Jumamosi, 11 Jumada al-awwal 1447 | 2025/11/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uholanzi

H.  6 Jumada I 1447 Na: 05 / 1447
M.  Jumanne, 28 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kupiga Kura Ndani ya Mfumo wa Kisekula Kunapelekea Kuoanishwa

(Imetafsiriwa)

Mara nyingi zaidi, maimamu, mabaraza, na viongozi wa kidini huwataka Waislamu nchini Uholanzi kupiga kura kwa wingi na kushiriki katika mchezo wa kisiasa wa mfumo wa kisekula. Mfumo ambao, kutoka asili na kiini chake, unapinga Uislamu, unautenga, na kujaribu kuudogosha hadi kitu kilichofungwa kwenye msikiti au sebule.

Usekula si mfumo usioegemea upande wowote bali ni fikra ambayo imelazimishwa kwa nguvu kwa Waislamu duniani kote. Hali mbaya ambayo Ummah unajikuta ndani yake inatokana sana na misingi hii ya kisekula ambayo ardhi za Waislamu zilijengwa juu yake. Miundo hii imesababisha mporomoko, udhalilifu, na kutengwa na Uislamu. Gaza ni mfano mchungu zaidi wa hili: Waislamu bilioni mbili wanaangalia huku serikali zikibaki tiifu kwa ajenda za Magharibi, maslahi yao wenyewe, na ulinzi wa msingi wa kisekula.

Ukweli kwamba hata mabaraza ya fiqh na fatwa katika baadhi ya matukio yametoa “ruhusa” ya kushiriki ni jambo linaloonekana, kwani kwa kitu ambacho ni halali waziwazi, hakuna fatwa inayohitajika. Hii ni kwa sababu uamuzi huu kimsingi ni haramu; kupotoka ndio ruhusa. Kwa hivyo si uaminifu kuwasilisha upotovu huo kama uhalali kamili, bila kutafakari kwa kina au kutambua kwamba makosa yanaweza kufanywa. Kuinua kitu ambacho hapo awali kilikuwa haramu kabisa hadi halali ni hatua hatari sana.

Lakini baadhi ya maimamu huwasilisha ushiriki katika mfumo wa kisekula kupitia kupiga kura kama halali, bila kuweka alama yoyote ya kukosoa. Hili linapotosha. Pia linawasilishwa kama kitu kinachoendelea na kinachodhaniwa kuwa kwa maslahi ya jamii ya Waislamu nchini Uholanzi. Kinyume chake ni kweli. Kushiriki katika mfumo huu bila shaka husababisha kuoanishwa na kupoteza utambulisho. Kwa kushiriki, mwelekeo hubadilika kutoka utiifu kwa sheria ya Uislamu hadi vitendo vya kimantiki na ulegezaji misimamo. Waislamu wanashikilia chanzo kile kile kilichosababisha kuanguka kwa hadhara ya Kiislamu: usekula. Mtu anawezaje kutarajia kwamba ushiriki katika msingi huu utawahi kusababisha heshima au maendeleo?

Makubaliano yanayofanywa si ishara za maendeleo bali ni ya kujisalimisha. Waislamu wanapoweka maono yao kwenye masuluhisho ya muda mfupi ndani ya mfumo wa kisekula, wanajiweka kwenye maudhui ya jamii yenye makombo. Tatizo halisi ni kutokuwepo kwa lengo kubwa zaidi. Hakuna maono ya kuchukua kubadilisha usekula unaokamatwa na ulimwengu wa Kiislamu kwa Uislamu. Maadamu hili halipo, mtu anabaki amekwama katika vitendo vya kimantiki na marekebisho ya juu juu ambayo hayaleti mabadiliko ya kweli.

Hii ndiyo sababu wito wa kupiga kura ni tatizo kubwa. Unawaongoza Waislamu kupunguza matarajio yao hadi maslahi ya muda mfupi, huku dhamira yao ya kweli ikiwa kubwa zaidi. Ni kuhusu kuregesha Uislamu kwa ukamilifu wake na kufanya kazi kuelekea kuregea kwa mfumo wa Kiislamu utakaoinua Ummah na kuregesha nafasi yake duniani.

Yeyote anayepoteza mtazamo wa lengo hili kubwa na kushikilia lengo la muda mfupi bila shaka atazama katika kufuata na kuona kitambulisho chake kikimomonyoka. Ingawa dhamira ya kweli ya Waislamu inapaswa kuwa kubadilisha usekula kwa Uislamu, sio kujiingiza katika usekula.

Tunasema haya sio kutokana na uadui bali kama ushauri wa dhati. Kwa sababu tunawajali Waislamu na tunajali mustakabali wa vizazi vijavyo. Lazima pia iulizwe kwa dhati: je, mabaraza ya fatwa na wasomi waliotoa ruhusa wamewahi kuzungumza kwa nguvu dhidi ya usekula, na je, wamejitolea hadharani kuubadilisha na Uislamu? Maadamu hili halipo, uamuzi wao unabaki kuwa wa upande mmoja na wenye matatizo.

Umuhimu wa kweli haupo katika utambuzi ndani ya usekula, bali katika kushikamana kwa dhati na kanuni za Uislamu na kufanya kazi kwa ajili ya ukombozi wa Ummah kutoka kwa mfumo huu uliolazimishwa, kwa kuubadilisha na mfumo wa Uislamu. Ni wale tu wanaokubali lengo hili kubwa zaidi ndio wanaofanya kazi kwa ajili ya mustakabali na kuinuliwa kwa Waislamu.

Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Uholanzi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uholanzi
Address & Website
Tel:  0031 (0) 611860521
www.hizb-ut-tahrir.nl
Fax:  0031 (0) 611860521
E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu