Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
H. 4 Dhu al-Qi'dah 1446 | Na: Afg. 1446 H / 14 |
M. Ijumaa, 02 Mei 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hatua Mpya za UN na za Kanda za Kuoanisha Serikali Tawala ya Afghanistan ndani ya Mfumo wa Kisekula wa Dunia
(Imetafsiriwa)
Katika siku za hivi karibuni, Umoja wa Mataifa umekuwa ukifuatilia shughuli zake nchini Afghanistan kwa kasi zaidi kuliko hapo awali. Ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Kibinadamu jijini Kabul na Kandahar, pamoja na mwaliko wa Amir Khan Muttaqi-Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali tawala nchini Qatar, inaashiria juhudi mpya za kuendeleza mipango ya kimataifa na kushawishi serikali ya Afghanistan.
Kutokana na hali hii, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan inaangazia maoni kadhaa muhimu:
Ni dhahiri kwamba kile kinachojulikana kama "ramani ya utendakazi" ya Umoja wa Mataifa - yenye lengo la kuoanisha serikali tawala ya Afghanistan katika jumuiya ya kimataifa ya kisekula - imekumbana na changamoto kubwa za utekelezaji na imesimama. Hii ni kwa sababu uongozi wa utawala huo, kinyume na matarajio ya Magharibi, umekataa kukumbatia mabadiliko ya kimsingi katika mtazamo wake. Licha ya kufeli huko, Magharibi, ikiongozwa na Marekani, haiko tayari kunyamaza. Kutokana na hali hiyo, mipango mipya imeibuka ili kutekeleza azma hiyo hiyo kupitia njia badali. Kotovu cha juhudi hizi ni mkakati wa kuioanisha serikali hatua kwa hatua katika mfumo wa sasa wa kilimwengu kupitia ushiriki uliokokotolewa—kumomonyoa kitambulisho chake cha Kiislamu hatua kwa hatua.
Amerika inaendeleza ramani hii ya utendakazi kupitia mbinu mbili za shinikizo na ushawishi—karoti na fimbo. Wakati fulani, hutenda moja kwa moja kwa kuwaondoa watu binafsi katika orodha ya vikwazo au kutoa motisha za kisiasa. Wakati mwingine, inakaza skrubu kwa kusitisha misaada ya kimataifa. Kando na vitendo hivi vya wazi, Washington inaendeleza ajenda hiyo kimya kimya kupitia waamuzi kama Umoja wa Mataifa na nchi kama vile Qatar. Mbinu nyingine inayotumiwa ni kuugawanya utawala kindani kwa kuainisha watu wake kama "wenye msimamo wa kati na kati" au "wenye msimamo mkali," kwa nia ya kudhoofisha mshikamano wake na kusukuma sehemu zake kuelekea kwenye upotovu zaidi, unaoitwa Uislamu poa.
Qatar, ambayo kwa muda mrefu inatazamwa kama kitovu cha wakala wa Magharibi katika kanda hii, inacheza dori kuu katika ujanja huu wa kisiasa. Kwa uratibu na Umoja wa Mataifa, inalenga kukabiliana na mizozo ya enzi ya Trump kwa kupeana mirengo fulani ndani ya serikali vishawishi vya kidiplomasia na kisiasa. Athari za juhudi hizi sasa zinaonekana waziwazi katika matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nje Amir Khan Muttaqi. Katika mahojiano ya hivi karibuni na Al Jazeera, alihimiza jumuiya ya kimataifa kuibadilisha Afghanistan kuwa nafasi ya "ushindani chanya wa kiuchumi." Ilhali historia na uzoefu wa kisasa unaonyesha kwamba ushindani kama huo wa kiuchumi katika mataifa dhaifu mara nyingi hutumika kama kielelezo cha kupenya kwa wageni, utegemezi, na hatimaye, ukoloni wa kiuchumi.
Akizungumzia juu ya Palestina, Waziri wa Mambo ya Nje alisema: "Tuna wajibu wa kimaadili kwa Palestina." Kiukweli, hata hivyo, jukumu la Waislamu—hasa watawala wao—kwa Palestina sio la kimaadili au kihisia tu; ni faradhi ya kisheria katika Shariah. Watawala wa Waislamu wana wajibu wa kuyakusanya majeshi yao katika kuwatetea wanaodhulumiwa, na sio kujificha nyuma ya lugha ya kinadharia ya kimaadili kama njia ya kukwepa hatua halisi. Hisia hii ya hasira ya kimaadili imedhihirishwa zaidi na baadhi ya wasiokuwa Waislamu katika nchi za Magharibi—wale walioingia mitaani au, kama vile askari wa Kimarekani aliyejiteketeza moto nje ya ubalozi wa ‘Israel’.
Kwengineko katika mahojiano hayo hayo, Amir Khan Muttaqi alitoa wito kwa Donald Trump kuonyesha "ujasiri wa kisiasa" kuhusu Afghanistan. Lakini ukweli ni kwamba kila mtu na kila taifa huonyesha ujasiri kwa kadiri ya imani yake katika maadili yake. Ikiwa Trump atachukua hatua kwa ujasiri, itakuwa kutumikia maslahi yake mwenyewe. Swali ni je: yuko wapi mtawala wa Kiislamu—anayesimamia Dini ya Uislamu, anafanya kazi kwa ajili ya kuisimamisha, na haogopi lawama au matokeo? Ni mtawala wa Kiislamu ambaye lazima awe na ujasiri wa kusimamisha tena Khilafah Rashida kwa njia ya Utume na kufuata sera ya kigeni inayoegemezwa katika Da’wah na Jihad. Ndiyo, kutangaza haki ya Uislamu kunahitaji ujasiri—na huu ndio ujasiri tunaoutafuta kutoka kwa watawala wetu.
[الَّذِينَ يُبَلِّغُونَ رِسَالَاتِ اللَّهِ وَيَخْشَوْنَهُ وَلَا يَخْشَوْنَ أَحَدًا إِلَّا اللَّهَ]
“(Hao wa zamani) walio kuwa wakifikisha risala za Mwenyezi Mungu na wanamwogopa Yeye, na wala hawamwogopi yeyote isipo kuwa Mwenyezi Mungu.” [Al-Ahzab:39]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Afghanistan |
Address & Website Tel: http://hizb-afghanistan.org/ |
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org |