Jumamosi, 14 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uagizaji Mchele kutoka Nje: Ukoloni na Uuaji wa Kilimo

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mahakama Kuu ya Kenya hivi majuzi imeondoa marufuku ya serikali ya kuagiza mchele kutoka nje ya nchi bila ushuru, na hivyo kufungua njia kwa wafanyibiashara kulijaza sokoni kwa mchele wa bei nafuu wa kigeni. Ingawa hatua hiyo inaweza kusherehekewa na wengine kama njia ya kupunguza gharama ya maisha, athari zake za kina haziwezi kupuuzwa.

Maoni:

Uamuzi huu sio tu kuhusu mchele; badala yake, ni sehemu ya muundo mkubwa zaidi wa urekebishaji uchumi uliowekwa kwa Kenya kupitia maagizo ya taasisi za fedha za kimataifa kama vile Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF). Taasisi kama hizo zinajionyesha kama waokoaji wa uchumi unaotatizika, lakini yale yanayojulikana kama “masuluhisho” yameundwa kubomoa viwanda vya ndani, kulemaza uwezo wa kujitegemea, na kuimarisha utegemezi. Nchini Kenya, kilimo daima kimekuwa ndio uti wa mgongo wa uchumi. Hata hivyo, kwa kulijaza soko kwa bidhaa za bei nafuu kutoka nje, wakulima wa ndani wanaachwa hawawezi kushindana, maisha yao yanaharibiwa, na msingi wa kilimo wa taifa unadhoofika.

Njia ya Kenya chini ya IMF siyo kwake peke yake. Somalia inatoa mfano wa kusikitisha wa jinsi sera hizi zinaweza kusambaratisha kabisa uti wa mgongo wa uchumi wa taifa. Kwa karne nyingi, uchumi wa wafugaji wa Somalia ulistawi kwa uzalishaji wa mifugo na biashara. Wafugaji waliishi kwa staha, kujitosheleza, na ustahimilivu. Lakini katika miaka ya 1980 na 1990, Somalia ilikabiliwa na IMF na mageuzi ya Benki ya Dunia ambayo yaligeuka kuwa mabaya. Kama sehemu ya Mipango ya Marekebisho ya Miundo (SAPs), masharti yaliyowekwa na IMF na Benki ya Dunia, Somalia ililazimika kuvunja misingi ya uchumi wake wa chakula na mifugo. Serikali nchini Somalia ilipunguza matumizi katika sekta muhimu na kufanya biashara huria, hivyo kuwanyima wakulima wa Somalia ulinzi, na kuwaacha katika hatari ya kuagiza bidhaa za bei duni kutoka nje na hatimaye kuwasukuma kwenye utegemezi.

Kutokana na athari za biashara huria ya IMF, utupaji wa misaada ya chakula uliigeuza Somalia kutoka kuwa nchi ni ya kujitegemea na kuwa moja ya utegemezi sugu. Umaskini ulizidi kuongezeka, njaa ikatokea mara kwa mara, na hadhi ikaondolewa kwani jamii nzima hazikuweza kujiendeleza tena.

Kenya sasa iko hatarini kutembea katika njia hiyo hiyo. Kwa kuruhusu uagizaji kutoka nje wa vyakula vikuu vya nchi kama vile mchele bila ushuru, serikali inaweka mazingira ya kuwaangamiza wakulima wake, kama vile wafugaji na wakulima wa Somalia walivyotelekezwa kwenye umaskini. Kwa muda mrefu IMF imeweka Programu za Marekebisho ya Miundo (SAPs) kama masharti ya mikopo na ulipaji madeni. Programu hizi zinaweza kuonekana kuwa za kiufundi, lakini zinawakilisha udhibiti wa moja kwa moja na njia ya unyonyaji rasilimali.

Athari ni mbaya. Kama vile Somalia, wakulima ambao wakati mmoja walilisha taifa sasa hawawezi kuuza mazao yao, licha ya ahadi tupu za serikali za kuyanunua. Uhalisia unabakia: uagizaji wa bidhaa za bei nafuu utafurika nchini. Sekta ambayo inatoa ajira kwa mamilioni ya watu na kudumisha jamii nzima za vijijini inadhoofishwa kimakusudi. Hii sio bahati mbaya; limeundwa.

Badali pekee ya kweli ipo katika Uislamu, unaotabikishwa kwa ukamilifu kupitia Khilafah. Uislamu hautenganishi uchumi na siasa, wala haulidunishi tatizo la uchumi hadi kuwa takwimu na masoko tu. Badala yake, unalichukulia kama tatizo la kibinadamu ambalo lazima litatuliwe. Uislamu unatoa mfumo wa kiwahyi unaolinda riziki na staha. Khilafah inawajibika kuhakikisha kwamba kila raia anapata chakula, mavazi na malazi. Na hili lilionekana katika zama za Umar ibn ́Abd al-Aziz, Khalifah ambaye alihakikisha kwamba hakuna mtu yeyote katika dola aliyeachwa na njaa. Utajiri uligawanywa kwa haki kiasi kwamba wakusanyaji zaka hawakupata mtu wa kuikubali. Aliagiza kwa maneno haya maarufu: “Tawanyeni chakula juu ya vilele vya milima, ili isisemekane kwamba wanyama walikufa kwa njaa wakati wa utawala wangu.”

Njia pekee ya kutoka katika duara hili ni kukataa mfumo wa kibepari unaolazimishwa na taasisi kama IMF na kukumbatia mfumo ulioteremshwa na Mwenyezi Mungu: Uislamu chini ya Khilafah. Ni hapo tu ndipo usalama wa chakula, heshima na uhuru vinaweza kuregeshwa kwa Ummah.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Musa Kipngeno Rotich – Kenya

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Kuhuisha Uislamu: Njia Pekee ya Kuepuka Majanga

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu