Jumapili, 02 Safar 1447 | 2025/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Pongezi kwa Mnasaba wa Idd Al-Adha Iliyobarikiwa Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Illallah, Allahu Akbar, Allahu Akbar wa lillahi Al-Hamd

Maumivu yetu yanazidi tunaposhuhudia jinai hii kwa macho yetu wenyewe, huku majeshi ya Umma wa Kiislamu yakibaki bila kuchukua hatua yoyote, yakiwa hayana mwelekeo wa kuwasaidia ndugu zao wanaodhulumiwa. Vilio vya wafiwa na machozi ya watoto haviwasumbui, na majeshi haya bado hayajibu kwa sauti ya juu kabisa “Labbaik Allahumma Labbaik” katika kuitikia mwito wa Mola wao wa jihad na kuwanusuru Waislamu wanaodhulumiwa. Je, udhaifu na udhalilifu umefikia kiwango hiki?

Soma zaidi...

Kesi ya Kisiasa Inafichua Uungaji Mkono wa Denmark kwa Uvamizi wa Mauaji ya Halaiki

Serikali ya Denmark inaendelea na uungaji mkono wake wa dhati kwa uvamizi wa Kizayuni wa Palestina na mauaji ya halaiki yanayoendelea huko Gaza, ambayo yameitia hofu kila nafsi adhimu katika sayari hii, na kuwaamsha watu kuona kwamba vima vinavyodaiwa vya dola za Magharibi vimezikwa na maiti hizo za maelfu ya wanawake na watoto chini ya magofu ya Gaza. Haki za binadamu, haki ya kuishi na kujiamulia, haki za wanawake na ustawi wa mtoto - yote haya yanatupwa chini ya tingatinga la Uzayuni na wanasiasa na mamlaka, ambao kwa hivyo wanaonyesha unafiki wao wa hali ya juu na kufichua jinsi gani "vima" hivi kivitendo ni ala tu za kisiasa.

Soma zaidi...

Mbweha ni Mbwa Mwitu Anayetuma Maua… Mbweha Ana Hila Nyingi…

Aliyekuwa balozi wa Marekani katika umbile la Kiyahudi, Martin Indyk, mnamo Alhamisi tarehe 20 Juni aliamua kuondoa mwaliko kwa Waziri Mkuu wa Kiyahudi Benjamin Netanyahu kutoa hotuba mbele ya Bunge la Congress. Hii ni ili aombe radhi kwa kuutuhumu utawala wa Rais Joe Biden kwa kuinyima silaha “Israel,” huku vyombo vya habari vya Kiyahudi vikisema kuwa Netanyahu anapendelea makabiliano ya hadharani na Washington.

Soma zaidi...

Tanzania na Janga la Utegemezi

Jumapili ya tarehe 02 Juni, Juni 2024, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Korea Kusini zilitia saini mikataba ya makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili jijini Seoul. Mikataba hiyo ilijumuisha mkopo wa dolari bilioni 2.5 (Tsh trilioni 6.5) uliotolewa na Korea Kusini chini ya Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Korea Kusini (EDCF) kwa ajili ya miradi mbalimbali ya miundombinu.

Soma zaidi...

Kuwekwa Kizuizini kwa Sababu ya Majadiliano Tu ya Hadhara kuhusu Kanuni za Shariah ya Kiislamu katika Demokrasia Kubwa Zaidi Duniani

Mamlaka za polisi kutoka jimbo la Tamil Nadu nchini India zimeripoti kuzuiliwa kwa Waislamu sita kwa kufanya amali za Hizb ut Tahrir (HT). Watu hao waliokamatwa ni pamoja na Dkt Hameed Hussain, ambaye ana shahada ya uzamifu ya Uhandisi Mitambo, Baba yake Hussain Ahmed Mansoor na kaka yake Abdul Rehman ambaye ni Msomi wa Kiislamu na wengine watatu, Mohammed Maurice, Khader Nawaz Sherif na Ahmed Ali.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu