Jumapili, 02 Safar 1447 | 2025/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Mateso ya Wanawake wa Gaza Waliodhulumiwa, je wana Mlipizaji Kisasi? na je Umma wa Kiislamu Umepoteza Mu’tasem wake?!

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ilifichua mnamo Jumatatu kwamba idadi kadhaa ya wanawake na wasichana katika Ukanda wa Gaza wamebakwa na jeshi la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu. Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema leo kuwa wataalamu wake wana wasiwasi kuhusu ripoti zinazoonyesha kuwa wanawake na wasichana wa Kipalestina wanaoshikiliwa mateka wamekuwa wakifanyiwa vitendo mbalimbali vya unyanyasaji wa kingono.

Soma zaidi...

Uamuzi wa Houthi wa Kuziainisha Marekani na Uingereza kama Maadui wa Yemen

Mehdi Al-Mashat, Rais wa Baraza Kuu la Kisiasa, alitoa uamuzi mnamo Jumatatu, 19/02/2024, kuziainisha Marekani na Uingereza kuwa nchi mbili zenye uadui dhidi ya Yemen. Uamuzi huo ulikuja baada ya kupitishwa kwa sheria katika Bunge la Wawakilishi jijini Sana'a, na muda mfupi baada ya kuainishwaji wa Mahouthi kama "kundi maalum lililoundwa la kigaidi la kimataifa."

Soma zaidi...

Kinachopaswa kufanywa na Misri na Jeshi Lake ni Kuvunja Mipaka na Kuling'oa Umbile la Kiyahudi, Sio Kutafuta Usitishaji Vita na Kutoa Misaada!

Balozi Ahmed Abu Zaid, msemaji rasmi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, alisisitiza kuwa ‘Israel’ lazima ikomeshe ukiukaji wake, akithibitisha kuwa Israel inakiuka sheria za kimataifa. Alidokeza kuwa maamuzi ya haki ya kimataifa yanaifunga ‘Israel’.

Soma zaidi...

Nini Kinachotofautisha Uteuzi wa bin Mubarak kutoka kwa bin Abdul Malik katika Serikali ya Aden?!

Mnamo tarehe 6/2/2024, uamuzi ulitolewa na Baraza la Rais mjini Aden kumteua Ahmed Awad bin Mubarak kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya Aden, akimrithi Maeen Abdul Malik. Uteuzi wa Ahmed bin Mubarak umekuja baada ya Baraza la Rais kufeli katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wake kuafikiana juu ya idadi ya wagombea wa nafasi ya uwaziri.

Soma zaidi...

Kisimamo cha Familia za Mashababu Wanaozuiliwa wa Hizb ut Tahrir mbele ya Bunge la Wawakilishi

Familia za Mashababu wa Hizb ut Tahrir nchini Jordan, wanaozuiliwa na Mahakama ya Usalama ya Serikali, walifanya walilaani mbele ya Bunge la Wawakilishi, asubuhi ya leo, Jumatano 14/02/2024, ambapo waliitaka Afisi ya Mkuu wa Bunge la Wawakilishi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uhuru wa Umma na Haki za Kibinadamu kufanya kazi na kuwasiliana na wale wanaohusika kwa ajili ya kuachiliwa huru mara moja kwa watoto wao waliowekwa kizuizini kwa sababu ya kutoa maoni yao ambapo hawakufanya kitendo chochote cha kigaidi, au uhalifu wowote kwa sheria za usalama wa serikali.

Soma zaidi...

Ni Nani Atakayefuta Aibu Yenu, Enyi Wanajeshi wa Kinana?!

Baada ya mkuu wa ujasusi wa Misri kuwaonya Hamas juu ya ulazima wa kukubali makubaliano ya kubadilishana wafungwa yaliyoandaliwa chini ya mwavuli wa Marekani ndani ya wiki mbili, na kisha tangazo la redio ya jeshi la umbile la Kiyahudi kwamba Misri ingekubali kuivamia Rafah kwa masharti ya kuhakikisha kuwa Wapalestina hawafurushwi hadi Sinai, pia mnamo Jumapili asubuhi, tarehe 11/2/2024, redio hiyo ilinukuu maafisa wa Misri wakiufahamisha upande wa 'Israel' wa kutoupinga uvamizi wa kijeshi wa Rafah katika mji wa Rafah kwa sharti la kuepuka majeruhi ya raia wa Palestina.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu