Jumatatu, 02 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/08/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uhuru wa Kweli kwa Indonesia

(Imetafsiriwa)

Habari:

Sherehe ya miaka 80 ya Siku ya Uhuru wa Indonesia ilichangamshwa na mavazi ya kitamaduni ya kupendeza katika Kasri la Merdeka, Jakarta, Jumapili, Agosti 17, 2025. Waziri wa Afya Budi Gunadi Sadikin alihudhuria akiwa amevalia vazi la Batak, akisema alilichagua kwa sababu ya turathi ya mke wake. Waziri wa Nishati na Rasilimali za Madini Bahlil Lahadalia alivalia vazi la kitamaduni la Solo, akibainisha kuwa hapo awali alikuwa amevaa mavazi ya Papua, Sulawesi, na Maluku. Rais Prabowo Subianto alionekana akiwa amevalia Nusantara yenye rangi ya pembe za ndovu akiwa na peci nyeusi, songket sarong, yenye maua ya yasmini. Watu mashuhuri Raffi Ahmad na Nagita Slavina walivalia mavazi ya Kijava, huku Raffi akiwakumbusha wananchi kuchangia vyema kwa taifa. Mabalozi kutoka nchi marafiki walihudhuria wakiwa wamevalia suti rasmi, huku wananchi wengi pia wakiwa wamevalia mavazi ya kikanda, yakionyesha umoja katika utofauti katika sherehe hizo. (Chanzo: rri.co.id)

Maoni:

Tangu Tangazo la Agosti 17, 1945, Indonesia sasa imeingia mwaka wake wa 80 wa uhuru. Kwa kweli, kwa karibu karne moja ya uhuru, taifa hili lilipaswa kuwa limepata maendeleo makubwa, ufanisi, ustawi wa jamii, na haki. La kusikitisha, kilichotokea ni kinyume kabisa: Indonesia inaendelea kulemewa na matatizo mbalimbali kama vile umaskini, ukosefu wa usawa wa kijamii, kuzorota kwa maadili, udhibiti wa kigeni juu ya maliasili, madeni yanayoongezeka, ufisadi, na masuala mengine mengi.

Chanzo kikuu cha matatizo haya kinatokana na ukoloni wa kimfumo, yaani mfumo wa Ubepari, ambao msingi wake ni usekula. Kwa sababu ya kutawala kwa mfumo huu wa kisekula wa kibepari, matarajio ya wapiganiaji uhuru—kwamba Indonesia ingekombolewa kikamilifu kutoka kwa ushawishi wa kigeni—hayajatimizwa kabisa. Kwa kweli, urithi wa dola za kikoloni bado ungali unalikamata vikali taifa hili.

Kwanza, katika uwanja wa kanuni na sheria, mfumo wa sheria wa Indonesia unabaki kuwa wa kisekula. Ingawa wakoloni wa Uholanzi walifukuzwa, sehemu kubwa ya mfumo wao wa kisheria umehifadhiwa na kutekelezwa. Michakato ya kutunga sheria bado inaathiriwa na maslahi ya kigeni. Pili, katika uchumi, taifa hili linakabiliwa na deni kubwa, hasa mikopo ya nje ambayo mzigo wa riba umefikia maelfu ya trilioni za rupiah. Rasilimali zake za asili pia zinadhibitiwa kwa kiasi kikubwa na vyombo vya kigeni. Tatu, katika nyanja za kijamii na kitamaduni, athari haribifu zimekita mizizi kutokana na utitiri wa maadili ya kisekula. Hili limedhihirika katika matatizo ya kijamii kama vile uasherati, mikengeuko ya kijinsia ikijumuisha matendo ya LGBT, ponografia, ufisadi, kamari mtandaoni na aina mbalimbali za vurugu. Nne, katika siasa, Indonesia inaendelea kutekeleza mfumo wa kidemokrasia wa kisekula ambao unaathiriwa sana na ajenda za kigeni zinazokuzwa kupitia washirika wa ndani. Matokeo yake, sheria nyingi zinazopitishwa na Bunge na kanuni zinazotolewa na Serikali zinapendelea maslahi ya kigeni badala ya ustawi wa watu wa Indonesia.

Kwa mtazamo wa Kiislamu, uhuru wa kweli unamaanisha kukombolewa kutokana na utumwa kwa wanadamu wengine, na kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (swt), Muumba wa wanadamu na ulimwengu mzima. Kwa Waislamu, hivyo basi, uhuru si haki ya kulindwa tu, bali ni dhamira kuu ya ujumbe wenyewe wa Kiislamu.

Maadhimisho ya kila mwaka ya uhuru wa Indonesia hayapaswi kudunishwa kuwa tu hafla ya sherehe. Yanapaswa kutumika kama tafakari ya kimfumo kwamba Indonesia bado haijapata uhuru wa kweli. Taifa limesalia chini ya kutawaliwa na mfumo wa kisekula wa kibepari, ambao umezidisha matatizo yake na kuzidisha mateso ya watu wake.

Suluhisho liko katika kuikomboa Indonesia kutoka kwa mfumo huu wa kisekula wa kibepari. Hili linaweza kupatikana tu kwa kuregea katika sheria za Mwenyezi Mungu (swt) kupitia utabikishaji wa kina wa Sharia ya Kiislamu katika nyanja zote za maisha, chini ya mfumo wa Khilafah. Kusimamishwa kwa Khilafah kwa njia ya Utume kutaleta uhuru wa kweli kwa Umma wa Kiislamu—sio tu nchini Indonesia bali duniani kote.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdullah Aswar

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu