Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
| H. 3 Jumada II 1447 | Na: HTY- 1447 / 10 |
| M. Jumatatu, 24 Novemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mahouthi Wawakamata Mashababu wa Hizb ut Tahrir kwa Kufichua Mkataba wa Trump!
(Imetafsiriwa)
Mnamo Ijumaa, 21/11/2025, kundi la Mahouthi katika Jimbo la Ibb liliwakamata wanachama wawili wa Hizb ut Tahrir, ndugu: Osama Muhammad Mas’ad Al-Wurafi (umri wa miaka 19) na Ibrahim Muhammad Mas’ad Al-Wurafi (umri wa miaka 15) kufuatia usambazaji wao wa toleo lililotolewa na Hizb ut Tahrir lenye kichwa: “Trump Anawaongoza Wafuasi Wake miongoni mwa Watawala katika Ardhi za Waislamu Kwenye Mkataba wa Fedheha na Aibu, Wakiinamisha Vichwa Vyao Nyuma Yake kwa Kuiweka Gaza Hashem chini ya Usimamizi na Ukoloni!” Toleo hili lilisambazwa nchini Yemen na nchi nyingi za Waislamu.
Toleo hilo lililosambazwa na Mashababu wa Hizb ut Tahrir linafichua mkataba wa mhalifu Trump na linafichua watawala wasaliti wanaohusika nao. Miongoni mwa yaliyosemwa ndani yake: “Azimio hili la Baraza la Usalama halikuzaliwa kutokana na wakati huu bali lilibuniwa na Trump kwa idhini ya wafuasi wake kutoka kwa watawala katika ardhi za Waislamu tangu mkutano wa Umoja wa Mataifa mnamo Septemba 2025, ambapo Trump aliongoza mkutano uliojumuisha Saudi Arabia, Imarati, Qatar, Misri, Jordan, Uturuki, Indonesia na Pakistan, kando ya mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Jumanne, 23/9/2025, akiusifu kama mkutano muhimu zaidi, kisha akawasilisha—au akalazimisha—juu yao mpango wa nukta 20, na nukta hizo ishirini za mpango wake zilizungumzia kupotea kwa Gaza na usimamizi na ukoloni wake, na kuifanya Gaza kuwa bustani linalofurahiwa na Trump na washirika wake Mayahudi!”
Ukamata wa Mahouthi wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir unathibitisha madai yao ya uongo na udanganyifu kuhusu kusimama na Gaza. Kiuhalisia, wao ni gora moja na watawala wasaliti waliotajwa kwenye toleo hilo kama vile Bin Salman (MBS) na Bin Zayed—ingewezaje kuwa kinyume wakati wanawatetea na kuwakamata wale wanaowafichua na kuwafichua mabwana zao wa Marekani mbele ya Ummah? Kitendo hiki kinawavua Mahouthi na kuangusha pazia ambayo kila mara walijaribu kujificha nyuma—wakidai kusimama na Gaza Hashem—ijapokuwa msimamo wao si kitu chengine ila ni kauli mbiu wanazotumia kuwadanganya watu! Lakini ni jambo la ajabu kweli—kwani mzunguko huo utawageukia kama vile ulivyowageukia wale waliowatangulia, iwe Ali Saleh aliyeangamia nchini Yemen au watawala wengine wahalifu katika nchi za Waislamu. Inashangaza sana! Mahouthi wananyanyua kauli mbiu “Kifo kwa Amerika” huku wakiwakamata wanachama wa Hizb ut Tahrir wanaofanya kazi mchana na usiku kuing'oa Amerika na mfumo wake wa kibepari!!
Ujumbe wetu kwa wanachama wanyoofu wa taasisi ya usalama katika nchi ya Al-Ansar—Yemen ya imani na hekima—ni kwamba Hizb ut Tahrir ina mizizi iliyojikita ndani ya mwili wa Ummah wa Kiislamu, na da'wah yake ya dhati inasafiri katika upeo wa dunia.
Hizb inajulikana kwa wote kama chama cha kisiasa ambacho lengo lake ni kurudisha maisha kamili ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na haitumii vitendo vya kisilaha kufikia lengo lake, si kwa hofu au uoga, bali kwa kujitolea kwa njia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika kusimamisha Dola. Utapata katika misingi ya Hizb iliyochapishwa kwenye tovuti maelezo wazi na jibu la kutosha linalothibitisha ukweli wake—kwamba ni kiongozi asiyewadanganya watu wake.
Tunathibitisha kwamba Mashababu wa Hizb ut Tahrir hawaogopi vitendo hivyo vya ukandamizaji, iwe ni Yemen au nchi zengine za Kiislamu ambapo wanakabiliwa na kukamatwa mikononi mwa tawala za huko. Vitendo hivi havijawazuia kuendelea na da’wah yao, na hizb haitasita katika njia yake, kufuata nyayo za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ili kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, hivi karibuni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ * يَوْمَ لَا يَنفَعُ الظَّالِمِينَ مَعْذِرَتُهُمْ وَلَهُمُ اللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوءُ الدَّارِ]
“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi, * Siku ambayo hautawafaa madhaalimu udhuru wao, nao watapata laana, na watapata makaazi mabaya kabisa.” [Ghafir: 51–2].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: 735417068 https://www.hizb-uttahrir.info |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |



