Jumatatu, 11 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  29 Jumada I 1447 Na: BN/S 1447 / 08
M.  Alhamisi, 20 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Gaza Inavuna Mavuno Uchungu ya Baraza la Usalama na Uamuzi wa Baraza la Amani
(Imetafsiriwa)

Siku chache baada ya uamuzi wa Baraza la Usalama, watu wa Gaza walianza kuvuna hasara yake; katika muda usiozidi masaa 24, mashahidi 34—wengi wao wakiwa watoto na wanawake—walikuwa wamepanda daraja hiyo hadi kufikia Alhamisi asubuhi, 20/11/2025, pamoja na makumi ya waliojeruhiwa kutokana na uzito wa njaa na kwenye makucha ya baridi kali. Damu hizi safi zilikuwa maana halisi ya uamuzi ulioipa Amerika usimamizi na mamlaka juu ya Ukanda wa Gaza, ikiruhusu kukata vichwa kama ilivyotaka. Ni uamuzi uliopuuza damu, utajiri, na ardhi za watu wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi na kuachilia mkono wa Mayahudi kutumbukia ndani ya damu yetu, ambayo ilienea zaidi ya Gaza hadi Kambi ya Ain al-Hilweh nchini Lebanon. Hata rais mhalifu wa umbile la Kiyahudi anakanyaga ardhi ya al-Sham kana kwamba ni ardhi yake mwenyewe, kana kwamba watawala nchini Uturuki, Pakistan, Indonesia, Saudi Arabia, Qatar, Misri, Jordan, na Imarati—kwa kauli yao ya pamoja ambayo waliunga mkono uamuzi wa Baraza la Usalama kabla haujatolewa—waliwaachilia Mayahudi kufanya chochote walichotaka katika nchi zote, wakampa Trump Gaza, na kuwatoa watu wake kama kafara kwenye kizingiti cha Jumba Jeusi.

Umma ulikuwa ukikasirika ulipoona damu ikitiririka Gaza, huku watu wake wakiwa wamekufa njaa na kunyongwa na kuzingirwa. Kuhusu watawala wahalifu, ndimi zao zinalaani, huku mikono yao ikiwa mikononi mwa umbile hilo halifu katika uvamizi wake dhidi ya Gaza, wakijificha nyuma ya kulaani, shutma, na pingamizi. Lakini mzingiro huo unawafichua, usaliti unawapomoa barakoa zao usoni, na kulipa umbile hilo silaha na vifaa kunawalaani.

Watawala wamefichua nyuso zao zilizopakwa rangi ya usaliti na kutangaza uadui wao kwa Uislamu na Waislamu kwa kuwawezesha Amerika na Mayahudi kumiliki silaha za mujahidina wa Gaza na damu ya watu wake, na kwa kuwakabidhi kwa usimamizi wa Marekani. Je, inaruhusiwa baada ya uhalifu huu wote kukaa kimya?!

Je, kimya si aina ya kuidhinisha uhalifu wao?! Harakati za Ummah na wanajeshi wake ni faradhi kabla ya mauaji kuenea Gaza, kwa kweli, ilikuwa faradhi siku ambayo Waingereza walitia miguu yao michafu katika Ardhi hii Iliyobarikiwa zaidi ya karne moja iliyopita. Kila tone la damu lililomwagika Palestina lilitokana na kuchelewa kwa Ummah na wanajeshi wake kusonga kuelekea huko. Na kila siku ambayo Ummah na wanajeshi wake hawasongi hutafsiriwa kuwa damu, njaa, na ukandamizaji kwa watu wa Palestina.

Sasa kwa kuwa jambo hilo limefikia kikomo cha kufurika na watawala wameiuza Gaza, watu wake, Palestina yote, na matukufu yake wakiuza makubaliano basi hasira ya Ummah lazima iongezeke maradufu hadi iwe kama volkano inayojaza vifua na kisha kulipuka, ikichoma njama zote, ikiyeyusha maamuzi na ulinzi wote, na kuviondoa viti vya enzi vya serikali ambazo uadui wao kwa watu wa Palestina na waumini unadhihirika, hasira ambayo haizimiki isipokuwa kwa swala ya ukombozi katika Masjid al-Aqsa na kumsujudia Mwenyezi Mungu kwa shukrani kwamba Masjid al-Aqsa imerudi kama ilivyokuwa hapo awali, ikiwa imefunikwa na Uislamu na wanajeshi wake.

Hadi siku hiyo ifike, dhambi ya kuitelekeza na dhambi ya watawala haitaondolewa kwa yeyote isipokuwa kila mtu mwenye ikhlasi anayefanya kazi ya kuhamasisha Ummah na askari wake; kwa ajili ya damu safi, roho zenye hofu zinaogopa kunyakuliwa, na Masjid al-Aqsa—mahali pa safari ya usiku ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), wote hao wanasimama mbele ya Mwenyezi Mungu wakitoa hoja dhidi ya Ummah hadi watakapochukua haki zao kamili bila kupungua.

[أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنْظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ دَمَّرَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ وَلِلْكَافِرِينَ أَمْثَالُهَا * ذَلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ مَوْلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَأَنَّ الْكَافِرِينَ لَا مَوْلَى لَهُمْ]

“Kwani hawakutembea katika ardhi wakaona ulikuwaje mwisho wa walio kuwa kabla yao? Mwenyezi Mungu aliwaangamiza, na kwa makafiri hawa itakuwa mfano wa hayo. * Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Na makafiri hawana mlinzi.” [Surah Muhammad:10–11].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 0598819100
www.pal-tahrir.info
E-Mail: info@pal-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu