Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 420
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo Novemba 24, 2022, BBC iliripoti juu ya uhaba mkubwa wa chakula ambao unakumba Afghanistan. Mgogoro huo ni kiasi kwamba Abdul Wahab, baba mmoja wa kijijini, ananukuliwa akisema, "Watoto wetu wanaendelea kulia, hawalali, hatuna chakula. Kwa hiyo tunakwenda kwenye duka la dawa, tunachukua vidonge na kuwapa watoto wetu, hivyo wanahisi kusinzia."
Mnamo tarehe 16 Novemba 2022, gazeti la Telegraph iliripoti juu ya dhurufu za ndoa ya kulazimishwa ambayo inawasibu wanawake wa Kiislamu huko Turkestan Mashariki. Makala hayo yana kichwa "Wachina walipwa kuwaoa Waislamu katika mpango wa kuwaangamiza Wauyghur".
Vita nchini Ukraine vimefichua udanganyifu mkubwa katika udhibiti mpya wa hifadhi za silaha baada ya Vita Baridi, na kuacha baadhi ya nchi zikijitahidi kukabiliana na mahitaji ya ulinzi. Ujerumani imekuwa ikikabiliwa na shinikizo la kudumisha dhamira yake ya ulinzi kwa NATO huku ikiipa Ukraine silaha zinazohitajika ili kukabiliana na Urusi.
Kwa kujibu maneno ya Luteni Jenerali Upendra Dwivedi wa India na Waziri wa Ulinzi Rajnath Singh, ni wakati sasa wa uongozi wa kijeshi wa Pakistan kuchukua hatua madhubuti. Maneno matupu kamwe hayatoshi, wakati hatua ndizo zinazohitajika, kujibu vitendo vya adui.
Akizungumza katika kikao cha Mazungumzo Maalum cha Jukwaa la 8 la Mazungumzo ya Mediterania, Waziri wa Mambo ya Nje Mevlüt Çavuşoğlu alisema, “Itakuwa ni makosa kufikiria kuwa kuhalalisha mahusiano na Israel ni usaliti kwa kadhia ya Palestina.”
Huku India ikipitia baadhi ya maonyesho muhimu ya uchaguzi katika majimbo yake tofauti tofauti kama Himachal Pradesh, Gujarat na uchaguzi mkuu wa ndani lakini wenye hisa nyingi kwa Mashirika ya Manispaa ya Delhi, inakuwa chanzo cha masuala machafu, yenye uvundo na ugomvi ambayo ni sarafu za uchaguzi zenye uwezo wa kununua tena kura ili kusaidia kuunga mkono mfumo uliofeli.
Katikati ya mateso ya wananchi kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu na kuzorotesha uzalishaji viwandani kutokana na tatizo la umeme, serikali ya Hasina danganyifu imeamua kuongeza bei ya umeme kwa asilimia 19.92 hadi Tk6.20 kWh kutoka bei ya awali ya Tk5.17 kWh. kwa kutii agizo la Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF).
Ufilipino ndiyo nchi yenye uzalishaji mkubwa zaidi wa nyenzo za unyanyasaji wa watoto. Mashirika ya kutoa misaada yamekadiria kwamba mtoto 1 kati ya 5 hudhulumiwa, na kwa kawaida wazazi na watu wa ukoo hufaidika kutokana na unyanyasaji huo. Kufungwa kwa miji wakati wa Janga la maambukizi kuliwaacha watoto walio hatarini wakiwa wamenaswa na watu wazima walio na tamaa ya kifedha.
Pamoja na mabadiliko katika amri ya jeshi la sita kwa ukubwa duniani, mjadala ulizushwa ndani, nchini Pakistan, na kiulimwengu, juu ya dori ya taasisi yenye nguvu ya kijeshi na mkuu wake wa jeshi. Mengi yamejadiliwa kuhusu urithi wa wakuu wa jeshi, waliomtangulia Jenerali Syed Asim Munir, Mkuu wa Jeshi wa Kumi na Saba wa jeshi la nyuklia, la tisa kwa nguvu zaidi duniani.