Ijumaa, 21 Safar 1447 | 2025/08/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Amerika

H.  18 Safar 1447 Na: 01 / 1447 H
M.  Jumanne, 12 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tanzia ya Anas Al-Sharif na Wenzake

(Imetafsiriwa)

Jioni ya Jumapili, 10 Agosti 2025, hema dogo la vyombo vya habari mbele ya Hospitali ya Al-Shifa Medical Complex katika Mji wa Gaza liliharibiwa kabisa na shambulizi la moja kwa moja kutoka kwa umbile la Kizayuni, na kuua waandishi wa habari watano waliokuwa wakinakili mauaji ya halaiki yanayoendelea huko Gaza. Miongoni mwa waliouawa shahidi walikuwa wanahabari Anas Al-Sharif, Mohammad Qreiqeh, na wapiga picha Ibrahim Zaher, Moamen Aliwa, na Mohammad Noufal. Mwenyezi Mungu (swt) awakubalie miongoni mwa Mitume, wakweli, mashahidi na watu wema – ni maswahaba wema walioje.

Watu wa Palestina na hususan Gaza wanaendelea kukabiliwa na uvamizi usiokoma kutoka kwa umbile la Kizayuni na dola za kimataifa zinazolilinda zikiongozwa na Marekani. Maisha yao, nyumba, hadhi, na maeneo matakatifu yote yamekiukwa bila kizuizi. Waandishi wa habari - ambao kazi yao ni kushuhudia na kufikisha ukatili huu kwa ulimwengu - wamekuwa wakilengwa kimpangilio. Kwa mujibu wa Al-Jazeera, takriban waandishi wa habari 270 na wafanyikazi wa vyombo vya habari wameuawa kimakusudi na umbile la Kizayuni, kwa kukaidi wazi wazi sheria ya kimataifa, maadili ya kimsingi, na hata kanuni za kimsingi za ubinadamu.

Ile inayoitwa jumuiya ya kimataifa inawajibika moja kwa moja kwa uhalifu huu. Kauli tupu za kulaani na nembo za ishara za huzuni haziziondolei uwajibikaji serikali zilizo na uwezo wa kuchukua hatua. Wakati mamia ya maelfu wameandamana katika miji kuanzia Sydney hadi Tokyo hadi London, serikali zao zimekataa kuchukua hatua za maana dhidi ya umbile la Kiyahudi. Wakati huo huo, nchi jirani za Kiislamu - ambazo majeshi yake yana uwezo wa kukomesha mauaji haya - zinasalia kimya.

Mauaji ya Gaza yanasimama kama ishara ya kutelekezwa - neno ambalo sasa halitoshi kuwasilisha kiwango cha usaliti. Shutuma za mara kwa mara zinazotolewa na Umoja wa Mataifa na miji mikuu ya dunia, kwa kweli, ni vitendo vya ushirikiano. Dola hizi zinaendelea kulipatia umbile la Kizayuni msaada wa moja kwa moja wa kijeshi, kisiasa na kiuchumi.

Umbile hili halitasitisha jinai zake wala halitawajibishwa isipokuwa kwa kusimamisha tena Dola ya Khilafah Rashida kama alivyobashiri Mtume Muhammad (saw): «ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha utakuwepo utawala wa kidhalimu utakaodumu kwa muda apendavyo Mwenyezi Mungu, kisha Mwenyezi Mungu atauondoa apendapo kuuondoa, kisha kutakuwa na Khilafah kwa njia ya Utume.” (Imepokewa na Ahmad)

Kusimamishwa kwa Khilafah Rashida ndio muundo pekee wa kisiasa na kijeshi wenye uwezo wa kuilinda Gaza na ardhi zote za Waislamu zinazodhulumiwa. Umma lazima udai kuondolewa kwa watawala wa Waislamu wanaozuia majeshi ya Waislamu kutekeleza wajibu wao. Ni wajibu kwa majeshi haya kuvunja safu, kusonga kwa ajili ya Gaza na kutoa Nusra - msaada wa kivitendo - kwa wale wanaofanya kazi kwa ikhlasi kwa ajili ya Khilafah, kwanza kabisa kwa Hizb ut Tahrir. Faradhi hii inaondoa dhimma kutoka kwa dhamiri ya kila Muislamu aliye na hamu ya kuwasaidia wanaodhulumiwa na kuyahami matukufu ya Uislamu. Hii ndio hatua madhubuti.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24]

Haitham Ibn Thbait
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir in Amerika

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Amerika
Address & Website
Tel: 
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Amerika Yala Sanamu Lake Yenyewe!

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu