Hali Baada ya Mvua na Mafuriko kwa Mara Nyingine Tena Imeweka Wazi Kuwa Waislamu Wanahitaji Mchungaji Khalifah
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Tangu Juni 26, mafuriko katika maeneo mbalimbali ya Khyber Pakhtunkhwa, Punjab, na Karachi yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 650 na kujeruhi zaidi ya elfu moja. Maelfu ya nyumba zimesombwa na maji, pamoja na akiba za maisha yote za watu, mali za nyumbani, na magari. Dada na mabinti zetu—ishara za staha na heshima—wamenyimwa nyumba na faragha zao, wakilazimishwa kuishi chini ya anga wazi.



