Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 21 Rabi' I 1447 | Na: HTS 1447 / 32 |
M. Jumamosi, 13 Septemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Sudan Wilayah – Mji wa Kosti, Jimbo la White Nile Wakutana na Dkt. Muhammad al-Haitham, Katibu Mkuu wa chama cha National Unionist Party katika Jimbo la White Nile
(Imetafsiriwa)
Mnamo Ijumaa, 12 Septemba 2025, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan ulimtembelea Dkt. Muhammad al-Haitham, Katibu Mkuu wa chama cha National Unionist Party, katika Uwanja wa Azraq Taiba huko Kosti.
Ujumbe huo uliongozwa na Dkt. Ahmed Fadl al-Sayyid, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, na akifuatana na Ustadh Abdul Majeed Osman (Abu Hajar) na Ustadh Muhammad Babiker, wote wanachama wa Hizb ut Tahrir.
Baada ya kujitambulisha, kiongozi wa ujumbe alieleza kuwa ziara hii inajiri ndani ya muundo wa kampeni iliyoanzishwa na Hizb ut Tahrir/Sudan Wilayah ya kuzuia kujitenga kwa Darfur, akibainisha hatari ya mpango huo kwa umoja wa nchi kwa kuzingatia kuwa suala la umoja wa dola na umoja wa Umma ni suala nyeti na kwamba ni lazima hatua zichukuliwe kuhusiana na suala hilo katika hali ya uhai au kifo.
Pia alitaja kampeni ya awali hizb iliyoifanya ili kukwamisha mpango wa kuitenga Sudan Kusini, akiashiria maafa na masaibu yaliyoikumba Sudan kutokana na kujitenga kwa eneo la kusini, na jinsi Marekani ilivyofanikiwa kufanya hivyo, na sasa inataka kutenganisha Darfur.
Kisha amiri wa wajumbe, akambebesha Dkt. Muhammad al-Haitham, jukumu akimwambia kwamba kuna wanaume nyuma yenu ambao lazima muwajulishe kuhusu mpango huu wa uhalifu unaotekelezwa na Marekani. Daktari huyo alikubaliana na kauli ya ujumbe huo, akithibitisha kuunga mkono umoja wa Umma, ambao ndio kadhia yake nyeti. Alisema, “Tunakubaliana na mradi wa Hizb ut Tahrir wa kukwamisha mpango wa makafiri wa Magharibi wa kutenganisha Darfur.” Aliongeza, “Hapana budi Hizb iendelee na njia yake hiyo, na lazima tushikane mikono ili kufelisha mpango huu mchafu wa kutenganisha Darfur kutoka Sudan.”
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Wilayah Sudan
https://www.hizb-uttahrir.info/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/sudan/4957.html#sigProId6891a1158a
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |