- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Idhini ya Marekani sio Kipimo cha Uamuzi wa Kisiasa kwa Umma wa Kiislamu
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mnamo tarehe 17 Julai 2025, Dawn News ilinukuu kutoka Reuters, "Ikulu ya White House mnamo Alhamisi ilisema kwamba hakuna ziara ya Rais wa Marekani Donald Trump iliyopangwa Pakistan "kwa wakati huu" baada ya kuenea kwa taarifa za safari hiyo. Mapema siku hiyo, baadhi ya vituo vya habari vya televisheni vya ndani viliripoti, vikinukuu vyanzo, kwamba Trump alitarajiwa kuzuru Pakistan mwezi Septemba. Chaneli za habari zilisema kwamba Trump pia angetembelea India baada ya kuwasili jijini Islamabad mwezi Septemba. Chaneli hizo baadaye ziliondoa ripoti zao.” [Dawn]
Maoni:
Taasisi ya jeshi la Pakistan inaamini kwamba tawala za Republican nchini Marekani kwa jumla zina huruma na ni rafiki kwa Pakistan, kinyume na tawala za Kidemokrasia ambazo zinatabanni sera ya hasimu. Rais Biden, kwa mfano, hakukutana na kiongozi yeyote wa Pakistan. Wala hakupiga simu kwa Waziri Mkuu yeyote wa Pakistan Imran Khan au Shahbaz Sharif, wakati wa Urais wake wa miaka minne. Hii ilichukuliwa kama dharau nchini Pakistan.
Mkuu wa jeshi la Pakistan, Asim Munir, na makamanda wengine wa kijeshi wanaamini kuwa kuregea kwa Trump katika Ikulu ya White House kumefungua fursa kwa Pakistan kuregesha uhusiano wake na Marekani, ambao ulisitishwa vilivyo wakati wa utawala wa Rais Biden, ambaye alikuwa ametoa usimamizi wa uhusiano na Pakistan kwa Pentagon. Katika muktadha huo, Asim Munir, amebuni mkakati wa kumtuliza na kumfurahisha Trump, kwani sasa inajulikana sana miongoni mwa viongozi wa kitaifa na marais wa nchi kwamba Trump anapenda viongozi wanaomsifu, kujisalimisha kwa matakwa yake na kumsaidia kupata nia njema kwa kambi yake ya wapiga kura.
Ili kujipendekeza kwa Trump, Asim Munir alikubali ombi la Trump la kumkamata na kumkabidhi anayedaiwa kuwa ndiye mpangaji mkuu wa shambulizi la Agosti 2021 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kabul ambalo liliua wanajeshi kumi na tatu wa Marekani. Akifahamu hamu ya kibiashara ya Trump katika sarafu ya crypto, Pakistan ilitangaza kuundwa kwa Baraza la Crypto la Pakistan, na mkuu wa PCC, Bilal bin Saqib alitembelea Ikulu ya White House na kufanya mkutano wa kina na Bo Hines, Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Rais Trump juu ya Mali za Kidijitali. Hii ilifuatiwa na ziara ya Asim Munir katika Ikulu ya White House na mkutano wake na Trump ambapo aliahidi uungaji mkono wa Pakistan kwa mpango wa Marekani wa kujenga Mashariki ya Kati mpya.
Majenerali wa Pakistan pia wanafahamu hamu ya Amerika katika madini adimu ya ardhini na wanakaribisha uwekezaji wa Marekani katika sekta ya madini ya Pakistan. Pakistan pia ilitangaza haraka nia yake ya kujadili suluhisho na utawala wa Trump na kufikia makubaliano ya kibiashara baada ya Trump kutangaza Ushuru wa 29% kwa Pakistan. Na Pakistan ilimpendekeza rasmi Trump kwa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa "utawala wake wa hali ya juu", tangazo ambalo lilisababisha hasira kubwa dhidi ya watawala wa Pakistan. Na sasa watawala wa Pakistan wanatumai ziara ya Trump nchini Pakistan na wanachukulia hii kuwa mafanikio makubwa na heshima kwao wenyewe.
Hakika ni usaliti mkubwa na jambo la aibu na udhalilifu kwamba watawala wa kijeshi wa Pakistan wanakimbilia kuitumikia Amerika na Rais wake Trump, kwa matumaini ya kupata nia njema ya Amerika. Sera hii ya kujipendekeza kwa Amerika ya watawala wa Pakistan inasimama kinyume kabisa na rai jumla nchini Pakistan. Waislamu wa Pakistan wanamchukia Trump na wanamchukulia yeye na mtangulizi wake Biden kama wauaji wa Gaza. Ilikuja kama mshtuko kwa Waislamu wa Pakistan walipomwona mkuu wao wa jeshi akila chakula cha mchana na Rais wa Marekani, wakati Rais wa Marekani alikuwa akisimamia na kuunga mkono shambulizi la umbile haramu la Kiyahudi dhidi ya Iran.
Tofauti hii kati ya watawala wa Pakistan wanaokimbilia kutumikia maslahi ya Marekani na Waislamu nchini Pakistan, wanaotaka kupigana na Marekani na washirika wake India na umbile haramu la Kiyahudi ni wazi kwa kila mtu kuona. Pakistan iko tayari kwa mapinduzi. Waislamu nchini Pakistan, sawa na Waislamu kila mahali, walishangazwa na mauaji ya Waislamu mjini Gaza na wanawalaumu watawala wa Waislamu kwa kushindwa kuyakusanya majeshi ya Kiislamu ili kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na kuwasaidia ndugu zao Waislamu.
Kuna hamu kubwa nchini Pakistan ya kuwaondoa watawala ambao ni vibaraka wa Amerika. Mapinduzi ya Syria na Bangladesh yamewapa Waislamu nchini Pakistan matumaini kwamba wao pia wanaweza kuwaondoa watawala wao. Kiungo pekee kinachokosekana kwa mapinduzi nchini Pakistan dhidi ya watawala wanaotii Amerika ni uamuzi wa vikosi vya jeshi vyenye nguvu vya Pakistan kuchukua hatua madhubuti kuunga mkono rai jumla ya umma nchini Pakistan na kukumbatia uongozi mpya na ruwaza mapya kwa Pakistan, iliyo huru na utumwa wa Marekani na utiifu kwa Mfumo wa Ulimwengu wa Marekani. Ushindi wa hivi majuzi wa Pakistan dhidi ya India umewapa wanajeshi wa Pakistan imani katika uwezo wao wenyewe. Nguvu ya majeshi ya Pakistan inatosha kwa ajili ya kujenga Mashariki ya Kati mpya yenye msingi wa umoja wa ardhi zote za Waislamu chini ya Khilafah Rashida ya Pili. Ni ruwaza hii ambayo kwayo tunawalingania Waislamu wote kuifanyia kazi. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱسْتَجِيبُوا۟ لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal:24].
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yahya Malik – Wilayah Pakistan