Jumatatu, 02 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/08/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina inamuomboleza mmoja wa wanaume wa Hizb kutoka kizazi cha kwanza ambaye alifanya kazi katika safu zake tangu miaka ya 1950, marehemu mbeba da’wah, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Ustadh Muhammad Abdullah Amr (Abu Abdullah)

Soma zaidi...

Uhakiki wa Habari 17/05/2023

Vita vya baada ya 9/11 vya Marekani vimesababisha vifo vya zaidi ya milioni 4.5, kwa mujibu wa ripoti kuu mpya kutoka kwa Mradi wa Gharama za Vita katika Chuo Kikuu cha Brown. Takriban vifo milioni 1 kati ya hivyo vilitokana na mapigano ya moja kwa moja katika maeneo ya vita kote Afghanistan, Pakistan, Iraq, Libya, Syria, Somalia, na Yemen, huku milioni 3.5 vilivyobaki ni "vifo visivyo vya moja kwa moja" vilivyotokana na mizozo ya "kuharibiwa kwa uchumi, huduma za umma, na mazingira,” kulingana na ripoti hiyo.

Soma zaidi...

Sakata ya Imran Khan

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan alikamatwa kwa kasi na maafisa wa kutuliza ghasia alipokuwa mahakamani kujibu mashtaka ya ufisadi na uchochezi. Wafuasi wa Khan waliingia mabarabarani, wakiteketeza magari, kushambulia kambi za jeshi pamoja na nyumba za baadhi ya makamanda.

Soma zaidi...

Huwezi Kupeana Usichokuwa Nacho

Mnamo Jumanne na Jumatano, Mei 9 na 10, 2023, Baghdad ilikuwa mwenyeji wa kongamano lake la kwanza wa kimataifa kuhusu udhibiti wa dawa za kulevya, katika uwepo wa wawakilishi wa nchi nane: Saudi Arabia, Misri, Lebanon, Jordan, Kuwait, Syria, Iran, Uturuki na mabaraza na afisi za Kiarabu na kimataifa. Kama kawaida, mkutano haukutoa suluhisho lolote kwa sababu walitafuta mbali na sababu za jambo hili na kuenea kwake kwa njia ya kutisha.

Soma zaidi...

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: Risala za Dharura kuhusu Uhalifu na Ukiukaji wa Hay'at Tahrir Ash-Sham!

Risala zilizotolewa na kundi la wabebaji Da’wah zilizoelekezwa kwa Hay’at Tahrir Ash-Sham (HTS) baada ya kuvamia nyumba za wabebaji Dawah na kuwakamata mashababu kadhaa wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria kwa njia ya kishenzi, ukiukaji utukufu, katika mandhari ya kutisha iliyo mbali na maadili ya Uislamu na Waislamu.

Soma zaidi...

Wanawake wa Kiislamu nchini Iraq walio katika Mgomo wa Njaa Hawana Msaidizi Chini ya Sheria za Kibepari za Kiliberali

Mnamo tarehe 6 Mei 2023, BBC iliripoti kuwa mamia ya wanawake wamegoma kula katika gereza moja la Iraq katika mji mkuu wa Baghdad. Wanapinga kuzuiliwa kwao kwa kuwa sehemu ya kundi la Dola ya Kiislamu, baada ya kile wanachosema kuwa ni kesi zisizo za haki. Kundi hilo linasemekana kujumuisha raia wa kigeni kutoka Urusi, Uturuki, Azerbaijan, Ukraine, Syria, Ufaransa, Ujerumani na Marekani. "Inafikiriwa kuwa takriban watoto 100 pia wanazuiliwa katika kituo hicho".

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu