- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Ajifanya Kuijali Palestina, Huku Mikono Yake Ikiloa Damu ya Watu Wasio na Hatia wa Gaza
(Imetafsiriwa)
Habari:
Tarehe 07-09-2025, Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark, Lars Løkke Rasmussen, alisafiri hadi Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kukutana na marafiki zake na wenzake Wazayuni “kuonyesha kujali” na “kutia shinikizo” kwa serikali vamizi ya Kizayuni. Ziara hii ya kirafiki utawala vamizi wa Kizayuni inakuja siku chache tu baada ya Waziri wa Mambo ya Nje huyo kuchapisha video kwenye mtandao wa kijamii, ambapo alitoa maoni kwamba “Serikali ya Denmark sasa inachukua hatua za kuondoa kura ya turufu ya Israel juu ya msimamo wetu [kuhusiana na utambuzi wa baadaye wa Palestina]”.
Maoni:
Baada ya siku 700 za mauaji ya halaiki ya moja kwa moja, mauaji ya kikatili dhidi ya wanawake na watoto, na njaa ya pamoja, ambayo dola ya Denmark inaendelea kutoa vifaa vya kijeshi, na imetoa msaada usiotingishika, Lars Løkke Rasmussen anasafiri hadi Tel Aviv kusema: “Ninajichukulia mimi - na Denmark – rafiki wa ‘Israel’. Lakini rafiki anayejali”
Baada ya serikali ya Denmark kuanzisha ukandamizaji ambao haujawahi kushuhudiwa dhidi ya sauti zinazotaka kukombolewa kwa Palestina, na kushinikiza mamlaka ya mahakama kuibua mashtaka yanayohusiana na ugaidi dhidi ya makumi ya raia na kutoa hukumu kali kwa kuonyesha uungaji mkono watu halali wa Palestina, wakati Wizara hiyo hiyo ya Mambo ya nje ya Lars Løkke Rasmussen, inaendelea kuidhinisha uuzaji wa zana za kijeshi nje ya nchi hadi kwa Wazayuni – yeye sasa, ghafla, “anajali”.
Baada ya kuendesha kampeni za kisiasa zenye lengo la kulingania chuki dhidi ya Uzayuni na chuki dhidi ya Mayahudi na kushambulia vikali madai yoyote ya ushawishi wa Kizayuni kwa wanasiasa wa Denmark, serikali sasa inakiri kwamba msimamo wake kuhusu suala la Palestina hadi sasa umefafanuliwa, sio jijini Copenhagen, bali ndani ya katikati ya utawala vamizi wa Kizayuni.
Kuna, hata hivyo, sababu nzuri za Serikali ya Denmark kujali. Lakini kujali kwake haikuwa kamwe kwa Palestina. Huku matukio yakitokea na hasira ya umma juu ya kuendelea kwa Denmark kuunga mkono mauaji ya halaiki mjini Gaza ikiendelea kuongezeka – hofu inaongezeka ndani ya serikali iliyokumbwa na mgogoro, huku uchaguzi ujao ukikaribia zaidi. Kote barani Ulaya, viongozi wa kisiasa sasa wanapanga foleni kwenye shimo la kisiasa katika majaribio duni ya kunawa mikono yao kwa damu ya Gaza.
Hakuna mtu mzuri na mwenye akili timamu ambaye angekubali hata kidogo maneno matupu ya “kujali” kutoka kwa wafuasi wa mauaji ya halaiki, ambao hata wana ujasiri wa kuamuru – kwa pumzi hiyo hiyo – kwa masharti ya Waislamu wa Palestina kwa mustakabali usio na mauaji ya halaiki!
Waislamu mashujaa wa Ardhi Iliyobarikiwa hawahitaji kujali wala kutambuliwa na watu kama Lars Løkke Rasmussen. Pamoja na wenzake katika Serikali ya Denmark, atakumbukwa milele kama mhalifu fisadi, ambaye kujali kwake pekee kwa kweli ni kazi yake na urithi wake wa kibinafsi, ambao umejaa damu isiyo kauka ya watu wasio na hatia wa Gaza.
Ni pale tu jeshi la Waislamu litakapojikusanya kutoka katika nchi zinazoizunguka Palestina na kukomesha umbile ovu la Kizayuni, ndipo Palestina itakapokombolewa. Na ni pale tu itakapounganishwa na nchi nyingine za Kiislamu kwa umoja chini ya uongozi wa Kiislamu ndani ya Khilafah Rashida, ndipo hapo itakuwa huru kweli kweli.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Elias Lamrabet