Jumanne, 13 Shawwal 1447 | 2026/03/31
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa

Amiri wa Hizb ut Tahrir

Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah katika Ukurasa Wake wa Kifikra wa Facebook
Jibu la Swali

Nusra (Msaada) Inatafutwa Kutoka Kwa Nani?!

Kwa: Ammar Samman

(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh

Mwenyezi Mungu akubariki na akuongoze. Swali langu kwa Amir, ikiwa utakuwa mkarimu, linahusu kutafuta Nusra (msaada).

Je, kuwasilisha Uislamu kama mradi wa hadhara kunahusiana tu na maeneo yenye nguvu ndani ya nchi za Kiislamu pekee? Au pia kunahusisha nchi zisizo za Kiislamu, kama alivyofanya Mtume Muhammad (ﷺ)?

Ningependa Sheikh wetu ajibu swali hili kwa msingi wa kifiqhi.

Na pia ningependa jibu lichapishwe kwa umma, kwani suala hili linahusiana na uelewa wetu wa njia ya Mtume Muhammad (ﷺ).

Mtoto wako na ndugu yako, Abu Muhammad Zaid.

Jibu:

Wa Alaikum Assalam wa Rahmatullahi wa Barakatuh

Tumewahi kujibu maswali yanayofanana hapo kabla. Nitakunukulia yale yanayohusiana na swali lako kutoka jibu letu la tarehe 24/6/2021:

[[ Swali: Sheikh wetu, nina swali tafadhali: inajulikana kuwa Mtume (ﷺ) alitafuta Nusra kutoka kwa makabila, je, Quraysh ilikuwa miongoni mwa makabila ambayo Mtume (ﷺ) alitafuta Nusra kutoka kwao?

Jazakallahu Khair.

Jibu:

Wa Alaikum Assalam wa Rahmatullahi wa Barakatuh,

Kutafuta Nusra (kuomba msaada) kunapaswa kufanywa kwa yule anayekubali Uislamu na kuuingia, na ambaye ni miongoni mwa watu wa nguvu na ulinzi, ili aweze kuinusuru dini na kusimamisha utawala kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu. Masharti haya mawili lazima yatimie kwa mnayeitafuta Nusra kwake. Ikiwa hatakubali Uislamu na kuuingia, au si katika watu wa nguvu na ulinzi wenye uwezo wa kuleta mabadiliko, peke yake au pamoja na wengine, basi hatakuwa miongoni mwa watu wa Nusra. Ama Quraysh, haikuwa hivyo kabla ya ufunguzi wa Makka; kwani watu wake wenye nguvu na ulinzi hawakuingia Uislamu wakati huo, hivyo Mtume (ﷺ) hakutafuta nusra yao. Bali alikuwa akilingania katika Uislamu huko Makka, na waliokubali walikuwa ni wanyonge na baadhi ya watu wenye nguvu kama watu binafsi bila makabila yao, hivyo hawakuwa na uwezo wa kuleta mabadiliko, kama Umar na Hamza (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao). Kwa hiyo, hapakuwa na kutafuta Nusra kutoka kwa watu wa Makka kwa sababu masharti hayo mawili hayakutimia. Bali kulikuwa na da’wah ya Uislamu Makka, na hakuna waliokubali kutoka kwa watu wa nguvu na ulinzi wenye uwezo wa kuleta mabadiliko; hivyo hapakuwa na Talab an-Nusra Makka, bali Makka ilifunguliwa kwa ushindi.

Ndiyo maana Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alikuwa akijiwasilisha kwa watu wa nguvu na ulinzi kutoka makabila; alikuwa akiwaalika kwanza katika Uislamu, na wakikubali ndipo anatafuta nusra yao. Miongoni mwa yaliyotajwa katika Sira:

Kwanza: Kutoka Sira ya Ibn Hisham:

1- Kutafuta Nusra kutoka kwa Thaqif:

... Mtume (ﷺ) alipofika Taif aliwaendea wakuu wa Thaqif, akakaa nao na kuwalingania kwa Mwenyezi Mungu na kuwaomba wamnusuru katika kueneza Uislamu... lakini walimjibu vibaya na hawakukubali, hivyo akaondoka kwao bila matumaini.

2- Kutafuta Nusra kutoka kwa Bani Amir ibn Sa’sa’ah:

... aliwalingania kwa Mwenyezi Mungu na kuwaomba nusra. Mmoja wao akasema: “Ikiwa tutakupa bay’ah kisha Mwenyezi Mungu akakupa ushindi, je, tutakuwa na mamlaka baada yako?”

Mtume (ﷺ) akasema: «الْأَمْرُ إلَى اللّهِ يَضَعُهُ حَيْثُ يَشَاءُ» “Mamlaka ni ya Mwenyezi Mungu, huiweka anapotaka.” Wakasema: “Je, tujitoe kupigana na Waarabu kisha ukishinda mamlaka iwe kwa wengine? Hatuna haja na jambo lako.” Hivyo wakamkataa.

Pili: Kutoka kwa Tafsiri ya Ibn Kathir:

[“Kisha tukafika kwenye mkusanyiko uliojaa heshima ambapo kulikuwa na wazee kadhaa wa hadhi ya juu na mashuhuri. Abu Bakr aliwakaribia na kuwasalimia. Ali alisema: Abu Bakr alikuwa mtu wa kuchukua hatua katika kila tendo jema. Abu Bakr akawaambia: Nyinyi watu mnatoka wapi? Wakasema: Kutoka kabila la Banu Shayban bin Tha’laba. Kisha Abu Bakr akamgeukia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kusema: “Baba yangu na mama yangu na watolewe kafara kwa ajili yako! Hakuna mtu mwenye heshima zaidi katika kabila lao kuliko hawa!”

Mafrooq akasema: Unalingania nini, ewe kaka Mquraysh? Kisha Rasulullah (saw) akasongea mbele na kukaa, Abu Bakr akasimama na kumfunika Rasulullah (saw) kwa nguo zake. Rasulullah (saw) akasema:

«أَدْعُوكُمْ إِلَى شَهَادَةِ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، وَأَنِّي رَسُولُ اللَّهِ، وَأَنْ تؤوونىوَتَمْنَعُونِي وَتَنْصُرُونِي حَتَّى أُؤَدِّيَ عَنِ اللَّهِ الَّذِي أَمَرَنِي بِهِ، فَإِنَّ قُرَيْشًا قَدْ تَظَاهَرَتْ عَلَى أَمْرِ اللَّهِ، وَكَذَّبَتْ رَسُولَهُ، وَاسْتَغْنَتْ بِالْبَاطِلِ عَنِ الْحَقِّ، وَاللَّهُ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ»

“Ninakulinganieni kushuhudia kwamba hakuna anayestahili kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu Mmoja na kushuhudia kwamba mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Pia naomba munipe ulinzi na nusra ili niweze kufikisha ujumbe ambao Mwenyezi Mungu ameniamuru niupitishe, kwa sababu Maquraysh wameungana dhidi ya Dini ya Mwenyezi Mungu; wamemkataa Mtume Wake, na wameridhika na batili badala ya haki. Lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye Kujitegemea, Anayestahiki Sifa zote.”

Muthanna akasema, “Ndugu Mqurayshi! Nimesikiliza ulichosema. Ninapenda ulichosema kwani kimenivutia sana. Hata hivyo, jibu langu kwako litakuwa jibu lile lile ambalo Haani bin Qabeesah ametoa; tunajikuta katikati ya mipaka ya nchi mbili. Moja ni Yamaamah na nyingine ni Samaawah.”

 Rasulullaah (saw) alimuuliza, «وما هذان الصريان؟» “Mko kwenye mipaka ya nchi zipi mbili?” Akajibu, “Upande mmoja nasi tuna ardhi, vilima virefu na milima ya Waarabu huku upande mwingine tuna ardhi ya Wafursi na mito ya Kisra. Kisra imeturuhusu kuishi huko kwa sharti kwamba tusianzishe chochote kipya na tusimuunge mkono mtu yeyote anayeanzisha harakati mpya. Uwezekano ni mkubwa kwamba wafalme wa Fursi hawatapenda kile unachotuitia, ilhali desturi katika nchi ya Waarabu ni kuwasamehe wale watakaokuwa wamekosea na kukubali udhuru wao; desturi ya nchi ya Wafursi ni kwamba watu wanaofanya makosa hawasamehewi wala udhuru wao haukubaliwi. Kwa hivyo, ikiwa mnataka tuwarudishe kwenye nchi yetu na kuwanusuru dhidi ya Waarabu, tunaweza kukubali jukumu hili” Rasulullaah (saw) aliwaambia,

«ما أسأتم الرد إذ أفصحتم بالصدق، إنه لا يقوم بدين الله إلا من حاطه من جميع جوانبه» "Jibu lenu halijawa baya kwa sababu mumesema ukweli. Hata hivyo, watu pekee wanaoweza kusimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu ni wale wanaoilinda kutoka kila pembe.” 24/6/2021] Mwisho wa Nukuu.

Tatu: kama inavyoonekana, Mtume (ﷺ) alikuwa akiwaalika kwanza katika Uislamu kisha anaomba nusra yao. Wakikubali kwa uaminifu na wakawa na nguvu na uwezo wa kusimamisha utawala wa Kiislamu, ndipo anaomba nusra yao. Ama wakitoa masharti ya kidunia, kama kutaka wao watawale baada yake au kuchagua kupigana na baadhi ya watu tu, basi hilo halikubaliwi. Ndiyo maana katika Bay’at al-Aqaba, Ansar walipouliza: “Tutapata nini tukikuhami?” Mtume (ﷺ) akasema: “Pepo.” Hawakuweka masharti ya kidunia.

Katika Sira ya Ibn Hisham (1/446) - Sura kuhusu maneno ya al-Abbas ibn Ubadah kwa Khazraj kabla ya kiapo cha utiifu: [قال ابن إسحاق: وحدثني عاصم بن عمر بن قتادة: أن القوم لما اجتمعوا لبيعة رسول الله ﷺ قال العباس بن عبادة بن نضلة الأنصاري، أخو بني سالم بن عوف: يا معشر الخزرج، هل تدرون علام تبايعون هذا الرجل؟ قالوا: نعم، قال: إنكم تبايعونه على حرب الأحمر والأسود من الناس، فإن كنتم ترون أنكم إذا نهكت أموالكم مصيبة وأشرافكم قتلا أسلمتموه فمن الآن، فهو والله إن فعلتم خزي الدنيا والآخرة، وإن كنتم ترون أنكم وافون له بما دعوتموه إليه على نهكة الأموال وقتل الأشراف فخذوه فهو والله خير الدنيا والآخرة. قالوا: فإنا نأخذه على مصيبة الأموال وقتل الأشراف. فما لنا بذلك يا رسول الله إن نحن وفينا (بذلك)؟ قال: «الْجَنَّةُ». قالوا: ابسط يدك. فبسط يده فبايعوه...] [Ibn Ishaq alisema: Asim ibn Umar ibn Qatada aliniambia: Watu walipokusanyika kutoa kiapo cha utiifu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), al-Abbas ibn Ubadah ibn Nadhlah al-Ansari, ndugu wa Banu Salim ibn Awf, alisema: “Enyi watu wa Khazraj, mnajua mnachotoa kiapo cha utiifu kwa mtu huyu?” Wakasema: “Ndiyo.” Akasema: "Mnatoa kiapo cha utiifu kwake ili kupigana na watu wote, bila kujali rangi. Mkifikiri kwamba ikiwa mali zenu zitapungua na viongozi wenu watauawa, mtamsalimisha, basi fanyeni hivyo sasa. Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, mkifanya hivyo, itakuwa fedheha katika dunia hii na Akhera. Lakini mkifikiri kwamba mtakuwa waaminifu kwa kile mlichomwita, hata kwa gharama ya mali zenu na kupoteza viongozi wenu, basi mchukueni. Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, itakuwa jambo bora zaidi katika dunia hii na Akhera.” Wakasema: “Tutamchukua hata kwa gharama ya mali zetu na hasara ya viongozi wetu. Tutapata faida gani kutokana na hilo, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ikiwa sisi ni waaminifu?” Akasema: “Pepo.” Wakasema: “Nyoosha mkono wako.” Akanyoosha mkono wake nao wakaapa utiifu kwake].

Kwa kumalizia: Nusra hutafutwa kutoka kwa wale wanaokubali Uislamu na kuuingia, na ambao ni watu wa nguvu na ulinzi wenye uwezo wa kuinusuru dini na kusimamisha hukmu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, peke yao au pamoja na wengine. Ikiwa hawatakubali Uislamu au hawana nguvu na uwezo wa kuleta mabadiliko, basi hawahesabiwi kuwa ni miongoni mwa watu wa Nusra.

Natarajia haya yanatosha, na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi na Mwenye hekima. ]] Mwisho wa nukuu.

Ndugu yenu,

Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah

9 Shawwal 1447 H

27/3/2026 M

Link ya Jibu hili kutoka kwa ukurasa wa Amiri wa Facebook: Bofya Hapa

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu