Jumamosi, 21 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Matarajio Yasio na Msingi:
Nchini Uzbekistan, Mhubiri Aliyetoka Nchini Uturuki Ashtakiwa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mahakama ya Jinai ya Wilaya ya Uchtepa ya Tashkent ilianza kusikiliza mnamo Agosti 19 kesi ya jinai dhidi ya mtu wa dini Alisher Tursunov, anayejulikana kwa umma kwa jina bandia la Mubashshir Ahmad. Habari hiyo iliripotiwa na Aziz Abidov, mkuu wa huduma ya vyombo vya habari wa Mahakama ya Upeo ya Uzbekistan. Kulingana na tuhuma ya mashtaka, Tursunov anashtakiwa chini ya vifungu vitatu vya Kanuni ya Jinai ya Uzbekistan, ikiwemo:

- Kifungu cha 156, Sehemu ya 2 – vitendo vya kimakusudi vinavyodhalilisha heshima na hadhi ya taifa, vinatusi hisia za raia kwa msingi wa imani zao za kidini au za upagani, vinavyofanywa kwa madhumuni ya kuchochea uhasama, kutovumiliana, au mifarakano kati ya makundi ya watu kwa msingi wa utaifa, rangi, kabila, au dini...

- Kifungu cha 244-1, Sehemu ya 3, Aya ya "g" - uzalishaji, uhifadhi, usambazaji, au maonyesho ya nyenzo ambazo zinatishia usalama wa umma na utulivu wa umma kupitia matumizi ya vyombo vya habari, mitandao ya mawasiliano ya simu, au Intaneti.

- Kifungu cha 244-3 - uzalishaji haramu, uhifadhi, uagizaji, au usambazaji wa nyenzo za kidini.

Yakichukuliwa kwa pamoja, mashtaka haya yana uwezekano wa kifungo cha muda mrefu gerezani.

Maoni:

Ikumbukwe kwamba Mubashshir Ahmad, kama viongozi wengine wengi wa kidini, aliamini ikhlasi ya ahadi za mageuzi za Rais Shavkat Mirziyoyev baada ya kuingia madarakani. Mnamo mwaka wa 2017, alianzisha kikundi cha Azon New Media, ambacho kilijumuisha tovuti ya Azon.uz, ​​redio ya mtandaoni Azon FM, na televisheni ya mtandaoni ya Azon TV. Tovuti ya Azon.uz ikawa chombo kikuu cha habari cha Uzbekistan kinachoangazia mada za kidini na kielimu.

Mnamo 2021, Mubashshir Ahmad aliripoti shinikizo kutoka kwa Kamati ya Uzbekistan ya Masuala ya Kidini kuhusu sera ya uhariri wa tovuti – jambo ambalo Kamati hiyo ilikanusha hadharani wakati huo. Baadaye, wafanyikazi wa Azon.uz walitozwa faini kwa kuchapisha nyenzo za kidini ambazo, kulingana na mahakama, zinaweza kudhuru uhusiano wa kigeni wa Uzbekistan.

Wakati tovuti hiyo ilipofungwa mnamo Agosti 2023, Mubashshir Ahmad alihamia Uturuki, ambayo – kama watu wengine wengi wa dini – aliona kuwa mahali salama pa kuendelea na kazi yake. Mnamo Novemba mwaka huo huo, alizindua tovuti mpya, Azon Global. Hata hivyo, mwishoni mwa Disemba mwaka huo, watekelezaji sheria wa Uturuki walimtia kizuizini Mubashshir Ahmad, na kumweka katika kituo cha kizuizi. Baada ya miezi kadhaa kizuizini, hatimaye aliachiliwa huru.

Hatimaye, mnamo Februari mwaka huu, vikosi vya usalama vya Uzbekistan vilitangaza kuanzishwa kwa kesi ya jinai dhidi ya Tursunov kwa madai ya “kuunda, kuongoza, au kushiriki katika siasa kali za kidini, za kujitenga, zenye msimamo mkali, au mashirika mengine yaliyopigwa marufuku.” Mnamo Mei, huduma ujasusi za Kituruki zilimtia kizuizini tena, na wakati huu alihamishiwa Uzbekistan haraka.

Kesi ya Mubashshir Ahmad ni mfano kwa wanaharakati wa leo wanaotarajia kupata usalama na fursa kwa kushirikiana na watawala wa nchi za Waislamu. Inasemekana kwamba watawala hao hawana vizuizi vyovyote vya kiakhlaki na wanatenda kwa maslahi ya kibinafsi tu. Ikiwa itawanufaisha kisiasa, hawatasita kumkabidhi Muislamu mwenzao. Na hii bila ya kutaja ukweli kwamba watawala hawa kikweli hawajitawali wenyewe—kwa kiasi kikubwa wanacheza dori waliyopewa na wakoloni wa Magharibi waliowaingiza madarakani.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Mansour

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu