Jumatano, 28 Muharram 1447 | 2025/07/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mkataba wa Biashara na Unyenyekeaji wa Indonesia kwa Maslahi ya Marekani

(Imetafsiriwa)

Habari:

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza makubaliano ya kibiashara na Indonesia, kupunguza ushuru unaotishiwa wa 32% kwa bidhaa za Indonesia hadi 19%. Kwa upande wake, Indonesia ilijitolea kununua nishati ya Marekani kwa dolari bilioni 15, bidhaa za kilimo kwa dolari bilioni 4.5, na ndege 50 za Boeing, ikiwa ni pamoja na aina ya 777. Trump alidai Marekani itapata ufikiaji kamili wa soko la Indonesia bila kulipa ushuru. Makubaliano hayo yalifuatia vitisho vya ushuru wa juu na yalikamilishwa baada ya mazungumzo na Rais wa Indonesia Prabowo Subianto. Bado haijulikani ni lini upunguzaji wa ushuru na ununuzi utaanza kutekelezeka. Biashara ya Indonesia na Marekani ilifikia karibu dolari bilioni 40 mwaka 2024, na nakisi ya biashara ya bidhaa za Marekani ya takriban dolari bilioni 18. Trump amekuwa akisukuma mikataba kama hiyo ya kibiashara na nchi kama Uingereza, Vietnam na China, huku mazungumzo yanaendelea na India na EU. Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi pana za kushughulikia kile Trump anachokiita vitendo vya kibiashara visivyo vya haki vinavyodhuru biashara za Marekani. (Chanzo: The Guardian)

Maoni:

Maendeleo ya hivi majuzi ya biashara kati ya Indonesia na Marekani—yamesifiwa na serikali ya Indonesia kama mafanikio ya kidiplomasia kutokana na kupunguzwa kwa ushuru wa Marekani kutoka 32% hadi 19%—kwa hakika yanasisitiza udhaifu mkubwa wa kimuundo katika diplomasia ya kimataifa ya Indonesia. Hili linaloitwa "mafanikio" limefunikwa na ukweli kwamba Marekani ilipata makubaliano makubwa: ufikiaji kamili wa soko la Indonesia bila ushuru, ununuzi wa kulazimishwa wa ndege 50 za Boeing, na mabilioni ya dolari katika nishati na bidhaa za kilimo za Marekani. Kimsingi, Indonesia haishiriki katika mazungumzo yenye mizani sawa, na huru lakini inashinikizwa kuafiki.

Nguvu hii sio mpya. Tangu uhuru wa Indonesia, Marekani imekuwa na mchango mkubwa katika kuunda mwelekeo wa kisiasa na kiuchumi wa nchi hiyo. Kupitia mbinu kama vile deni la nje na utegemezi wa wafadhili, Marekani ilijikita katika michakato ya utungaji sera ya Indonesia, na kuathiri kila kitu kuanzia ukombozi wa kiuchumi hadi utawala wa kisiasa. Utajiri wa asili wa Indonesia—mafuta yake, gesi, shaba na dhahabu—umetolewa na kusafirishwa kwa muda mrefu chini ya mikataba ambayo inapendelea mashirika ya kigeni, hasa yale yanayohusishwa na maslahi ya Marekani.

Kinachovunja moyo hasa ni sauti ya sherehe kutoka kwa maafisa wa Indonesia kujibu kile ambacho kimsingi ni ushurutishaji wa kiuchumi. Badala ya kupinga umbile lislo na usawa la makubaliano hayo au kudai haki ya Indonesia kulinda viwanda vyake vya kitaifa na ubwana wake wa kiuchumi, serikali imechagua kukumbatia hadharani mkataba huo kama ushindi. Hii inaakisi mwelekeo mpana zaidi miongoni mwa nchi zenye Waislamu wengi, ambapo utegemezi wa baada ya ukoloni na kukosekana kwa uhuru wa kweli wa kisiasa kunaendelea kuzuia juhudi za kuendeleza uchumi imara na unaojitosheleza.

Kwa upana zaidi, kipindi hiki kinaonyesha hatari ya kijiografia ya ulimwengu wa Kiislamu. Licha ya rasilimali zake nyingi za asili na za kibinadamu, ulimwengu wa Kiislamu bado umegawanyika, dhaifu, na hauwezi kujishindilia kwenye jukwaa la kimataifa. Udhaifu huu sio tu wa kiuchumi, bali pia wa kisiasa na kifikra. Inaelezea kutoweza kudumu kwa mataifa yenye Waislamu wengi kulinda watu wao, achilia mbali kutoa mshikamano wa maana kwa ndugu zao wanaokandamizwa kama Wapalestina.

Hadi jamii za Kiislamu zitakapounda mifumo ya kisiasa inayotanguliza ubwana, umoja na kujitegemea badala ya kujisalimisha kwa dola za kigeni na taasisi za kiliberali mamboleo, zitaendelea kuwa vyombo tu mikononi mwa dola za kilimwengu. Uhuru wa kweli unahitaji zaidi ya kupunguza ushuru—unahitaji ujasiri wa kusimama kidete dhidi ya unyonyaji wa kiuchumi na kujenga utaratibu unaohudumia watu, sio maslahi ya nje.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdullah Aswar

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu