Jumapili, 25 Muharram 1447 | 2025/07/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Tatizo la Umeme wa Ghali Halitatuliwi kwa Kupunguzwa kwa Malipo ya Nyuzi za Umeme na Majadiliano Mapya ya Mikataba Pekee. Suluhisho ni Kukomeshwa Kabisa kwa Ubinafsishaji katika Sekta ya Kawi, kwa mujibu wa Amri ya Mwenyezi Mungu (swt)

Kutolewa kwa data kuhusu malipo ya nyuzi za umeme kwa mitambo ya kuzalisha umeme na aliyekuwa waziri wa muda wa biashara, Gohar Ejaz, kumewashangaza watu. Muundo wa kandarasi za malipo ya nyuzi za umeme, ambao thamani yake ni zaidi ya rupia bilioni 2,000, umepangwa na mashirika ya wakoloni ya kimataifa, Benki ya Dunia na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF).

Soma zaidi...

Kwa Shangwe na Nderemo ya Hali ya Juu, Bunge la Marekani Lilimkaribisha Muuaji wa Gaza!

Baada ya miezi kumi ya mauaji ya kila siku dhidi ya watu wa Gaza, ambayo yanatangazwa muda baada ya muda kwa sauti na picha za hali ya juu, kwa idadi, takwimu, ushuhuda na hukumu za mahakama... baada ya yote hayo, Bunge la Congress lilimpokea kiongozi wa Baraza la Vita huko Gaza, Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi Netanyahu, kwa karamu ya nderemo na shangwe kana kwamba yeye ni mmoja wa mashujaa wa watu wao. Sauti yao ya ndani ikisema: Tunataka kukupa ujira, Netanyahu, kwa kuwaua Waislamu wa Gaza kwa niaba yetu.

Soma zaidi...

Ajenda ya Mapinduzi ya Uislamu Kurekebisha Uchumi wa Pakistan, Baada ya Kuharibiwa kupitia Sera za Wakoloni

Utabikishaji wa sera za wakoloni umeharibu uchumi wa Pakistan, ambao una rasilimali nyingi sana. Kwa hatua na vipimo vyote, serikali na watu wa Pakistan wako kwenye ukingo wa kufilisika. Madeni ya mzunguko wa sekta ya nishati na bili za umeme haziwezi kumudika. Licha ya ongezeko la mara nne la ukusanyaji wa ushuru katika miaka tisa iliyopita, nakisi ya kifedha ya bajeti ya shirikisho, ya rupia bilioni nane na nusu, inazua maswali mazito kuhusu uwezo wa serikali.

Soma zaidi...

Mkono wa Umbile Halifu Wavamia nchi Yetu ya Yemen na ash-Sham chini ya Njama za Tawala na Kukosekana kwa Uzuiaji

Ndege za umbile halifu la Kiyahudi zilianzisha msururu wa mashambulizi ya kichokozi dhidi ya Yemen. Wakati wa mkutano wake jana, Baraza la Mawaziri la umbile hilo linalohusika na masuala ya usalama liliidhinisha shambulizi hilo dhidi ya Yemen, kwani uvamizi huo ulilenga vituo vya kuhifadhi mafuta na kituo cha umeme katika bandari ya Hodeidah.

Soma zaidi...

Kama Umma Mmoja: Waislamu Wanasimama pamoja na Watu wa Bangladesh Dhidi ya Dhalimu Sheikh Hasina

Watu wa Bangladesh—zaidi ya 92% yao ni Waislamu na sehemu ya mojawapo ya Waislamu wengi zaidi duniani—wamejitokeza katika maandamano ya amani yanayoongozwa na wanafunzi dhidi ya dhalimu Sheikh Hasina. Maandamano ya hivi punde yalizuka baada ya serikali inayoongozwa na Hasina kujaribu kuongeza mgawo wa nafasi za kazi serikalini kwa kuwapendelea wafuasi watiifu wa serikali badala ya wagombea wenye sifa stahiki. Sera hii ni ya hivi punde tu katika mfululizo wa vitendo vya rushwa na uonevu vinavyofanywa na serikali ya Awami League tangu iingie mamlakani mwaka wa 2009.

Soma zaidi...

Waislamu wa Pakistan Wanashikiliwa Mateka na Watawala kwenye Mpango Angamivu wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa

Mnamo tarehe 13 Julai, 2024, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ulithibitisha katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba Pakistan na IMF wamefikia makubaliano ya kifurushi cha mkopo wa msaada wa dolari bilioni 7, wakidai kuwa “Programu hiyo mpya inalenga kuunga mkono juhudi za mamlaka za kuimarisha utulivu wa uchumi mkuu.”

Soma zaidi...

Serikali nchini Jordan Inatumikia Malengo ya Kikoloni ya NATO: Jaribio Lililofanywa Upya la Kuitenga Jordan kutoka kwa Ummah Wake wa Kiislamu

Wizara ya Mambo ya Nje na Wageni ya Jordan ilitangaza kuanzishwa kwa Afisi ya Mahusiano ya NATO (North Atlantic Treaty Organization) katika Ufalme huo, ambayo itachangia kuimarisha uhusiano wa ushirikiano na muungano huo. Wizara hiyo ilitoa taarifa ya pamoja na NATO kuhusu uamuzi wa kufungua afisi hiyo jijini Amman.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu