wa sasa na dira yenye saratani ya utumwa wanayoiwakilisha, hakuna njia ya wokovu kwa Waislamu wa Pakistan.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu