Jumapili, 20 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Mashambulizi ya "Warefu Tisa" yatamalizwa tu kwa Utekelezaji wa Adhabu za Sharia chini ya Dola ya Khilafah

Habiba Al-Amin, mwandishi wa habari wa tovuti ya Kush News, alishambuliwa vikali na wanachama wa genge la "Warefu Tisa" katika eneo la kivuko kwenda Port Sudan alipokuwa akiregea kutoka kwenye uangaziaji wa habari akiwa na wenzake kadhaa. Hili ni moja tu ya matukio mengi ya uporaji, ujambazi na mauaji katika miji inayodaiwa kuwa salama, kama vile Omdurman, Khartoum, na sasa mji mkuu wa utawala, Port Sudan. Hii ni miji iliyo chini ya udhibiti wa serikali na vyombo vyake vya usalama.

Soma zaidi...

Ziara ya Azerbaijan: Hatua kuelekea Kusukuma Uhalalishaji Mahusiano na Umbile la Kiyahudi Ambayo Itakuwa ni Mchomo wa Kisu ndani ya Moyo wa Ummah

Chanzo cha kidiplomasia jijini Damascus kilisema mnamo Jumamosi kwamba mkutano wa moja kwa moja utafanyika kati ya afisa mmoja wa Syria na afisa mwengine wa 'Israel' huko Baku kando ya ziara ya Rais wa Syria Ahmad Al-Shara nchini Azerbaijan, kulingana na shirika la habari la Agence France-Presse (AFP).

Soma zaidi...

Mauaji ya Kikatili ya Sohag katika eneo la Midford la Mji Mkuu Dhaka, ni Matokeo Yasiyoepukika ya Siasa za Kisekula na za Kiwendawazimu zisizomtambua Mungu

Katika eneo la Mitford la mji mkongwe wa Dhaka, baadhi ya viongozi wa eneo la Jubo Dal, wakiongozwa na chama kikuu cha kisekula cha kisiasa nchini humu BNP, walimuua kikatili mfanyibiashara wa vyuma vichakavu aitwaye Sohag (39) kwa kumdunga kisu na kumpiga na jiwe kubwa mfululizo kwa kukataa kulipa pesa za ulaghai. Walioshuhudia walisema kwamba wahalifu hao hawakuishia kumuua tu, bali waliendelea kuonyesha unyama kwenye mwili mfu wa Sohag hata baada ya kifo chake kuthibitishwa. Mwili uliojaa damu, ulioganda uliachwa katikati ya barabara na wauaji wakasimama juu ya mwili huo huku wakisherehekea kiwendawazimu.

Soma zaidi...

Mfuko wa Fedha wa Kimataifa: Chombo Mikononi mwa Makafari cha Kudhibiti Sera ya Ndani ya Nchi Inayokopa

Mnamo Jumatano, 9/7/2025, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ulionya kwamba uchumi wa Iraq unakabiliwa na changamoto kubwa. Bodi ya IMF, katika taarifa yake ya kuhitimisha mashauriano ya Kifungu cha IV na Iraq, ilisema kuna nafasi ya kuimarisha mapato yasiyo ya mafuta kupitia ongezeko la kodi na ushuru wa forodha.

Soma zaidi...

Enyi Waislamu: Yaelekezeni macho yenu kwenye makasri ya watawala wenu, sio Ikulu ya White House!

Macho ya Waislamu kwa jumla, na waandishi wa habari, wachambuzi, waangalizi, na wale wanaohusika hasa, yanaelekea Ikulu ya White House, na kwenye matokeo ya mikutano ya Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi, Benjamin Netanyahu. Je, Trump atamshinikiza Netanyahu kukubali kwa upole kusitisha vita vyake dhidi ya Gaza?

Soma zaidi...

Usaliti wa Watawala wa Pakistan na Kukumbatia Kwao Uhalalishaji wa Mahusiano: Utangulizi wa Kujiunga na Mkataba wa Khiyana wa Abraham na Kutumikia Maslahi ya Amerika ya Trump na Umbile la Kiyahudi

Marekani ya Trump sasa inajitahidi kuunda "Mashariki ya Kati Mpya," ambayo inatumikia maslahi ya Marekani katika kanda hiyo, shauku kuu ikiwa ni kuhakikisha amani, usalama, na upanuzi wa kambi ya kijeshi ya Amerika katika Ulimwengu wa Kiislamu, inayojumuishwa ndani umbile la Kiyahudi. Inatafuta kuliweka umbile la Kiyahudi kama mamlaka kuu katika eneo hilo kisiasa, kiuchumi, na kimfumo. Licha ya haya yote, vibaraka wa Amerika ya Trump wamekimbilia kutekeleza mradi huu, na kutumikia maslahi ya bwana wao.

Soma zaidi...

Ajali za Barabarani nchini Misri: Ushahidi Tosha wa Kukosekana kwa Ustawi wa Jamii na Ufisadi wa Mfumo wa Kirasilimali

Katika tukio ambalo limekuwa la kusikitisha, watu waliamka siku chache zilizopita na kushuhudia maafa mengine ambayo yalisababisha vifo vya watu tisa wasio na hatia katika ajali iliyotokea kwenye Barabara ya Kanda katika Jimbo la Monufia, chini ya wiki moja baada ya maafa ya kuhuzunisha ambapo wasichana wachanga kumi na nane waliangamia katika ajali sawia, ikitofautiana na ile ya awali tu na kwa idadi ya wahasiriwa. Barabara ya Kanda - ambayo serikali imekuwa ikiitangaza kwa muda mrefu kama "mafanikio ya kitaifa" - imekuwa shahidi wa kudumu wa upuuzi wa yale yanayodaiwa kuwa mafanikio yanayosifiwa na watawala huku wakijificha nyuma ya mabango ya vyombo vya habari vya uwongo na kupuuza haki msingi ya watu: kuishi kwa usalama kwenye barabara ambazo hazinyakui maisha yao.

Soma zaidi...

Utambuzi wa Urusi wa Serikali ya Afghanistan: Hatua Zaidi ya Kuzuia Kuibuka kwa Mfumo wa Kiislamu katika Kanda hii

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan inauona utambuzi huu kama sehemu ya mchakato mpana ambao kwao utawala wa sasa utayeyushwa hatua kwa hatua ndani ya mfumo wa kimataifa wa kisekula wa dola ya kitaifa. Mfumo huu, baada ya muda, utaiweka mbali serikali hii na lengo kuu la Kiislamu la kusimamisha na kubeba Dini ya Mwenyezi Mungu (swt). Zaidi ya hayo, utambuzi huo unaweza kuigeuza Afghanistan kuwa uwanja wa vita vya kiushindani kati ya dola za kikanda na kimataifa.

Soma zaidi...

Mjadala juu ya Upandaji wa Malori ya Kuhitimu Unafichua Chuki iliyokithiri ya Vyombo vya Habari na Wanasiasa wa Denmark dhidi ya Uislamu

Wiki hii iliyopita kumeshuhudiwa vurumai kubwa la vyombo vya habari na kisiasa kutokana na machapisho ya mitandao ya kijamii ambapo Waislamu waliwapongeza wahitimu wa mwaka huu huku pia wakiwasilisha mtazamo wa Kiislamu kuhusu kupanda malori ya kuhitimu yenye sifa ya ulevi na tabia mbaya.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu