Ukiritimba wa Kisiasa wa Vifaa vya Ujenzi Zanzibar: Pigo Jengine kwa Masikini
- Imepeperushwa katika Tanzania
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Tunaitahadharisha kwa dhati kabisa serikali ya Zanzibar kuepusha kufadhaisha zaidi sekta ya ujenzi inayofanya maisha ya mtu wa kawaida kuwa magumu zaidi hasa katika harakati zao za kumiliki nyumba. Kwa kufanya na kusababisha hali ya ugumu na ukali katika maisha ya watu ni dhulma za wazi kwa raia na khiyana kwao na itahesabiwa vikali na Mwenyezi Mungu Mtukufu kesho Akhera na kufanya mambo kuwa magumu zaidi katika maisha haya.



