Ijumaa, 06 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/08/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  4 Rabi' I 1447 Na: H 1447/02
M.  Jumatano, 27 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Siku ya Katiba: Miaka Sitini ya Kufeli kwa Katiba ya Kisekula

(Imetafsiriwa)

Tarehe 27 Agosti 2025, ni kumbukumbu ya miaka kumi na tano ya kutangazwa kwa Sheria Kuu ya 2010. Katiba ya Kenya ya 2010 ilisifiwa kuwa ya mageuzi kwani ilileta mageuzi ya kimsingi ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi yaliyolenga kumaliza miongo kadhaa ya ukosefu wa utulivu chini ya katiba iliyopita.

Katika suala hili, tungependa kufafanua yafuatayo:

Tangu kutangazwa kwake, mizozo ya kikatiba ya Kenya imejikita zaidi kwenye mapungufu ya utekelezaji, mizozo ya uchaguzi, ugavi wa mamlaka, kanuni ya kijinsia na mchakato wa marekebisho. Kama ambavyo Dkt. Willy Mutunga, Jaji Mkuu wa kwanza wa Kenya mara kwa mara alisema kuwa Katiba ya Kenya 2010 ni waraka endelevu ambao ungechukua angalau miaka 20-30 kutekelezwa kikamilifu. Wazo kwamba katiba mpya itaweza kushughulikia matatizo ambayo katiba ya kikoloni ilishindwa kuyashughulikia, miaka 15 ni zaidi ya ushahidi tosha wa kufeli kwa katika ya kisekula, hadithi pekee yenye mafanikio ni kurefushwa kwa maisha duni na kuongezeka kwa viwango vya ufisadi, hali mbaya ya kiuchumi, mauaji yanayokiuka sheria na mengine mengi.

Katiba zilizotungwa na mwanadamu huchakachuliwa kwa urahisi na umbo la kisiasa kwa vile maslahi ya kisiasa yanapewa kipaumbele kuliko hata kanuni (sheria) na katiba.

Msingi wa Katiba mpya iliyopigiwa kura na Wakenya baada ya kura ya maoni ya 2010 ni ule ule wa katiba ya zamani ya kikoloni katika kumpa mwanadamu ubwana kamili wa kujitawala na kukataa hilo kwa Muumba wa Mwanadamu, Uhai na Ulimwengu kama chanzo pekee cha mwongozo na sheria. Uhalisia wa katiba zenye misingi ya kisekula hudhihirisha umbile dhaifu la mwanadamu katika kuamua mwongozo wa wanadamu kwani mara nyingi hukabiliwa na kuchakachuliwa na mabadiliko au hata kuandikwa kikamilifu kwa hati mpya. Hatimaye, historia imethibitisha mara kwa mara kwamba mwanadamu hawezi kuwa chanzo cha mwongozo.

Ili kutambua ukombozi wa kweli kutoka kwa dosari za katiba za Kidemokrasia ambazo kwazo mfumo muovu wa Ubepari unastawi. Kwa hakika, tunatoa wito kwa watu kutoka matabaka mbalimbali ya maisha wakiwemo wanafikra, wasomi na wanasiasa kufanya kazi katika kuweka muongozo wa kimungu ambao haukubali kurekebishwa na kuwindwa na uongozi wa ubinafsi. Hakika, Mwanadamu anahitaji mwongozo unaotoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Ukombozi huu ulifafanuliwa vyema na hotuba ya Rabiu bin Amri kwa Rustom Kamanda wa Dola ya Fursi: “Mwenyezi Mungu ametutuma ili tumtoe amtakaye kutoka katika ibada ya waja na kumwabudu Mola Mlezi wa waja, na kutoka katika ufinyo wa dunia hadi kwenye upana wake; na kutoka kwenye ukandamizaji wa mifumo hadi kwenye uadilifu wa Uislamu.”

Katiba ni waraka muhimu unaobainisha sura ya mfumo wa utawala na kutengeneza mkataba kati ya watawala na raia na vilevile kuwa kielelezo cha mfumo na maadili ya watu yanayoainisha nyanja zote za maisha. Uislamu kama mfumo mpana, unataka katiba ambayo imeegemezwa kwa uwazi juu ya sheria ya Mwenyezi Mungu. Katiba hii inaweza tu kutabikishwa kwa njia ya Khilafah, dola ambayo kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu itasimamishwa hivi karibuni katika moja ya nchi za Waislamu.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu